Bwana Mwiba. Maisha ni safari ndefu, maisha ya ndoa yana milima na mabonde, lazima utapanda na kushuka. Maisha ya uchumba kwa wengi wetu huwa yamejaa bashasha nyingi mno, hufanya watu wakafikiria kwa nini walichelewa kupata mchumba au rafiki wa jinsia tofauti. Kipindi cha uchumba kila mmoja huficha kabisa makucha yake ili yasije yakaharibu mahusiano. Ngoja mfunge ndoa na baada ya muda kupita, tabia halisi huanza kujitokeza. Mwanaume mlevi anaanza kuchelewa kurudi nyumbani tofauti na awali. Mnaanza kuonana wa kawaida tofauti na zamani, aliyeko nje unamuona mzuri kuliko mke wako au mume wako. Mungu aliyaona hayo akasema USITAMANI KITU CHA JIRANI YAKO, HATA MKE WAKE NA MTUMISHI WAKE, NA CHOCHOTE ALICHONACHO JIRANI YAKO. Baada ya mwaka mmoja mke amejifungua mtoto, asilimia 80 ya mapenzi ya mama yanahamishiwa kwa mtoto, wewe unabaki mpweke, unapomhitaji mkeo awe karibu na wewe, yeye anakuwa bize na mtoto. Ndio mwanzo wa kuanza kwenda chobizi. Mapenzi yanakwisha inabaki mazoea. Ndoa zina mambo mengi sana ila inategemeana na umahiri wenu, mume na mke mtakavyoweza kulinda ndoa yenu pasipo kutetereka. Usiogopeshwe na maneno ya wana jf. Ingia kwenye ndoa pasipo woga.