Ukweli ni Kujua na kutambua hali halisi na kutoa utata wa sintofahamu. Knowing, casying the shadow of doubt, replacing belief with knowledge.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kweli kinyume cha Uwongo. Biblia imesema Mungu ni Kweli na Shetani ni Baba wa Uwongo. Yesu alisema yatupaswa kumuabudu Mungu kwa Njia ya Roho na Kweli. Kuijua kweli lazima tupate picha halisi ya Uwongo kwani kinyume chake cha Uwongo ndio Kweli. Kwa mfano nikikuuliza jee unajua rangi ya Kinyonga? Hakuna anaeijua Rangi halisi ya Kinyonga kwani inabadilika kila inapotokea hali ya mabadiliko ya mazingira yanayo mzunguka.
Kutokuwa halis, na kubadilika ndio tunaita hali ya uwongo. Haijalishi madailiko hayo ni ya muda mfupi au mrefu ilimradi kuna uwezekano wa kutokea mabadiliko ya aina yeyote ile au mabadiliko ya msimamo basi huo ni uwongo.
So long jiwe linaweza kubasilika na kuwa kokoto likilipuliwa na baruti basi nalo sio halisi ni uwongo, au chuma hakikuwa kilivyo kimebadilika kutoka Iron ore basi sio halisi ni uwongo, mbao ilikuwa mti, ambao ulikuwa kambegu kaliko jipanda aridhini na kuvyoza virutubisho udongo hivyo sio halisi ni uwongo.
Kwa utambuzi wetu twaona kuwa vitu vyingi vina hali ya kweli wakati sio. Mfano hali ya maji, maji yana hali ya kimiminika, lakimi ukiyaweka kwenue jokofu yanaganda na kuwa barafu, ukiyachemsha yanapata moto, na joto likipanda ya kuwa mvuke na kukauka. Kama rangi ya kinyonga maji hali ya maji hubadirika hivyo ni hali ya uwongo.
Ukweli ni ile hali kuwa bila mabadiliko ya aina yeyote katika hali yeyote, kwa jua, kwa mvua, au kwa muda, au mahali uliopo ni hali ya milele. Ukweli uko kama ulivyo sasa, kabla ya sasa, na baadae, Ukweli ni hali ya umilele.
Kweli ni Uhai na Uwongo na Maumbile yake.
Binadamu ana nafsi mbili, ananafsi ya kweli ambayi ni Roho na nafsi ya uwongo ambayo ni Mwili. Roho haina mwanzo wala mwisho, lakini mwili una mwazo na mwisho, unakua na kuzeeka, unazaliwa na kufa.
Ndio maana YESU anataka tumwabusu Mungu kwa Njia ya Kweli yaani Kwa Roho zetu kwa Mungu Roho.
Kila unachokiona, unachokitamani kukipata, kula, kunywa, kuzini au kufurahi nacho ni vyo uwongo. Hivyo vinakinaisha, havikidhi matarajio, haviridhishi.