Ukweli ni upi baada ya kuoa au kuolewa

Ukweli ni upi baada ya kuoa au kuolewa

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
jamani duniani kuna mambo ,juzi nilikutana na mzee akanambia yatawkisha ukishaoa ,nilimfungulia mlango mdada mmoja , nilipozunguuka kwenye mlango wa usukani ndipo njemba hiyo ikarusha dongo ila nikamjibu lady is first hao tukaondoka.

Ila sikulala uzingizi mnono nikifikiria yale maneno kuwa kuna nini baada ya ndoa ladha na utamu wa maisha kabla ya ndoa huwa unabadilika,yaani itakuwa hakuna tena kufunguliana milango na menginemengi yatakuwa hayafanyki tena au najizonga tu ?
Embu wakuu tuelezeni tuyajue na mapema ! Mapenzi huzidi au hupungua ? Au ni aina nyengine ya mapenzi yaani nimechanganyikiwa kabisa.
 
Mwaego usisikilize maneno ya mtaani hayo, we endelea kumpenda gal wako mpaka ndani ya ndoa. Mambo yatakuwa matamu zaidi ukiingia ndoani
 
Halafu kuna msemo ule usemao ndoa ndoana ,yaani we wacha tu !
 
ndoa ikijengwa ktk misingi artificial, tegemea hayo mambo kuisha hata kabla ya mwezi sukari kuisha. so marriage depends on how you couples make it
 
Hilo gari lako mlango ni mbovu au mzima? Jibu Hili swali la kwanza tujue tunaanzia wapi kukushauri

Huu ni ujumbe ukalale nao leo

,
"Ndoa nyingi hazidumu kwa kufuata maisha ya tamthilia"
 
Ndugu yangu umeongea kitu kikubwa sana hapo chini. Mia
 
Hilo gari lako mlango ni mbovu au mzima? Jibu Hili swali la kwanza tujue tunaanzia wapi kukushauri

Huu ni ujumbe ukalale nao leo

,
"Ndoa nyingi hazidumu kwa kufuata maisha ya tamthilia"

Gari ni zima BMW 325i ,milango yote ni mizima na hayo maisha ya tamthilia ndio yepi mbona ni msemo mpya kwangu ?
 
Ukweli ni kwamba kulala bila pichu litakuwa jambo la kawaida kwenu.
 
jamani duniani kuna mambo ,juzi nilikutana na mzee akanambia yatawkisha ukishaoa ,nilimfungulia mlango mdada mmoja , nilipozunguuka kwenye mlango wa usukani ndipo njemba hiyo ikarusha dongo ila nikamjibu lady is first hao tukaondoka.

Ila sikulala uzingizi mnono nikifikiria yale maneno kuwa kuna nini baada ya ndoa ladha na utamu wa maisha kabla ya ndoa huwa unabadilika,yaani itakuwa hakuna tena kufunguliana milango na menginemengi yatakuwa hayafanyki tena au najizonga tu ?
Embu wakuu tuelezeni tuyajue na mapema ! Mapenzi huzidi au hupungua ? Au ni aina nyengine ya mapenzi yaani nimechanganyikiwa kabisa.

Ladies First.......
 
Wasikutishe...! Oa tuje kula pilau bana...
 
Ladies First.......

Una uhakika ,maana alikuwa mmoja halafu nilimjibu mtu ! labda wanojua lugha hii ya kigeni watusaidie hapa naona kuna mvutano wa luga !
 
We unaonaje kwani? Haya ni mambo binafsi, ukiamua kuendelea nayo baada ya kuoa au kuacha ni uamuzi. Sioni kwa nini maneno ya mtu mmoja yakupe presha kiasi hicho.
 
Ukifanya jambo lolote kwa mapenzi ya dhati kwa girlfriend wako, hata ndani ya ndoa utayafanya hayo hayo kwa mapenzi ya dhati. Kinacho matter ni upendo tu kwa mpenzio.
 
Inshu sio utakuta nini kwenye ndoa yako bali ni nini unataka ukuye kwa sababu ndoa ni wewe na umpendae. Nyote wawili mnajukumu LA kuifanya ndoa I we nzuri au mkaibomoa.
 
Back
Top Bottom