Ukweli mchungu: Lowassa ameshatoswa na CCM

Ukweli mchungu: Lowassa ameshatoswa na CCM

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Jana nilimsikia Katibu mkuu wa Ccm redio Clouds, nadhani alikuwa Tanga akisema kigezo cha kwanza kwa mgombea atakayeteuliwa na Ccm itakuwa ni uadilifu. Alisema pia wagombea wa Ccm wanaoutaka urais itabidi wajipime kwa kigezo hicho namba moja. Ni juzi tu Mzee Msuya alisema Lowassa kama anaenda upinzani aende lakini chama hakiwezi kumpitisha fisadi kugombea urais.

Kama ni mfuatiliaji wa mambo ya iasa za nchi hii utajua kwamba Lowassa alikuwa karibu sana na viongozi wa dini, lakini juzi tu walitoka hadharani na kumnanga kama 'fisadi msaka Ikulu'. Hawa ni watu wanaheshimika sana na mara nyingi wanakuwa taarifa nyeti toka hata Ikulu. Mtu kama Pengo ni figure kubwa nchi hii, anajua yaliyo uvunguni Ikulu.Kama angekuwa amedokezwa kwamba ndiye mgombea wa Ccm ajaye asingethubutu kumchana hadharani au maaskofu wenzake kumnanga!

Wale 'Team Lowassa' mjiandae kisaikolojia kutupwa kwa mgombea wenu maana tangu imeanza 2015, hali inazidi kuwa mbaya. Mashambulizi yanatoka kila pembe tena kwa watu wanaoheshimika. Baba Askofu Mokiwa, Baba Askofu Pengo, Nzigirwa, Mzee Msuya! Mlishajiuliza hivi karibuni Pengo alienda kufanya nini Ikulu?

Tafakari!
 
Yan Lowassa amewafanya watu wengi waugue magonjwa ya akili;hofu na kiwewe kimewajaa...he's a hard nut to crack take that from me;Msuya ana uadilifu gani wa kutusemea juu ya Rais tumtakaye ikiwa yeye anaishi na hatia ya kumwua Sokoine?Pengo ana uadilifu gani wakati benki ya kanisa lake ni taasisi ya utakatishaji fedha haramu?Kinana ana uadilifu gani wakati amemaliza tembo wetu?Kikwete aliye Rais wenu ana uadilifu gani wakati ameiba pesa za uma kupitia Escrow?Muwe mnafikiri kabla hamjaandika,otherwise kama hii inawasaidia kuondoa msongo wa mawazo kutokanana ugumu wa maisha basi go ahead and spread more lies
 
Huyu ametumwa si bure... Utake usitake usikojoe uache ule ushibe ufe ufufuke, Lowassa ndo rais wa Tanzania kuanzia 2015..

Kwa mipasho kama hii inaonekana mmekata tamaa!
 
Mbona mgombea wa CCM 2015 Yupo wazi tu,,, Mgombe ni BENARD MEMBE,,, Lowassa kiukweli kikwete kesha msaliti siku nyingi,,
 
Lowasa hawezi kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM labda huko UKAWA anakopanga kwenda

Nawaambia hajazaliwa wa kumzuia Lowassa ndani ya ccm. Kwa nini ahamie ukawa wakati kwenye chama chake ana mchango mkubwa kuliko mwanachama yeyote alie hai? Hao kina kinana na maaskofu wake hawana ubavu. Edo ndio mtaji mkubwa wa ccm na ndie raisi wetu. Hao kina Msuya na maaskofu wana usafi gani wao?
 
Back
Top Bottom