Ukweli mchungu: Lowassa ameshatoswa na CCM

Ukweli mchungu: Lowassa ameshatoswa na CCM

Jana nilimsikia Katibu mkuu wa Ccm redio Clouds, nadhani alikuwa Tanga akisema kigezo cha kwanza kwa mgombea atakayeteuliwa na Ccm itakuwa ni uadilifu. Alisema pia wagombea wa Ccm wanaoutaka urais itabidi wajipime kwa kigezo hicho namba moja. Ni juzi tu Mzee Msuya alisema Lowassa kama anaenda upinzani aende lakini chama hakiwezi kumpitisha fisadi kugombea urais.

Kama ni mfuatiliaji wa mambo ya iasa za nchi hii utajua kwamba Lowassa alikuwa karibu sana na viongozi wa dini, lakini juzi tu walitoka hadharani na kumnanga kama 'fisadi msaka Ikulu'. Hawa ni watu wanaheshimika sana na mara nyingi wanakuwa taarifa nyeti toka hata Ikulu. Mtu kama Pengo ni figure kubwa nchi hii, anajua yaliyo uvunguni Ikulu.Kama angekuwa amedokezwa kwamba ndiye mgombea wa Ccm ajaye asingethubutu kumchana hadharani au maaskofu wenzake kumnanga!

Wale 'Team Lowassa' mjiandae kisaikolojia kutupwa kwa mgombea wenu maana tangu imeanza 2015, hali inazidi kuwa mbaya. Mashambulizi yanatoka kila pembe tena kwa watu wanaoheshimika. Baba Askofu Mokiwa, Baba Askofu Pengo, Nzigirwa, Mzee Msuya! Mlishajiuliza hivi karibuni Pengo alienda kufanya nini Ikulu?

Tafakari!

My friend; tafadhali sana tofautisha "The real from the Ideal!!"; if wishes were horses; each and everyone of us would ride ONE!!
Wataongea mpaka mpaka mapovu yawatoke; watajipandisha mori na kujitia ukakasi; lakini katika uteuzi wa mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Majambazi (CCM); read my lips; Edward Ngoyai Lowasa is the man to beat !!!

Vinginevyo; tuanze sasa kuandika "Tanzia" ya CCM; na maandalizi ya kuikaribisha jamhuri ya pili ya Tanzania

Freedom is comming tommorow; Let freedom reign; Aluta continua.
 
Lowasa hawezi kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM labda huko UKAWA anakopanga kwenda

Ukiendelea Na Hizi Siasa Zako Za Maji Taka. Ntakuweka Hadharani. Jina Lako,Namba Zako Za Simu,Mtaa Unaoishi, Pamoja Na Namba Ya Nyumba Unayokaa. Umekuwa Ni Mchochezi,Mnafiki,Na Mtu Hatari Sana Kwa Amani Ya Nchi Hii. Jaribu Kujirekebisha Mara Moja,La Sivyo Ntakuumbua Humu Jf
 
Yan Lowassa amewafanya watu wengi waugue magonjwa ya akili;hofu na kiwewe kimewajaa...he's a hard nut to crack take that from me;Msuya ana uadilifu gani wa kutusemea juu ya Rais tumtakaye ikiwa yeye anaishi na hatia ya kumwua Sokoine?Pengo ana uadilifu gani wakati benki ya kanisa lake ni taasisi ya utakatishaji fedha haramu?Kinana ana uadilifu gani wakati amemaliza tembo wetu?Kikwete aliye Rais wenu ana uadilifu gani wakati ameiba pesa za uma kupitia Escrow?Muwe mnafikiri kabla hamjaandika,otherwise kama hii inawasaidia kuondoa msongo wa mawazo kutokanana ugumu wa maisha basi go ahead and spread more lies
jiandae kisaikolojia....
 
My friend; tafadhali sana tofautisha "The real from the Ideal!!"; if wishes were horses; each and everyone of us would ride ONE!!
Wataongea mpaka mpaka mapovu yawatoke; watajipandisha mori na kujitia ukakasi; lakini katika uteuzi wa mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Majambazi (CCM); read my lips; Edward Ngoyai Lowasa is the man to beat !!!

Vinginevyo; tuanze sasa kuandika "Tanzia" ya CCM; na maandalizi ya kuikaribisha jamhuri ya pili ya Tanzania

Freedom is comming tommorow; Let freedom reign; Aluta continua.

Ndivyo ilikuwa inaonekana kabla ya mwaka huu kuanza, lakini mashambulizi haya yanaashiria kuna kitu nyuma ya pazia! Na nakwambia hakuna bahati mbaya kwenye siasa, kila kitu huwa kimepangwa.
 
Kwani Lowasa alishawahi kuwa msafi tangu lini.
 
Ni wale tu doubting Thomas ndio mpaka leo wanafikiri kwamba Lowassa atapita kizingiti cha CC ya CCM.

Ukweli mchungu ni kwamba mwisho wa ndoto ya matumaini ya Lowassa ni CC ya CCM. Hapo ndipo jina lake na majina mengine ya wana-CCM yatakapochinjiwa baharini.

Lowassa ameshaanza ku sense hilo na ndiyo chanzo cha vurugu zote hizo kuitisha CC ya CCM.

TEAM LOWASSA nawashauri waanze kutafuta ushauri nasaha, ili CC ya CCM itakapochomoa PANGA LAKE ALANI wasije wakafa kwa KISEBUSEBU NA KIHORO PAPO.
 
Mbona mgombea wa CCM 2015 Yupo wazi tu,,, Mgombe ni BENARD MEMBE,,, Lowassa kiukweli kikwete kesha msaliti siku nyingi,,
Katika watu wenye uwezo mdogo kabisa mmojawapo ni Membe! CCM wakitaka ianguke wamuweke MEMBE!
 
Edo anawatoa watu jasho balaa, hazuiliki huyu jamaa. Ni muda wa maamuzi magumu.
 
Lowasa atakapo gombea urais ameua chama hata kama ni upinzani.
 
Back
Top Bottom