Ukweli mchungu!! Usalama wa Taifa wanaamini Rais huchaguliwa na kamati ya CCM na si wananchi

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,114
Wale wapenda mabadiliko ya kweli tunapaswa kubadili mbinu za kupata yale mabadiliko tunayoyataka.

Tukiongelea uchaguzi wa kila baada ya miaka mitano kama ni ucahguzi wa wananchi tunajidanganya na tunawadanya wananchi ambao hawana uelewa mpana wa maswala ya nchi yetu.

Taasisi nyeti ya usalama wa taifa haimini katika mfumo wa vyama vingi wala katika mfumo wa kuchaguana katika sanduku la kura. Hivyo basi huu utaratibu wa kupiga kura ni kuhalalisha tuu kile walichokiamua wao huko vyumbani.

Nitatolea mfano kwa uchaguzi uliopita uliomuweka madarakani mheshimiwa magufuli. Taasisi nyeti ya usalama wa taifa ilianza kumlinda tangu pale alipochaguliwa na kikao cha ccm pale dodoma. Na bila aibu wala wasi wasi mlinzi wake waliomuweka tangu anachaguliwa magufuli dodoma ndio mlinzi wake mpaka leo hii. Wewe unaona mimi naona na wao wanaona na hakuna cha kuwafanya.

Kama wao wanaopaswa kusimamia haki wanamtambua mtu kuwa rais pale tuu anapochaguliwa na kamati za ccm wewe ni nani hata uje upindue maamuzi yao katika sanduku la kura??

Nasema hivi huku kufanya uchaguzi ni kupoteza muda na mali za nchi kwa mfumo tulionao.

Tupiganie kubadili mfumo wetu ndipo tuingie kwenye kushindana. Huwezi kushindana na watu unaotegemea wasimamie ushindani.

Huyu hapa chini mlinzi wa rais toka kwenye kampeni na kwa wakati ule alijifanya greengurd toka ccm na sasa ni mlinzi wa rais toka usalama wa nchi .

Tutafika tuu hata kama kwa shida ila tubadili mbinu za kushindana na hawa watu
 

Attachments

  • C8F977D7-251F-47BE-8D69-894381CA8BFE.png
    C8F977D7-251F-47BE-8D69-894381CA8BFE.png
    175.7 KB · Views: 140
  • 078B8216-946E-414A-A612-B6C43F889D32.png
    078B8216-946E-414A-A612-B6C43F889D32.png
    462.9 KB · Views: 101
Usalama wa Taifa ndiyo wadhibiti wa siasa na uchumi wa taifa letu, wanaona mbali kuliko ushabiki wetu wa kisiasa, walifanya kazi yao kikamilifu!



Sent using Jamii Forums mobile app
kwa hiyo wanaona mbele kabla ya kupiga kula kwamba wananchi watamchagua wa ccm tuu na si toka chama kingine???

hii ni nchi yetu sote ikiharibika tunaathilika sote tuijenge ijiendeshe na si kuendeshwa na kikundi cha watu wachache
 
kwa hiyo wanaona mbele kabla ya kupiga kula kwamba wananchi watamchagua wa ccm tuu na si toka chama kingine???

hii ni nchi yetu sote ikiharibika tunaathilika sote tuijenge ijiendeshe na si kuendeshwa na kikundi cha watu wachache
mkuu haya mambo yapo hata marekani, wazee wa kazi wakishaamua yupi ndiyo anafaa, hakuna namna, democracy is an imagination of beholders,

Huwezi kuachia nchi itawaliwe na yeyote anayejisikia, lazima achujwe na athibitishwe hasa kulingana na mwelekeo wa chama kwa uzito wake na ushawishi.

Unaposikia fulani kakatwa ndiyo mipango yenyewe, raia wengi hughubikwa na ushabiki kiasi kwamba wakiachwa waamue peke yao, athari nyingi zitatokea, Usalama wanawajua wagombea vizuri kuliko tunavyowajua sisi raia watiifu.
 
M nafikiri wapinzani wangekomaa na katiba,tume huru,alafu waweke nguvu kubwa kwenye ubunge na kutengeneza wanachama vyuoni na vijijini wakikomaa huko kukawa fresh ndo waje kuwekeza kwenye urais ila kwa sanduku la kura haitotkea
 
Kama ni hivyo uchaguzi ni wa nini? Lissu ongea na wazungu waje watoe msaada kama waliowapa watu wa Libya kumn'ngoa Gaddafi. Haiwezekani watu tupange mistari mirefu kupoteza muda huku watu wanapitisha watu wao.
Braza! democracy haijawahi kuwepo duniani, hata Marekani mambo ni yale yale!
 
Wewe uliopost hii utango'oka shauri yako. Usalama hawachezewi kabisa. Utawaachia majonzi familia yako bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwani hii ni siri?? au nimewatukana?? au huyu mlinzi nimemsingizia?? usalama hawako hivyo mnavyotaka tuamin wao ni makatili. yaan et ukiwazungumzia tuu wewe kwisha habari yako no. mm nitasema pale naona inafaa kusema kwa lugha sahihi isio na matusi. sasa kama wao ukweli ni maudhi kwao hadi kuua mtu hakuna shida waje tuu kufa ni kwa kila mtu
 
"Wewe unaona mimi naona na wao wanaona na hakuna cha kuwafanya".

hayo maneno hapo juu ni mazito sana mkuu. ninachoombea ni kutokuibuka kwa wale ambao hawana cha kupoteza hata wakijitoa mhanga kufa. wakitokea hao hakuna cha CCM wala TISS wala nani.... wote tutaishi kama digidigi!
umenielewa nadhani.
 
Back
Top Bottom