Ukweli mchungu!! Usalama wa Taifa wanaamini Rais huchaguliwa na kamati ya CCM na si wananchi

Uporaji wa madaraka hutokea pale ambapo wanaohusika na hayo madaraka wanaamua kukwepa wajibu wao wa kuyalinda kwa jasho na damu inapobidi. Tunapoona nchi yenye kuheshimu raia, inaonyesha ujasiri wa hao raia na wala siyo fadhila za viongozi. Trump kila siku analalamika jinsi katiba na mifumo ya nchi yake inavyomsumbua kutekeleza yale anayoyawaza na aliyowaahidi wafuasi wake.

Wananchi legelege huzaa viongozi madikteta.
 
Moja ya "legacy" mbaya sana ya Mwl Nyerere ni kuudanganya ulimwengu kuwa Tanzania imekubali demokrasia ya vyama vingi. Nyakati kama hizi ndio zinazotufanya tuamini kuwa ni bora angesimamia kile alichokiamini mpaka mwisho wake. Mambo ya demokrasia angetuachia mpaka tutakapoona wakati wake umefika ndipo tuyaanzishe kwa misingi mizuri.

Misingi ya demokrasia imeshavunjwavunjwa kabisa, na itachukua miaka mingine zaidi ya kumi kuisimika demokrasia ya kweli ndani ya nchi hii. Na endapo jiwe lina nia ya kuitawala nchi hii kifalme basi tuhesabu miaka 50 au zaidi mbele.
 
Nadhani tuwe fair. Yoyote anayeteuliwa kugombeanafasi ya Urais na chama chake hupewa ulinzi na serikalipia chama chake.Mbona hatuongelei wagombeawengine walilindwa na nani? Binafsi sijwahi kusikia malalamiko yamgombea yoyote kunyimwa ulinzi.
wapinzani huwa wanaogopa walinzi kutoka serikalini.tiss ni serikali,watu wa serikali hutoa siri za wagombea wengine kwa ccm.
 
Mtu mmoja ninayemfahamu sana na anayesemekana kuwa mtu wa TISS. Aliniambia Siku moja kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 kuwa: "kazi ya wananchi kesho no kazi ya kupiga kura tu ..... Kazi ya kuchagua raisi si kazi ya wapiga kura"!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitu ambacho nina uhakika nacho ni kwamba kia mtu atakuifa hata hao tiss watakufa tu,ila dhambi ya dhuruma haita waacha salama,kubadilisha matokeo au maamuzi ya watu ni dhambi mbaya sana.ni zaidi ya ujambazi.
 
Tanzania hatuhitaji demokrasia,wasio na elimu ya kutosha kuchagua Raisi sahihi ni asilimia zaidi ya 85, huwezi ruhusu nchi iangukue mikononi mwa Raisi aliye chaguliwa na wajinga wa taasisi ya uraisi kisa walichagua propaganda zilizowatosha na kuwaridhisha kwa ujinga wao, hivyo basi nionavyo Mimi ni sahihi watu wenye uelewa na taasisi ya uraisi wachague Raisi kwa maslahi mapana ya wengi wasio na uelewa huo. Kwa Sasa Bado mfumo wa ccm uko imara Sana namfumo ukiwa imara basi uwezekano wa kutoa Raisi bora ni mkubwa. Hivo jiongeze!!
Nb: miaka ya 23 (bc) kabla ya kristo mwana farisafa socret alihukumiwa kifo na kupewa sumu ya mmea Aina ya hemlock baada tu yakuweka wazi Kua kura ya mjinga na mwelevu wa taasisi ya uongozi haziwezi Kua na uzito sawa

Mwisho nisemetu Kua demokrasia ni nadharia tuu popote duniani.
kama mfumo wa ccm bado ni imara unawezaje kutuletea marais wa ajabu namna hii,au mfumo umeingiliwa na kirusi kutoka nchi jirani?,nyerer akiwa hai aliwezaje kuwalalamikia maraisi waliokuja baada yake kwa kumsaliti hasa kwenye sera za soko huria na baadae ubinafsishaji?,mfumo ulikua umelala wakati wa kuwapata maraisi waliomfuata?
 
Na ikumbukwe kwamba kama ni weli TISS ndio waliotuchagulia Magufuli awe Rais wa awamu ya tano wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania basi wako makini kuliko maelezo, si unaona jembe hilo linavyopiga kazi? si unaona asivyoteteleka, labda niwakumbushe tu kwamba huyu ni rais imara kuwahi kutoka katika Tanzania hii kwa miaka ya hivi karibuni. Nchi za waafrica wenzetu kama Zambia, Malawi Namibia na Botswana wanatamani wangepata Rais kama huyu labda wangepiga hatua kubwa kuliko pale walipo., Watswana wanamlinganisha Magufuli na Lan Kama ambaye alileta mageuzi makubwa na kuibadilisha nchi yao kwa mda mfupi sana, miongoni mwa mambo aliyoyafanya mi pamoja na kufanya mabadiliko ya sheria katika sector ya madini, kupambana na rushwa, kuzuia safari za nje ya nchi zisizo za lazima kwa viongozi, pamoja na kujenga miundo mbinu imara ndani ya nchi.KLKwahiyo tuache siasa nyepesi za kupotoshana.
pole sana
 
Usalama wa Taifa umekuwa ni tatizo katika hii nchi.
wamekua wakituingiza chaka kila baada ya miaka mitano,watanzania hawana furaha kabisa ,hofu na mashaka vimetamalaki,usalama wanakula chokcolate tu,huku ndugu zao (wafanyakazi)hawajapata ongezeka la mishahara mwaka wa nne sasa,kule jamaa zo (wakulima) wajalipwa madeni ya,na hata rafiki zao (wafanyabiashara) wanafunga biashara zao kwa sababu ya mazingira ya biashara zao yamekua magumu.
Mungu aingilie kati,hawa ndugu zetu( usalama) wameungana na watesi wetu.(ccm).
 
mkuu haya mambo yapo hata marekani, wazee wa kazi wakishaamua yupi ndiyo anafaa, hakuna namna, democracy is an imagination of beholders,

Huwezi kuachia nchi itawaliwe na yeyote anayejisikia, lazima achujwe na athibitishwe hasa kulingana na mwelekeo wa chama kwa uzito wake na ushawishi.

Unaposikia fulani kakatwa ndiyo mipango yenyewe, raia wengi hughubikwa na ushabiki kiasi kwamba wakiachwa waamue peke yao, athari nyingi zitatokea, Usalama wanawajua wagombea vizuri kuliko tunavyowajua sisi raia watiifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nakuomba ufute huu ufananisho wako wa uongo.
Marekani usalama wao wa taifa huwa hawafanyi hivyo unavyosema au unavyotaka wewe watu waamini,
Marekani na nchi zote zenye demokrasia ya vyama vingi wanausalama wao hutoa ushauri kwa vyama vyote vyenye nia ya kuweka wagombea kabla ya uchaguzi,ili siku watu wakichagua angalau wachague mgombea aliyechujwa na wanausalama,wanausalama wa marekani hutoa haki sawa kwa wagombea wote,na baadae huhesshimu maamuzi ya wananchi.
wao usalama kazi yao ni kuwasaidia vyama kumpata mgombea asie kinyume na usalama wa Marekani, lakini kazi ya kuchagua huachiwa wananchi,na huiheshimu.
ndio maana trump ni raisi ingawa haelewani na wanausalama.
 
mkuu haya mambo ni mipango iliyo kwenye siri kubwa sana, mtu hashindi kwa bahati mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
hakuna mipango yeyote ya siri ndugu,ni dhuluma tu,iweje nchi ipoteze rasilimali na mamilioni ya pesa kupitisha chaguzi ambazo zinafahamika matokeao yake?
uchaguzi mkuu tabia za usalama ni zilezile,chaguzi za marudio usalam tabia ni zilzile,chaguzi za serikali za mitaa usalama tabia nizilezile,usalama wetu tabia zao yaani kazi zao ni kulinda chama kilicho madarakani.
umedanganya broo.
 
Uzi wako huo unaousema nimeusoma hauna cha maana ,wewe ulileta huo uzi ili kuhalalisha dhulima fulani amabyo wewe unaijua ,siwezi kuwalaumu usalam wetu kwa hili,usalama wa kweli hawawezi kuwa na mipango ya kijinga namna hiyo ,maana ktk chaguzi za tz kuna watu hupoteza maisha,viungo na mali zao sasa ni kwa nini kuwe na mipango ya usalama yenye kuishia kuumiza watu>
nijuavyo mimi popote dunianusalama,jeshi,polisi and like huwa hawana vyama ama ushabuki wa vyama,lakini wewe ni wazi kabisa ni shabiki wa ccm .
 
Wewe vipi bwana!!! Hii ndo jambo ambalo nalichukia kuliona kuliko yote. Eti wazungu waje, why do we have this inferiority complex against white people?? Why??
They are nothing to us, they destroyed our civilization, changed our course of history, undermined us and they are still undermining us. Why do you even bring they there!!
Eti waje kutusaidia, kwani sisi hatuwezi tatua matatizo yetu wenyewe??
You hate your leader so much ati unataka wazungu wamtoe off people!!!
Mimi mwenyewe kuna mambo kibao sikubaliani nae. Ila sina chuki ya namna hii.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila wapenda weusi wanaofanya ujinga uleule?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wapinzani huwa wanaogopa walinzi kutoka serikalini.tiss ni serikali,watu wa serikali hutoa siri za wagombea wengine kwa ccm.

Wanaweza kuwa right lakini katika mazingira hayo then tatizoliko sehemu nyingine hivyo tuka deal tatizo liliko. Huyu baba wa watu aachwe afanye kazi yake.
 
Upinzani Tanzania - labda Mkwawa wengine ni kama makasuku tu - mchana wako CDM usiku CCM
 
mkuu haya mambo yapo hata marekani, wazee wa kazi wakishaamua yupi ndiyo anafaa, hakuna namna, democracy is an imagination of beholders,

Huwezi kuachia nchi itawaliwe na yeyote anayejisikia, lazima achujwe na athibitishwe hasa kulingana na mwelekeo wa chama kwa uzito wake na ushawishi.

Unaposikia fulani kakatwa ndiyo mipango yenyewe, raia wengi hughubikwa na ushabiki kiasi kwamba wakiachwa waamue peke yao, athari nyingi zitatokea, Usalama wanawajua wagombea vizuri kuliko tunavyowajua sisi raia watiifu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tafauti kubwa ya Tanzania na Marekani ni hii

Ndani ya U.S, CIA ndio wanayoiongoza nchi, Tanzania CCM ndio wanayoiongoza nchi. TISS wanawatumikia CCM wakati Vyama vyote US vipo chini ya CIA. Kwaiyo acha kulinganisha.
 
Wale wapenda mabadiliko ya kweli tunapaswa kubadili mbinu za kupata yale mabadiliko tunayoyataka.

Tukiongelea uchaguzi wa kila baada ya miaka mitano kama ni ucahguzi wa wananchi tunajidanganya na tunawadanya wananchi ambao hawana uelewa mpana wa maswala ya nchi yetu.

Taasisi nyeti ya usalama wa taifa haimini katika mfumo wa vyama vingi wala katika mfumo wa kuchaguana katika sanduku la kura. Hivyo basi huu utaratibu wa kupiga kura ni kuhalalisha tuu kile walichokiamua wao huko vyumbani.

Nitatolea mfano kwa uchaguzi uliopita uliomuweka madarakani mheshimiwa magufuli. Taasisi nyeti ya usalama wa taifa ilianza kumlinda tangu pale alipochaguliwa na kikao cha ccm pale dodoma. Na bila aibu wala wasi wasi mlinzi wake waliomuweka tangu anachaguliwa magufuli dodoma ndio mlinzi wake mpaka leo hii. Wewe unaona mimi naona na wao wanaona na hakuna cha kuwafanya.

Kama wao wanaopaswa kusimamia haki wanamtambua mtu kuwa rais pale tuu anapochaguliwa na kamati za ccm wewe ni nani hata uje upindue maamuzi yao katika sanduku la kura??

Nasema hivi huku kufanya uchaguzi ni kupoteza muda na mali za nchi kwa mfumo tulionao.

Tupiganie kubadili mfumo wetu ndipo tuingie kwenye kushindana. Huwezi kushindana na watu unaotegemea wasimamie ushindani.

Huyu hapa chini mlinzi wa rais toka kwenye kampeni na kwa wakati ule alijifanya greengurd toka ccm na sasa ni mlinzi wa rais toka usalama wa nchi .

Tutafika tuu hata kama kwa shida ila tubadili mbinu za kushindana na hawa watu
Braza weka kumbukumbu sahihi, unadhani wale waliokuwa wanamlinda lowasa wakati wa kampeni wanatoka chadema? Kama huna uelewa ni bora ukae kimya, kamuilize lowasa kuwa amebadirishiwa waliokuwa wanamlinda? Nadhan waliangalia ulazima wa wagombea wale kulindwa kulingana na ushawishi wao na uwezekano wa kufanyiwa hujuma. Maana tayar waliingia kwenye kundi la watu mashuhuri (VIP) ambao vyombo vya ulinzi vilipaswa viwalinde kwa nguvu zote. Sometimes nafikiri tusiwe mashabiki tuulozane wenyeewe kwanza maana hata ukisoma kwenye vitabu vya kiusalama hata mitandaoni vitakuonyesha ni watu wa aina gani wanastahili kulindwa. Hata MO na Bakhresa wakikubali kulindwa watalindwa kwa nafasi zao katika jamii na uchumi wa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom