Ukweli mchungu Kuhusu Loliondo

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
UKWELI KUHUSU LOLIONDO Naa Joseph #Yona

Mgogoro wa Loliondo umeshika kasi huku Catalyst mkubwa kwenye mgogoro ni wenzetu wa Kenya, Tanzania inaweka mpaka kwenye eneo la Km² 1,500 tu la Pori Tengefu, Km² 2,500 wanaachiwa ndugu zetu wafugaji waendelee na shughuli zao, Sababu ya Serikali kuchukua uamuzi huu ni kulinda hifadhi zetu za wanyama zisipotee.

NB:-Ukweli mchungu, kwa ushahidi kuwa Wamasai wa Loliondo kwa Upendo wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan amewapa Km² 2,500 na wanakadiriwa kuwa 70,000 tu lakini Dar Es Salaam nzima ina eneo la ukubwa wa Km² 1,393 watu zaidi ya Milioni 7?.

Eneo linalowekewa mipaka ni muhimu sana kwa hifadhi zetu hasa Serengeti kwa sababu eneo hilo ndilo linalotoa asilimia 48 ya maji yanayoingia Serengeti, Ndio eneo ambalo ni mazalia ya wanyawa, ndio njia ya Wanyama wanaohama hupita kutoka Serengeti kwenda Masai Mara Kenya, Pori hili ni Chanzo kikubwa cha Mapato ya Serikali kutokana na uwindaji na Utalii.

Shughuli za watu na ongezeko la Watu kwenye eneo hili ni tishio kwa Usalama wa nchi kwa kuwa Maji yakikauka eneo hili tutaua moja kwa moja Mbuga ya Serengeti, mbuga hii ikifa moja kwa Moja wanyama wote watahamia Masai Mara Kenya ambayo angalau ina sifa sawa na Serengeti.

Cha pili Mifugo mingi inayofugwa Pale Loliondo zaidi ya Asilimia 70 ni ya WaKenya, Ndio maana Serikali imekuja na Mpango wa utambuzi wa mifungo kwa kuleta sensa ya mifugo kwa kuivalisha hereni, hili ni pigo lingine kwa Kenya maana ili ngombe wako asajiliwe lazima mmiliki awe Raia wa Tanzania.

Tanzania itenge fedha kwa ajili ya program za Vijana kuwaelimisha na kulitambua taifa lao, kwani upotoshaji sugu unaendelea mitandaoni kutokea Kenya na wengine ni vijana wa Kitanzania hii inadhihirisha vijana wengi hawalijui Taifa lao na hawana uelewa Kuhusu RASILIMALI ZETU.
FB_IMG_1655711458794.jpg
FB_IMG_1655711642779.jpg
 
Kumbe ndo maana Kenya na Rwanda walikuwa wanasukuma agenda ya free movement of cattle flocks across EAC partner states for pasture! Shenzi kabisa. Sasa ndo naanza kuona hila nyuma ya hii kitu. Mungu saidia Tanzania ilikataa mpango ule ovu.
Agenda nyingi za EAC zimulikwe kisawasawa, ikionekana zinaleta hitilafu, tuwe tayari kurevise kama nchi, kama wataleta ugumu tunajitoa EAC, tunabase zaidi SADC.
 
Watakwama
 
UKWELI KUHUSU LOLIONDO Naa Joseph #Yona

Mgogoro wa Loliondo umeshika kasi huku Catalyst mkubwa kwenye mgogoro ni wenzetu wa Kenya, Tanzania inaweka mpaka kwenye eneo la Km² 1,500 tu la Pori Tengefu, Km² 2,500 wanaachiwa ndugu zetu wafugaji waendelee na shughuli zao, Sababu ya Serikali kuchukua uamuzi huu ni kulinda hifadhi zetu za wanyama zisipotee.

NB:-Ukweli mchungu, kwa ushahidi kuwa Wamasai wa Loliondo kwa Upendo wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan amewapa Km² 2,500 na wanakadiriwa kuwa 70,000 tu lakini Dar Es Salaam nzima ina eneo la ukubwa wa Km² 1,393 watu zaidi ya Milioni 7?.

Eneo linalowekewa mipaka ni muhimu sana kwa hifadhi zetu hasa Serengeti kwa sababu eneo hilo ndilo linalotoa asilimia 48 ya maji yanayoingia Serengeti, Ndio eneo ambalo ni mazalia ya wanyawa, ndio njia ya Wanyama wanaohama hupita kutoka Serengeti kwenda Masai Mara Kenya, Pori hili ni Chanzo kikubwa cha Mapato ya Serikali kutokana na uwindaji na Utalii.

Shughuli za watu na ongezeko la Watu kwenye eneo hili ni tishio kwa Usalama wa nchi kwa kuwa Maji yakikauka eneo hili tutaua moja kwa moja Mbuga ya Serengeti, mbuga hii ikifa moja kwa Moja wanyama wote watahamia Masai Mara Kenya ambayo angalau ina sifa sawa na Serengeti.

Cha pili Mifugo mingi inayofugwa Pale Loliondo zaidi ya Asilimia 70 ni ya WaKenya, Ndio maana Serikali imekuja na Mpango wa utambuzi wa mifungo kwa kuleta sensa ya mifugo kwa kuivalisha hereni, hili ni pigo lingine kwa Kenya maana ili ngombe wako asajiliwe lazima mmiliki awe Raia wa Tanzania.

Tanzania itenge fedha kwa ajili ya program za Vijana kuwaelimisha na kulitambua taifa lao, kwani upotoshaji sugu unaendelea mitandaoni kutokea Kenya na wengine ni vijana wa Kitanzania hii inadhihirisha vijana wengi hawalijui Taifa lao na hawana uelewa Kuhusu RASILIMALI ZETU.View attachment 2266384View attachment 2266386
Huna lolote unalolijua kuhusu hicho ulichoandika. Wewe endelea tu kulamba viatu vya hao mabwana zako. Ccm inastawi kwa watu wenye akili ndogo kuliko Wewe. Wakati serikali inatoa eneo la Loliondo kwa mwarabu Wakenya walishiriki kwenye hilo? Mnakaririshwa tu mambo ya propaganda kama makasuku na wewe unatoa mashudu tu.
 
Back
Top Bottom