CHADEMA kimejijenga kama tumaini mbadala wa CCM kutokana na hali duni na na kukata tamaa kwa watanzania kunakosababishwa na ubovu wa CCM wa kutojali na kushughulikia matatizo ya msingi wa wananchi kama afya, elimu , maji na miundombinu bila kusahau haki za binadamu na utawala bora.
CHADEMA kimejidhihirisha kama chama mbadala na kuungwa mkono na watanzania wengi hivyo kuongeza idadi ya wabunge wake hapo 2010 na pia kupata kura nyingi za urais katika uchaguzi huo.
HALI YA SASA.
CHADEMA imeanza kujisahau, viongozi wa juu hasa mbowe na slaa wamegeuka kutaka kuifanya CHADEMA mali yao binafsi ( HUU NI UKWELI HATA KAMA KUNA WATU WATATUKANA HAPA) , mchango wao katika kukijenga chama ni dhahiri ila waelewe chama sio chao , chama ni cha wanachama wanaopigwa mabomu na kuvumilia jua na mvua kwenye mikutano ya hadhara, wametengeneza makundi ndani ya chama kisa urais na uenyekiti, wameunda vitengo vya usalama bila kushirikisha viongozi wengine wa chama hi sio sahihi na haya yanayotokea sasa ni mavuno ya hila hizo kama JK anavyovuna athari za udini kupitia CCM. Huwezi kuwa na intelejensia ya chama wakati baadhi ya viongozi wenzio wa juu hawaijui, lazima ipo pale kuwamaliza ndio tafsiri ndogo tu.
Wabunge wa CHADEMA wanalalamika, MBOWE umeshindwa kuonyesha msimamo unatumia shangingi la serikali huku ukipinga manunuzi ya magari hayo, wanataniwa bungeni na kweli inaleta aibu kimsimamo, kuna malalamiko kuhusu wabunge baadhi wa viti maalumu kuwa walipendelewa, angalia kina shonza wanapata point sababu mbunge kama mukya hajawahi kusikika bungeni akitoa hoja yeyote , watanzania wanamini katika shutuma hizi, inaondoa umbadala wa CCM.
Suala la KM na mchumba wake pia lina walakini hasa kwenye utendaji na uingiliaji wa masuala ya chama, RAI yangu kwa viongozi hawa mjitafakari pia kabla ya kutupia mawe kwa usalama wa Taifa, kuweni wasafi na ishi kwa kadri ya maneno yenu ili kuimarisha imani ya watanzania kwa chadema.
Tunapoelekea, baada ya katiba mpya kama CHADEMA haitobadilika, watanzania watachagua wagombea binafsi na watakuwa wengi bungeni kuliko wanachama wa CHADEMA.Huu utakuwa mwisho wa vyama vya siasa visivyoishi kauli zao.
wenye kutukana tukaneni, wenye kukejeli sawa.ILA BADO HUU NI UKWELI MCHUNGU, PAMOJA NA CCM KUTOFAA, BADO HATA CHADEMA HAIJAFAA KUPEWA NCHI KWA SASA