Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ni Rais Halali, Uchaguzi ni 2020!

Maalim alipewa nafasi ya kushiriki uchaguzi ili kuhakikisha kwamba alishinda kama alivyodai, akasusa! Maalim ni Bingwa wa kupoteza muda wa wenzake. Uchaguzi umeshakwisha. Sasa tunajenga nchi!
Inajulikana tayari, CCM imekwapua ushindi wa CUF ili itimize lengo la kuipitisha ile Katiba ya Chenge/ Sitta. Kwa maneno ya Pro-pesa Lipumba, "Katiba ya ma-intarahamwe".
Lakini pia CCM kukubali kuachia madaraka Zanzibar ni kaburi la CCM kwa utawala wa CCM bara(Tanzania). Pia CCM kung'ang'ania serikali mbili 2 ndio njia inayokamilisha ule mduara ambao CCM Zanzibar inaitegemea CCM bara na CCM bara inanuafaika kutokana na kuibeba CCM Zanzibar na kuisimika madarakani.

Naomba ili kufahamu mduara (cycle)huo na mazingaombwe ya CCM na serikali mbili soma hizi mada:
Link Kura Ya Maoni Na Hatima Ya Muungano

Link2. CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Link3. CCM: Mwaka 1993 Tanganyika Ruksa, Mwaka 2014 Tanganyika Sio Ruksa

Link4. Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla

Link5. Tuache Kuwatisha Wazanzibari Kuhusu Udogo wa Taifa Lao na Hatima Ya Muungano

Link6. Mdahalo: Kipi Ni Sumu Ya Muungano - Je, Ni Kwa Kuikataa Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Tanganyika?

Link7. Hoja Mbadala: Katiba Ya Muungano Kuja Kabla ya Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara) ni Makosa!

Je mgogoro anaouleta Lipumba (ndani ya CUF na hatimaye UKAWA) akisaidiwa na Msajili wa vyama na mkono uliojificha una agenda kubwa na pana zaidi?
 
Uliepost hii habari unakaa ZANZIBAR au unapajua? Hivi kweli hakuna mgogoro? Au umetumwa na CCM? Au ndo chsma chako?.... Kiukweli ZANZIBAR hali sio nzuri na mgogoro bado uko maana viongozi wa CCM wiki ya tatu hii huweka vikao kujadili hali ya ZQNZIBAR tena wastaafu na magwiji wa CCM.. WAZANZIBAR wamekufa kifikra kasoro uhai 2 kwa dhulma tuliotendewa... Na unasema CCM iko madarakani kihalali hemu nipe vifungu vya kikatiba kuhusu uhalali wa ughairishaji matokeo na urudiaji? HAPO NDO UTAPOJUA KUWA WEWE ULIEPOST HUKO SAWA KIAKILI.... but wakati ni adui tena asiepigika... Waache wanaojua ZANZIBAR waongee yanayoendelea na sio wewe ulietumwa na CCM.. BULLSHIY
 
Inajulikana tayari, CCM imekwapua ushindi wa CUF ili itimize lengo la kuipitisha ile Katiba ya Chenge/ Sitta. Kwa maneno ya Pro-pesa Lipumba, "Katiba ya ma-intarahamwe".
Lakini pia CCM kukubali kuachia madaraka Zanzibar ni kaburi la CCM kwa utawala wa CCM bara(Tanzania). Pia CCM kung'ang'ania serikali mbili 2 ndio njia inayokamilisha ule mduara ambao CCM Zanzibar inaitegemea CCM bara na CCM bara inanuafaika kutokana na kuibeba CCM Zanzibar na kuisimika madarakani.

Naomba ili kufahamu mduara (cycle)huo na mazingaombwe ya CCM na serikali mbili soma hizi mada:
Link Kura Ya Maoni Na Hatima Ya Muungano

Link2. CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Link3. CCM: Mwaka 1993 Tanganyika Ruksa, Mwaka 2014 Tanganyika Sio Ruksa

Link4. Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla

Link5. Tuache Kuwatisha Wazanzibari Kuhusu Udogo wa Taifa Lao na Hatima Ya Muungano

Link6. Mdahalo: Kipi Ni Sumu Ya Muungano - Je, Ni Kwa Kuikataa Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Tanganyika?

Link7. Hoja Mbadala: Katiba Ya Muungano Kuja Kabla ya Katiba ya Tanganyika (Tanzania Bara) ni Makosa!

Je mgogoro anaouleta Lipumba (ndani ya CUF na hatimaye UKAWA) akisaidiwa na Msajili wa vyama na mkono uliojificha una agenda kubwa na pana zaidi?
Sahihisho, sio CCM ndiyo inayongangania bali ni matakwa ya wananchi yaliyowengi ndiyo yanayoprevail!
 
Nimefanya skim reading.
Ni ukweli ulio wazi na ni lazima tuukubali.
Mataifa ya magharibi ni opportunists huku wakiangalia maslahi yao na ndio maana Saudi Arabia ni rafiki yao pamoja na kuwa hawana demokrasia ya kimagharibi.
Ukweli ni kuwa CCM ipo madarakani Zanzibar na Shein ndiye Raisi wa nchi hiyo lakini ni kipi kimo ndani ya nyoyo za watu?Watakubali hivi mpaka lini?Majeshi yatapelekwa Zanzibar katika uchaguzo mpaka lini?Je kuondoka kwa Seif katika ulingo wa siasa kunaweza kupunguza joto?
Je wamekubali kwa dhati ya nafsi yao?Hapo ndipo mgogoro ulipo na ndipo ambapo watawala wanapaogopa.Aliyedhulumu hana amani abadani!!!
Kabisa kabisa. Halafu Mh. Shein mwenyewe na hivi sio wa maneno mengi anapiga tu kazi. Zanzibar imebadilika. Zanzibar inaendelea. Miaka mi3 niliyofika Zanzibar kwa amara ya kwanza si ya sasa. mageuzi makubwa yamefanyika serekalini kuondoa watu wanaofanya kazi kwa mazoea. Go Mh. Shein Go!
 
CUF ni chama cha siasa cha ajabu sana, lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola, hilo jambo lolote litakalo sababisha chama hicho kisishike dola ndio the most important thing with first priority! .

Uchaguzi wa October 25, CUF Ilishinda uchaguzi huo kihalali, Jecha akafuta matokeo kiubatili, this was the most important issue ya kuifungulia kesi.

Ukatangazwa uchaguzi mwingine wa marudio ambao ni uchaguzi batili, CUF badala ya kwenda mahakamani kuusimamisha, wao wakaamua kususa na kumwachia ngedere shamba la mahindi! .

Hizo ni issue muhimu sana zilizoikwamisha CUF kushika dola.

Issue ya Lipumba kujiuzulu CUF ni straight forward Lipumba alikwisha jiuzulu na vikao halali viliisha ridhia kujiudhuru kwake lakini hawakufuata utaratibu wa kujibu barua yake ya kujiuzuli. Hili ni kosa kubwa la kiutendaji. Barua ya Msajili sio maelekezo ni maoni tuu. Hiyo sio issue kubwa kivile ni issue ndogo tuu ya kuchukua polisi Kituo cha Buguruni kwenda kuwatimua wahuni fulani waliovamia ofisi Kuu ya CUF wakiongozwa na muhuni mmoja aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa CUF lakini alijiuzulu mwenyewe na kufukuzwa rasmi CUF na sio mwanachama tena.

Kumbe CUF wanaweza kufungua kesi, kwa nini hawakufungua kesi kwenye mambo muhimu? .

Paskali
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Haya ni maoni yangu katika kutekeleza uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yangu, na justification why me au mtu asiye Mzanzibari kuzungumzia issue za Zanzibar, hii ni kufutia mimi Paskali ambaye ni raia wa Tanzania, yuko huru kutoa maoni yake yoyote kuhusu jambo lolote la nchi yetu ikiwemo Zanzibar ambayo ni sehemu ya JMT, na pesa ya jasho langu kupitia kodi yangu, ndiyo inayotumika sio tuu kugharimia kuiendesha SMZ, bali hadi kuvigharimia nyama ikiwemo CCM na CUF ambayo vinatafuna tuu pesa yetu.

Hivyo nina haki na mamlaka yote kuhoji au kuzungumzia lolote kuhusu matumizi ya kodi yangu, na tayari nimeishamshauri Rais Magufuli, akiona vipi, afutilie mbali ruzuku kwa vyama vya siasa, ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote.

Sasa tuje kwa Zanzibar, tulipoungana tulikubaliana kuchangia gharama za kuendesha muungano, lakini zigo lote la muungano amebebeshwa mtu mmoja tuu, huku mwingine akibweteka kazi yake ni kubebwa tuu!, haiwezikani kuendelea kuishi kwa kujidai tuko sawa na tuna haki sawa ndani ya muubgani, huku mmoja akimenyeka na kutoka jasho, huku mwingine akiishi kama kupe!.R
uzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli Aifutilie Mbali?.

Habari Kuwa Zanzibar Kuna Mgogoro wa Kisiasa, Sasa ni Kelele!.
Kadri siku zinavyokwenda, bado kunajitokeza watu wanaendelea kuaminishwa kuwa Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa, na kuwa, kuna kitu kitafanyika ili kuutanzua mgogoro huo very soon!. Hao watu wanaoaminishwa, wanamini kuwa ni kweli Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa kwa sababu wanaowaambia hivyo ni viongozi wao wanaowaamini, habari hizi za Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa, zinaposemwa sana na kurudiwa rudiwa kusemwa tena na tena kuwa Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa na kuna kitu kitafanyika kuutanzua, ila hali halisi ya kiukweli halisi kuhusu Zanzibar, ni hakuna mgogoro wowote wa kisiasa na hakuna kitu chochote kinachofanyika sasa au kitakachofanyika baadae kabla ya 2020, ni kelele tuu za mfa Maji za kuwapa watu matumaini hewa au matatajio hewa matokeo yake 2020 itafika bila lolote bila chochote, sijui wataziweka wapi sura zao?! .

Ukweli Mchungu. Zanzibar Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa.
Huu ndio ukweli mchungu kuwa Zanzibar, hakuna mgogoro wowote wa kisiasa, mgogoro ukikuwepo mwanzo uchaguzi ulipofutwa lakini baada ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, japo ulisababishwa na sababu haramu, lakini uchaguzi huo ulikuwa ni uchaguzi halali kisheria, na umeendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi huru na wa haki, hivyo matokeo yake ni halali, na mshindi halali ni Dr. Ali Mohamed Shein, hivyo anakuwa ni Rais halali wa Zanzibar, hakuna jambo jingine lolote linaloweza kufanyika chini ya jua, kubadili chochote, Uchaguzi mwingine ni mpaka 2020!.

Huu ndio ukweli mchungu kuhusu Zanzibar, the sooner you accept, the plain truth, the better!, msiendelee kudanganywa na viongozi wenu kuwa kuna kitu chochote kitafanyika, hakuna kitu kingine chochote cha kufanyika zaidi ya uchaguzi wa 2020, kinyume cha hapo ni kuendelea kuishi kwenye matumaini au matarajio hewa, yaani kuishi in a living lie, ambayo ni sawa na kuukimbiza upepo.Uchaguzi umepita, umekwisha, sasa ni muda wa kufanya kazi tuu, na ndio maana halisi ya sasa kazi, na hapa kazi tuu.

Kufuatia Watanzania kuwa ni wavivu wa kusoma makala ndefu, naomba kuikatia hapa lakini kwa wanaopenda kuzama zaidi ndani, zameni na mimi.

Jee Ni Kweli Kuna Mgogoro wa Kisiasa Zanzibar?.
Mgogoro ulikuwepo pale mwanzo kulipofutwa matokeo, na kipindi chote cha mpito, kabla ya uchaguzi wa marudio, lakini baada ya uchaguzi wa marudio na matokeo kutangazwa, hakuna tena mgogoro wowote wa kisiasa Zanzibar, hii ni kufuatia haramu hiyo ya kubatilishwa kwa matokeo halali, kutoharimishwa rasmi, na badala yake,ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliotokana na haramu isiyoharimishwa, hivyo kuwa ni uchaguzi halali.

Kwa vile uchaguzi huo wa marudio ulifuata misingi yote ya uchaguzi huru na wa haki, then matokeo ya uchaguzi huo ni matokeo halali, then hakuna mgogoro wowote wa kisiasa Zanzibar, na Dr. Shein ni Kiongozi halali wa Zanzibar, aliyechaguliwa kwenye uchaguzi huru na wa haki, uchaguzi umekwisha, sasa ni wakati wa kuchapa kazi tuu, uchaguzi mwingine ni mpaka 2020!.

NB. Kususia kushiriki uchaguzi huru na wa haki, hakubatilishi matokeo ya uchaguzi huru na wa haki.

Paskali
Ukweli huu mchungu, leo umethibitishwa na Balozi wa Marekani.
Hayo yamesemwa na kaimu balozi wa MAREKANI nchini alipokuwa anahojiwa kuhusu maamuzi yao hadi sasa.
Sikiliza mahojiano hayo hapo chini:

Tanzania ni nchi moja ya JMT, na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ni uchaguzi mmoja tuu wa kumchagua rais wa JMT uliofanyika October 25, 2015 na ulikwenda vizuri, aliyeshinda kihalali kashinda, aliyeshindwa kashindwa!.

Bahati nzuri siku hiyo hiyo ya uchaguzi, pia ulifanyika uchaguzi mwingine wa ndani tuu wa sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani, inayoitwa Zanzibar, na kilichotokea, sote tunakijua!.

Marekani haina mamlaka kuingilia mambo yetu ya ndani, mwisho wa uwezo wake ni kutoa tuu maoni na mapendekezo na sio maamuzi yoyote!.

Nimeisikiliza hiyo clip kwa makini, hakuna mahali popote wametoa uamuzi wowote kuhusu Zanzibar, alichosema ni Marekani inashikilia msimamo wake kuhusu ripoti yao ya uchaguzi mkuu, lakini wenye maamuzi ya nini kifanyike ni Wanzanzibari wenyewe!.

Tena amesisitiza kwa vile huu sio mwaka wa uchaguzi, uchaguzi mwingine ukifika, watu wajitokeze wakajiandikishe!.

Hii maana yake ni hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika Zanzibar kabla ya 2020!.

Kauli yangu hii ni kweli.
Ukweli Mchungu Zanzibar: Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa, Shein ...

Paskali
 
Kumbe CUF wanaweza kufungua kesi, kwa nini hawakufungua kesi kwenye mambo muhimu? .

Paskali
Paskali nambie ukweli nitakufichia siri yako .Hivi wewe ni Bashite wa Sheria au unajipendekeza kwa Msukuma mwenzako huenda ukaukwea? Kama wewe ni mwanasheria wa kufuzu darasani na kuielewa Katiba ya Zanzibar na sheria za Tume ya uchaguzi ya Zanzibar usingelithubutu kuandika upuuzi na utumbo huo wa Kuchanganya Mgogoro wa Uchaguzi Zanzibar na Mgogoro wa CUF na kibaraka Lipumba kwa bara.
 
Hii nchi imeshindwa kupiga hatua za kimaendeleo kwa akil kama hizi za mtoa mada,njaa kitu kibaya sana.
 
Paskali nambie ukweli nitakufichia siri yako .Hivi wewe ni Bashite wa Sheria au unajipendekeza kwa Msukuma mwenzako huenda ukaukwea? Kama wewe ni mwanasheria wa kufuzu darasani na kuielewa Katiba ya Zanzibar na sheria za Tume ya uchaguzi ya Zanzibar usingelithubutu kuandika upuuzi na utumbo huo wa Kuchanganya Mgogoro wa Uchaguzi Zanzibar na Mgogoro wa CUF na kibaraka Lipumba kwa bara.
Mkuu Baragashi, kwanza mimi sii mwanasheria bali nimesoma tuu sheria. Kusoma sheria ni jambo moja na kuwa mwanasheria ni jambo jengine!.

Kwa bahati nzuri sana, wakati mnapiga kura ya maoni nilikuwa Zanzibar, mnapitisha mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar kuingiza SUK na kujiita nchi ili kujifurahisha pia nilikuwepo Zanzibar. Kwa kifupi katiba ya nchi ambayo ni katiba ya JMT haiyatambui mabadiliko hayo ila kwa vile lengo lake ni kujifurahisha, tumekuachieni mjifurahishe, as long as Zanzibar nchi mwisho ni Chumbe, nje ya hapo nchi ni moja tuu, JMT.

Kati ya fani zote, sheria ndio the most unpredictable, kusomea sheria sio kujua sharia na kujua sharia sio kutafsiri sheria na kujua kutafsiri sheria sio kutoa haki.

Kusoma sheria mtu yoyote mwenye kujua Kusoma na kuandika anaweza Kusoma sheria.

Kujua sheria ni uwezo wa kujua jinsi hizo sheria zinatumika vipi.

Kutafsiri sheria ni kujua lengo na kusudio la watunga sheria walikusudia nini, na mwisho sheria na haki ni vitu viwili tofauti.

Ni katakana na unpredictability hii ndio maana mtungaji wa sheria ni mwingine, mtafsiri na mtumiaji ni mwingine na mtekelezaji ni mwingine.

Na ndani ya utafsiri na utumiaji kuna ngazi tofauti tofauti, ndio maana mtu unahukumiwa unakata rufaa hukumu ile inawekwa pembeni na hakimu wa hukumu iliyowekwa pembeni haambiwi kuwa ni bashite.

Nilisema CUF ni chama cha ajabu sana!. Zoezi la uchaguzi linaendeshwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Na CUF mlishina, mna wanasheria makini, what did you do?.Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Jecha kafuta matokeo ya uchaguzi halali!. Alichokifanya Jecha ni kinyume cha sheria taratibu na kanuni na zipo sheria, taratibu na kanuni za kufuatwa hili lilipotokea CUF did nothing!.
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua hatua zozote

Jecha katangaza uchaguzi mpya kinyume cha sheria taratibu na kanuni, lakini hili likifanyika, pia zipo sheria, taratibu na kanuni za kuzuia lisifanyike, CUF did nothing!. Ila waliamua kususia. Kule kususa was nothing. Tukawauliza,

Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?

Kisha tukawaambia CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Uchaguzi ukarejewa na ulikuwa huru na wa haki, mshindi akiisha tangazwa hapo ndio mwisho there is nothing anyone can do!.
Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matokeo, Tuyakubali!

Uhalali wa Rais Dr. Shein Wa Zanzibar ni Kutokana na Uchaguzi Halali, Huru na Wa Haki! .

Sasa mnalia nini?.

Paskali
 
Mkuu Baragashi, kwanza mimi sii mwanasheria bali nimesoma tuu sheria. Kusoma sheria ni jambo moja na kuwa mwanasheria ni jambo jengine!
Na waswasi usije kuniambia kusoma Kiswahili na kukielewa ni jambo jengine ikiwa unajua maana ya "kusoma", Nikisema Umesomea udaktari na ukawa si Daktari ina maana umefeli au hukufuzu. Sasa unvtoonekana wewe umefeli sheria ya msingi ambayo haihitaji tafsiri, Sheria ya Zanzibar inasema Tume ya Uchaguzi maamuzi yake hayahojiwi na chombo chochote (Mahakama) Shauri linalohusu Tume Kulipeleka Mahakamani ni kwenda kulihalalisha sio kusikilizwa.Kiungwana ni bora uendelea kuichukuia haramu kuliko kushiriki kuitakasa haramu kuwa halali.
Kwa bahati nzuri sana, wakati mnapiga kura ya maoni nilikuwa Zanzibar, mnapitisha mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar kuingiza SUK na kujiita nchi ili kujifurahisha pia nilikuwepo Zanzibar
Najua ulikuwepo Zanzibar wakati ya kura ya maoni ambayo haikukuhusu. Ulikuwa ni kati ya kundi la watu wa Tanganyika waliotumwa kuja kuharibu maoni ya Wazanzibari lakini mlishindwa kwa " nguvu za ...."
Kwa kifupi katiba ya nchi ambayo ni katiba ya JMT haiyatambui mabadiliko hayo
Sheria umefeli, Kiswahili hujui basi hata kujihoji kuwa Baina ya JMT na Zanzibar kipi kilitangulia kwanza? Zanzibar kwa vile ilikuwepo kabla ya Tanganyika haijali wala haotamani Katiba yetu kujuulikana na Tanganyika.Kiyendo cha Seyyid Baraghash kuiuza Tanganyika kwa Mjerumani ni kulitambua hili mapema.
tumekuachieni mjifurahishe, as long as Zanzibar nchi mwisho ni Chumbe, nje ya hapo nchi ni moja tuu, JMT.
Basi yote umefeli hata historia ya mama yako Tanga nyika huijui?
1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. ( ikijumuisha Mafia na fungu Mbaraka - Latham Island near Kisiju)
2. Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania

Jecha katangaza uchaguzi mpya kinyume cha sheria taratibu na kanuni, lakini hili likifanyika, pia zipo sheria, taratibu na kanuni za kuzuia lisifanyike, CUF did nothing!
Tena unajua kuwa Jecha katangaza uchaguzi mpya kinyume cha sheria taratibu na kanuni, lakini hili likifanyika,Lkini chini uangalizi mkubwa wa Majeshi yenye silaha ya Tanganyika na vifaru n maroketi launchers na , Bazooka mitaani. Damu ya Mzanzibar ina thamani kuliko utawala wa CCM
Sasa mnalia nini?.

Paskali
Zanzibar hailii na wala haotolia kabla ya kuona Machozi ya wa Tanganyika kwanza. Kuona viuno vya watanganyika vimekondeana kwa kuza mikanda hapo labda macho ya wazanzibari yatakuwa na malengelenge.
 
Na waswasi usije kuniambia kusoma Kiswahili na kukielewa ni jambo jengine ikiwa unajua maana ya "kusoma", Nikisema Umesomea udaktari na ukawa si Daktari ina maana umefeli au hukufuzu. Sasa unvtoonekana wewe umefeli sheria ya msingi ambayo haihitaji tafsiri, Sheria ya Zanzibar inasema Tume ya Uchaguzi maamuzi yake hayahojiwi na chombo chochote (Mahakama) Shauri linalohusu Tume Kulipeleka Mahakamani ni kwenda kulihalalisha sio kusikilizwa.Kiungwana ni bora uendelea kuichukuia haramu kuliko kushiriki kuitakasa haramu kuwa halali.
Kujua kusoma ni jambo moja na kuelewa ulichosoma ni jambo jingine.

Yes unaweza kusomea udaktari bila kuwa daktari. Kusomea udakitari ni kuhudhuria masomo ya udaktari, ukiisha fuzu unatakiwa kupitia internship ndipo unapewa leseni ya kuwa daktari inayokuruhusu kutibu watu. Kuna madakitari kibao waliohitimu udakitari lakini hawatibu watu.

Kama ilivyo kusomea udakitari vivyo hivyo ndivyo ilivyo kusomea sheria bila kuwa mwanasheria. Kusomea sheria ni kuhudhuria masomo ya shahada ya sheria. Kuwa mwanasheria ni baada ya kuhitimu, unafanya petition au kupitia shule ya sheria na kupewa kibali kuwa wakili ndipo unakuwa mwanasheria.

Ukiisha hitimu uadakitari lakini hautibu haimaanishi ulifeli, na waliosomea sheria bila kuwa wanasheria haina maana walifeli.

Kama ulivyosema ZEC ikiishatangaza matokeo ya urais hakuna wa kuyapinga. Uko very right lakini

Sheria iko wazi kabisa kuwa uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na ZEC. ZEC ni corporate body yenye composition fulani ili iwe ndio ZEC. Kila kinachofanywa na ZEC kinafanywa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, naomba unijibu maswali haya.

1. Jecha alipofuta matokeo ya Zanzibar aliyafuta kama nani, Mwenyekiti wa ZEC sio ZEC, ZEC ni a composition tena ndani yake mna wajumbe wenu. Jecha alipojigeuza ZEC nlifanya nini?.

2. Uchaguzi unatawaliwa na kanuni na kunapotokea kasoro zipo taratibu za kuripoti kasoro hizo na kuzishughulikia. Jee Kuna kasoro zozote zilizoripotiwa ZEC na kuamuliwa kufuta matokeo?.

3. Kukitokea kasoro zozote, ZEC huchunguza na kufikia maamuzi kwa concensus ikikosekana ndipo kura hupigwa na zikifungamana, then kura ya M/Kiti ndio inakuwa a decisive vote. Jee kunalolote kati ya hayo lilifanyika hadi Jecha kwenda kutangaza uamuzi ule?.

4. Maamuzi yote ya ZEC ni kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, jee tangazo lile la Jecha alitumia kipengele gani cha sheria ipi, kanuni ipi, na taratibu ipi?.

Kwa kukusaidia tuu
1. Jecha ni Mwenyekiti wa ZEC ila yeye sio ZEC hivyo uamuzi wowote atakao utoa yeye Jecha kama Jecha ni auamuzi batili, ila uamuzi haufikiwi na Jecha, unafikiwa na ZEC. Jecha angetangaza uamuzi wa ZEC then uamuzi huo unakuwa ni halali.

2. Jecha alijigeuza ni msimamizi wa uchaguzi, kisha alijigeuza ni mlalamikaji kwa kujaza fomu za malalamiko ya kasoro za uchaguzi, kwa kuzijazia kichwani kwake. Kisha akajigeiza msimamizi mkuu kwa kuyawasilisha hayo malalamiko ya kichwani kwake. Kisha akajigeuza ZEC akayasikilikiza. Akayaundia kamati ya uchunguzi, akajigeuza ndio kamati, akakuta malalamiko hayo ni kweli kuna kasoro, baadae akajigeuza ZEC akaipokea ripoti ya uchaguzi. Akajigeuza Kamati ya ZEC kujadili kasoro hizo, kamati hiyo ikafikia maamuzi ya kufuta matokeo bila kuzingatia sheria yoyote, taratibu yoyote au kanuni yoyote. Baada ya hapo akajigeiza NEC, ikapokea ripoti ya kamati na kuyakubali mapendekezo ya kufuta uchaguzi, ndipo ZEC sasa ikamtuma Mwenyekiti akatangaze kule ZBC hivyo auamuzi ulipaswa kuwa wa ZEC na sio wa Jecha. Jecha alipata wapi mamlaka ya kujigeuza ZEC na kufuta uchaguzi?!.

Au katiba ya Zenj ndivyo ilivyoelekeza kuwa Mwenyekiti wa ZEC anaweza kujigeuza yeye ndio ZEC na akatoa kauli kwa niaba ya ZEC?.

Katiba imesema maamuzi ya ZEC kwenye matokeo ya Urais, hivyo katiba hivyo imesema hata mtu akajigeuza ZEC auamuzi wake ni halali na haupingwi popote?.

Kwa kukusaidia tuu kila alichofanya Jecha ni batili, au haramu, ila batili isipobatilishwa hugeuka haki; na haramu isipobatilishwa hugeuka halali!.

Hata Muislamu safi akinunua ile nyama tamu kuliko nyama zote, kutoka bucha iliyoandikwa "halal" akipika na watu wakajiramba, walaji hawana kosa lolote kula haramu, kwa kwa sababu hawakujua!. Hivyo haramu isipobatilishwa hugeuka halal!. Vivyo hivyo kwa batil isipobatilishwa hugeuka ni haki.

Kila alichofanya Jecha ni ubaliti mtupu na haramu, lakini hakuna yoyote aliyejitokeza kuibatilisha batil ile wala kuibatilisha haramu ile, hivyo Shein ni rais halali aliyetokana na haramu isiyoharimishwa na batil isiyo batilishwa!.

Hata mwanaharamu ni mwanaharamu tuu kama hadi anazaliwa kwenye haramu.

Ikitokea umembaka mwanasheria na kumpa ujauzito katika uzinifu wa ubakaji huo, mtoto atakayezaliwa atakuwa ni mwanaharamu, ila baada ya taarifa ya ujauzito ukaamua kumuoa huyo binti kwa ndoa halali, mtoto atakayezaliwa ndani ya ndoa ni mwana halali na sii mwanaharamu! .

Uchaguzi wa marudio Zanzibar, ulijengwa katika misingi haramu, lakini matokeo ni matokeo halali.

Paskali.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Haya ni maoni yangu katika kutekeleza uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yangu, na justification why me au mtu asiye Mzanzibari kuzungumzia issue za Zanzibar, hii ni kufutia mimi Paskali ambaye ni raia wa Tanzania, yuko huru kutoa maoni yake yoyote kuhusu jambo lolote la nchi yetu ikiwemo Zanzibar ambayo ni sehemu ya JMT, na pesa ya jasho langu kupitia kodi yangu, ndiyo inayotumika sio tuu kugharimia kuiendesha SMZ, bali hadi kuvigharimia nyama ikiwemo CCM na CUF ambayo vinatafuna tuu pesa yetu.

Hivyo nina haki na mamlaka yote kuhoji au kuzungumzia lolote kuhusu matumizi ya kodi yangu, na tayari nimeishamshauri Rais Magufuli, akiona vipi, afutilie mbali ruzuku kwa vyama vya siasa, ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote.

Sasa tuje kwa Zanzibar, tulipoungana tulikubaliana kuchangia gharama za kuendesha muungano, lakini zigo lote la muungano amebebeshwa mtu mmoja tuu, huku mwingine akibweteka kazi yake ni kubebwa tuu!, haiwezikani kuendelea kuishi kwa kujidai tuko sawa na tuna haki sawa ndani ya muubgani, huku mmoja akimenyeka na kutoka jasho, huku mwingine akiishi kama kupe!.R
uzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli Aifutilie Mbali?.

Habari Kuwa Zanzibar Kuna Mgogoro wa Kisiasa, Sasa ni Kelele!.
Kadri siku zinavyokwenda, bado kunajitokeza watu wanaendelea kuaminishwa kuwa Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa, na kuwa, kuna kitu kitafanyika ili kuutanzua mgogoro huo very soon!. Hao watu wanaoaminishwa, wanamini kuwa ni kweli Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa kwa sababu wanaowaambia hivyo ni viongozi wao wanaowaamini, habari hizi za Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa, zinaposemwa sana na kurudiwa rudiwa kusemwa tena na tena kuwa Zanzibar kuna mgogoro wa kisiasa na kuna kitu kitafanyika kuutanzua, ila hali halisi ya kiukweli halisi kuhusu Zanzibar, ni hakuna mgogoro wowote wa kisiasa na hakuna kitu chochote kinachofanyika sasa au kitakachofanyika baadae kabla ya 2020, ni kelele tuu za mfa Maji za kuwapa watu matumaini hewa au matatajio hewa matokeo yake 2020 itafika bila lolote bila chochote, sijui wataziweka wapi sura zao?! .

Ukweli Mchungu. Zanzibar Hakuna Mgogoro Wowote wa Kisiasa.
Huu ndio ukweli mchungu kuwa Zanzibar, hakuna mgogoro wowote wa kisiasa, mgogoro ukikuwepo mwanzo uchaguzi ulipofutwa lakini baada ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, japo ulisababishwa na sababu haramu, lakini uchaguzi huo ulikuwa ni uchaguzi halali kisheria, na umeendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi huru na wa haki, hivyo matokeo yake ni halali, na mshindi halali ni Dr. Ali Mohamed Shein, hivyo anakuwa ni Rais halali wa Zanzibar, hakuna jambo jingine lolote linaloweza kufanyika chini ya jua, kubadili chochote, Uchaguzi mwingine ni mpaka 2020!.

Huu ndio ukweli mchungu kuhusu Zanzibar, the sooner you accept, the plain truth, the better!, msiendelee kudanganywa na viongozi wenu kuwa kuna kitu chochote kitafanyika, hakuna kitu kingine chochote cha kufanyika zaidi ya uchaguzi wa 2020, kinyume cha hapo ni kuendelea kuishi kwenye matumaini au matarajio hewa, yaani kuishi in a living lie, ambayo ni sawa na kuukimbiza upepo.Uchaguzi umepita, umekwisha, sasa ni muda wa kufanya kazi tuu, na ndio maana halisi ya sasa kazi, na hapa kazi tuu.

Kufuatia Watanzania kuwa ni wavivu wa kusoma makala ndefu, naomba kuikatia hapa lakini kwa wanaopenda kuzama zaidi ndani, zameni na mimi.

Jee Ni Kweli Kuna Mgogoro wa Kisiasa Zanzibar?.
Mgogoro ulikuwepo pale mwanzo kulipofutwa matokeo, na kipindi chote cha mpito, kabla ya uchaguzi wa marudio, lakini baada ya uchaguzi wa marudio na matokeo kutangazwa, hakuna tena mgogoro wowote wa kisiasa Zanzibar, hii ni kufuatia haramu hiyo ya kubatilishwa kwa matokeo halali, kutoharimishwa rasmi, na badala yake,ukatangazwa uchaguzi wa marudio uliotokana na haramu isiyoharimishwa, hivyo kuwa ni uchaguzi halali.

Kwa vile uchaguzi huo wa marudio ulifuata misingi yote ya uchaguzi huru na wa haki, then matokeo ya uchaguzi huo ni matokeo halali, then hakuna mgogoro wowote wa kisiasa Zanzibar, na Dr. Shein ni Kiongozi halali wa Zanzibar, aliyechaguliwa kwenye uchaguzi huru na wa haki, uchaguzi umekwisha, sasa ni wakati wa kuchapa kazi tuu, uchaguzi mwingine ni mpaka 2020!.

NB. Kususia kushiriki uchaguzi huru na wa haki, hakubatilishi matokeo ya uchaguzi huru na wa haki.

Paskali

Hapa umejishusha kweli Paskali. Ni kweli Shein ndio anatawala ZNZ (sio kuongoza) yeye na chama chake, na ni kweli huenda hali ikawa hivyo mpaka 2020. Lakini, hii yote haifuti ukweli kwamba CCM na Shein wao wamekaa pale kibabe na kwa dhulma. Na pia haifuti ukweli kwamba hatua waliyochukua CUF ya kususia uchaguzi wa March, 2016 ulikuwa ni wa kijasiri na kizalendo kwa wale wanaoelewa na kuona mbali. Kwa kususia uchaguzi ule, CUF wamechagua kuwa upande wa wananchi, ambao waliwakataa CCM na kuwachagua wao. CUF wangeshiriki uchaguzi ule kharam basi wangekuwa wasaliti wa nchi yao na kwa wananchi wao. Zaidi ya hapo, kama walivyosema wachangiaji wengine, ni blah blah tu za kutaka kuhalalisha uongo uwe ukweli kwa kusema kwamba uchaguzi wa March, 2016 kule ZNZ ulikuwa halali. Uchaguzi ule ungekuwa halali vipi wakati ulikuwa ni zao la kufutwa uchaguzi na matokeo halali ya October, 2015? Kwa mantiki ya kawaida tu huwezi kuzungumzia uchaguzi wa March, 2016 bila kwanza kutoa majibu ya kuridhisha kuhusu kufutwa kwa ule wa October, 2015. Mpaka leo CCM na tume yake ya Jecha haijatoa maelezo ya kuridhisha kuhusu kufutwa ule uchaguzi wa October, 2015 achilia mbali kwamba Jecha hakuwa na mamlaka ya kuufuta kihuni vile.
 
Mkuu Wateule, kwanza nakubaliana na wewe kwa mengi japo sii yote. La kwanza ni uchaguzi wa October 25 uliofutwa ni kweli CUF ilishinda na hili nimelisema hapa

Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Swali linakuja jee CUF ilishindaje uchaguzi wa October 2015?. Jee ilishinda kihalali au baada ya kugundua kuwa kila siku CCM huwa inashinda kwa kutumia mbinu, hivyo this time around, CUF now wakaamua kutumia mbinu?!.

Kama CUF imeshinda kihalali, then nikauliza kuna haja gani kuogopa kushiriki uchaguzi wa marudio?.

Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?

Kitendo cha CUF kususia uchaguzi wa marejeo ambacho wewe umekiita ni cha kishujaa, mimi nakiita ni suicidal mission, kwa sababu CUF lost Pemba for good!. It will never be the same again!. Hili nimelizungumza hapa
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Kuna wengi wanajifariji kuwa kwa vile Pemba ni ngome ya CUF, then hata CUF wafanye madudu gani, Pemba will always remain loyal!. No way!. Kuna watu wengi Pemba ambao hawana time na politics, hivyo wamekuwa wakiichagua CUF kwa mkumbo tuu, maadam sasa Pemba iko chini ya CCM upande wa wajumbe wa BLW, japo wabunge wa Bunge la JMT wote ni CUF, wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT ni kama maboya tuu!. Hawawezi kupeleka maendeleo yoyote majimboni mwao, watakaoleta maendeleo Pemba ni Wajumbe wa BLW na sio Wabunge wa CUF!. Hoja za maendeleo ndio sababu pekee kwa nini CUF will never be the again in Pemba.

Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!

Pamoja na tofauti zetu, ila kuna jambo moja kubwa tunalokubaliana ni huu ukweli mchungu wa bandiko hili, kuwa there is nothing that will be done by any human being that will change the situation in Zanzibar shot of 2020!.

The only one who can change is "The One and Only!", na kwa vile tuliwahi kuelezwa kama kweli ni dhulma, na Zanzibar ni watu wa swala 5, swalini basi Itqwaf na kufanya Albadir ili mwenye uwezo afanye mambo kabla ya 2020!, vinginevyo ni kusubiria tuu hadi 2020, and I'm afraid 2020 to some might be too little too late!.

Paskali
 
Paskali nambie ukweli nitakufichia siri yako .Hivi wewe ni Bashite wa Sheria au unajipendekeza kwa Msukuma mwenzako huenda ukaukwea? Kama wewe ni mwanasheria wa kufuzu darasani na kuielewa Katiba ya Zanzibar na sheria za Tume ya uchaguzi ya Zanzibar usingelithubutu kuandika upuuzi na utumbo huo wa Kuchanganya Mgogoro wa Uchaguzi Zanzibar na Mgogoro wa CUF na kibaraka Lipumba kwa bara.
Pale Bashite anapomwita mtu mwenye uwezo Bashite. Ulichoandika Mayala kinaeleweka. Tatizo watu hawataki kuelewa ni ushabiki tu. Tizama hata watunga sheria wetu.
 
Some birds were not meant to be caged, that's all. Their feathers are too bright, their songs too sweet and wild. So you let them go, or when you open the cage to feed them they somehow fly out past you. And the part of you that knows it was wrong to imprison them in the first place rejoices, but still, the place where you live is that much more drab and empty for their departure. Qoute Stephen King.
Zanzibar shall be free.
 
Mkuu Wateule, kwanza nakubaliana na wewe kwa mengi japo sii yote. La kwanza ni uchaguzi wa October 25 uliofutwa ni kweli CUF ilishinda na hili nimelisema hapa

Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Swali linakuja jee CUF ilishindaje uchaguzi wa October 2015?. Jee ilishinda kihalali au baada ya kugundua kuwa kila siku CCM huwa inashinda kwa kutumia mbinu, hivyo this time around, CUF now wakaamua kutumia mbinu?!.

Kama CUF imeshinda kihalali, then nikauliza kuna haja gani kuogopa kushiriki uchaguzi wa marudio?.

Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar?

Kitendo cha CUF kususia uchaguzi wa marejeo ambacho wewe umekiita ni cha kishujaa, mimi nakiita ni suicidal mission, kwa sababu CUF lost Pemba for good!. It will never be the same again!. Hili nimelizungumza hapa
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Kuna wengi wanajifariji kuwa kwa vile Pemba ni ngome ya CUF, then hata CUF wafanye madudu gani, Pemba will always remain loyal!. No way!. Kuna watu wengi Pemba ambao hawana time na politics, hivyo wamekuwa wakiichagua CUF kwa mkumbo tuu, maadam sasa Pemba iko chini ya CCM upande wa wajumbe wa BLW, japo wabunge wa Bunge la JMT wote ni CUF, wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT ni kama maboya tuu!. Hawawezi kupeleka maendeleo yoyote majimboni mwao, watakaoleta maendeleo Pemba ni Wajumbe wa BLW na sio Wabunge wa CUF!. Hoja za maendeleo ndio sababu pekee kwa nini CUF will never be the again in Pemba.

Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!

Pamoja na tofauti zetu, ila kuna jambo moja kubwa tunalokubaliana ni huu ukweli mchungu wa bandiko hili, kuwa there is nothing that will be done by any human being that will change the situation in Zanzibar shot of 2020!.

The only one who can change is "The One and Only!", na kwa vile tuliwahi kuelezwa kama kweli ni dhulma, na Zanzibar ni watu wa swala 5, swalini basi Itqwaf na kufanya Albadir ili mwenye uwezo afanye mambo kabla ya 2020!, vinginevyo ni kusubiria tuu hadi 2020, and I'm afraid 2020 to some might be too little too late!.

Paskali

Paskali, nami nakubaliana na wewe hapo kwenye maombi yaendelee kufanyika na wa ZNZ (sio wapemba peke yao, kwani Wazanzibari wengi wakekerwa na dhulma ya October, 2015) ili mtoa haki wa kweli (MUNGU) afanye yake kabla ya 2020. Lakini, sikubaliana na wewe kwamba CUF walishinda kwa "mbinu" na hivyo walikuwa hawana sababu ya kuogopa kushiriki ule uchaguzi wa March, 2016. Katika hii hoja, nitarejea kwenye swali la msingi ambalo hata Maalim Seif mwenye amekuwa analiuliza mara kwa mara na mara zote sioni wala sisikii akipewa jibu la maana....hivi unafikiri na kuamini kwamba CCM walifuta uchaguzi wa October 25, 2015, ili wafanye mpya na kushindwa tena???

Wote tunajua kwamba majeshi, mabomu, vifaru, na mizinga vilikuwa vinatiririka ZNZ kuelekea huo unaoitwa "uchaguzi wa marudio" wa March, 2016 ili kuhakikisha ZNZ inabaki kuwa mali ya CCM na vibaraka wake kule ZNZ. Katika mazingira kama yake, ingekuwa ni ujinga na usaliti kwa Maalim Seif kama anavyopenda kusema "kuweka kichwa na kuchinjwa" wakati anajua atachinjwa tu. Katika uchaguzi ule wa zao la dhulma, CCM walishajiandaa "kushinda" kwa gharama yeyote, na pia walikuwa tayari kumpa Seif nafasi wanayotaka na kumchagulia wao, ambayo ni umakamu wa kwanza wa rais. Narudia tena, kitendo cha CUF kususia uchaguzi ule wa March, 2016 ni cha kijasiri na kizalendo kwani kwa kufanya hivyo wameonyesha kwamba hawakutaka kuweka maslahi ya vyeo vya kisiasa mbele na badala yake wamezingatia principle (ya kutohalalisha dhulma) na maslahi mapana ya ZNZ.

Wewe na wengine mnaona CUF wamekosea kwasababu mnaangalia kinachoendelea sasa kule ZNZ kwa CCM kufanikiwa kulazimisha Shein kuwa madarakani. Lakini, kwasisi tunaoona mbali CUF imeimarika zaidi ZNZ kwa uwamuzi ule. Na kama Mungu hajafanya yake kabla ya 2020, basi CCM watakuja kushangaa nguvu waliyoiongezea CUF kwa kitendo chao cha kuidhulumu ushindi wake halali. Waliodhulumiwa ambao kimsingi ni wananchi wa ZNZ wapo, na wao sio wajinga wa kutokuelewa maamuzi ya CUF. Kunapo uhai, tukutane tena hapa 2020 ili kujadili tena uhai na nguvu ya CUF kule ZNZ ambayo itakuja kuwashangaza wengi mnaoona na kufikiri masafa mafupi (short sighted thinking). Ukweli na haki siku zote hushinda hata kama ushindi huo utaonekana umechelewa.
 
Paskali, nami nakubaliana na wewe . Kunapo uhai, tukutane tena hapa 2020 ili kujadili tena uhai na nguvu ya CUF kule ZNZ.
Mkuu Wateule maadam hoja kuu ya msingi ya bandiko hili hakuna lolote Zanzibar hadi 2020, then Insh Allah, tukutane hiyo 2020 tukumbushane! .

P.
 
Back
Top Bottom