Ukweli ni kama ifuatavyo,
Unajiandikisha na kuwaandikisha marafiki/ndugu zako kama "wafuasi" wako. Sasa hizi details wanazopokea ni deal kwao kwani washapata chambo wakuwatumia hapo baadae, kumbuka kuwa hawa wamejiandikisha au kuandikishwa na "marafiki" zao kuwa wanapenda kupata haya mapesa bila kutoa jasho. Sasa biashara kama hizi wanakuwa na category za "wajinga" kama ifuatavyo,
Yule wa kwanza kuandikisha yeye ni chambo 100%, ameamini kuwa ndio atafaidika na hii kitu kwa hiyvo value yake ni kubwa sana kwao, baada ya kumtumia statistics ambazo hazina kichwa wala miguu ataona kuwa kweli hivi punde atapata utajiri wa kufa mtu. Sasa hapo ndio "business" itakapoanza, watamtumia e-mail kuwa sasa "wafuasi" wake wametimia na asubiri fungu lake ma mapesa, muda sio mrefu atapata barua nyingine kuwa mambo yote yanaendelea vizuri, na kumkumbusha awahimize wafuasi wake kutafuta wajinga wengine, pia wafuasi wote watapata e-mail kuwa "bosi" wenu fungu lake lipo njiani. hizi e-mails zitakuwa nyingi tu kuwa sasa pesa ipo tayari lakini atahitajika kutuma administration fee ndio ile pesa iwe released. Kumbuka wafuasi wapo mbioni kwani wanaona mapesa mbele yao na wao wanawahimiza wengi zaidi..
Nadhani ushanipata, ile release money ndio dili yao, kiongozi atachukua muda kidogo kuwaambia wafuasi kuwa jamani nimeliwa, na hii shame ndio watakayoitumia kuficha siri yao...
Kama unazo za kupoteza, basi jiunge wazzup...