Ukweli kuhusu vibanda vilivyochomwa moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu vibanda vilivyochomwa moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, May 12, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Written by Stonetown (Kiongozi) // 12/05/2011 // Habari // 3 Comments

  [​IMG]
  Ukweli kuhusu vibanda vilivyojengwa vya wafanyabiashara ya vinyago eneo la Pwani Mchangani, Kaskazini Unguja ni kama hivi: Ukweli ambao SMZ-GNU hautaki kuusema kwa faida yao na matakwa yao zaidi ya kisiasa. Soma maelezo sahihi na uchambuzi wa kina:
  - Vibanda hivi vimejengwa bila kibali cha aina yeyote ile au ya umiliki wa ardhi. Na kama kipo tunaomba tuonyeshwe. Balozi Seif Ali Iddi anajua hilo, lakini amekurupuka na kuzungumza siasa zaidi ya kutaka kukamilisha agenda yake ya Tanganyika. Nina challenge balozi Seif Ali Iddi atuonyeshe hati miliki ya hao wamachinga wa hapo. Jamani, tuzungumze sheria, na haki, sio hamasa wala siasa au chuki.
  - baada ya kuvamia, wamejenga kanisa, jambo lililowakera wananchi wazawa wa hapo. Balozi Seif Ali Iddi anisute kama sio kweli.
  - wanakijiji/wazawa, walilalamika kwa serikali, za wilaya, mkoa na serikali kuu kuhusu kadhia hiyo, hakuna lililochukuliwa, smz imepuuza madai ya wananchi wake. Leo, yametokea mengine, wanajaribu kugeuza kibao kwa wenyeji. Uonevu gani huu, ndani ya nchi yetu. Madai ya wananchi yapo hai, tena kwa maandishi na kesi ipo, files zipo. Madai yao yapo halali kabisa, lakini walipuuzwa kwa sababu wao ni wenyeji, na wamekuzwa watu wageni wasiokuwa na hata saa moja ya kuishi Zanzibar. Sasa, OK, tujaalie SMZ iamue kuwalipa watoto wa wafalme, wataanzia wapi; any document ya kuhalilisha malipo au uhalali wa umiliki wao hapo, kisheria; tusiende kisiasa.
  * Jamani, tunataka kuambiwa nini na Balozi Seif Ali Iddi, Charlie Chaplin. Nilisema awali kuwa huyu Seif NO.2 siye/hatufai. Na kadhalika Seif NO.1; pia ni mzigo kwetu kwa maslahi ya Zanzibar.
  Hiyo ni SET NO .1
  SET NO.2 ya mazungumzo yetu:
  - hoteliers pia wamelalamika sana na watu hawa – NO action. Kamisheni ya utalii pia wamekereka na watu hawa – no action: kwa sababu wanaiharibu sekta yote ya utalii Zanzibar.Hoteli nyingi ama zinakosa biashara kwa kuwepo vibanda vile pale. How? wageni wao wanaibiwa, wanakuwa harrased na hotels zinakosa ‘positve image/good image’ kwa kuzungukwa na vibanda hivyo. Hoteli ya fur star worth over 20m dollars, imezungukwa na kibanda cha shilingi elfu kumi. Uoza mtupu. Sekta ya utalii inakufa kutokana na wauza ugali na vinyago hawa. Hii ni serious, na naomba SMZ na nyie wote muitazame huko, kama angle ya biashara zaidi /sio siasa zaidi.
  SET NO.3 ya amzungumzo yetu:
  - biashara gani walikuwa wanafanya hawa watoto wa wafalme?
  1. Kuuza Vinyago
  2.Kuuza pombe/madawa ya kulevya
  3.Uhalifu wa kupindukia.
  4.Ukahba.
  Katika uhalifu, iliwahi kukamatwa hata silaha katika mabanda hayo, ingawa polisi imebana kimya. Haya na mengine , mstahiki balozi seif ali iddi hataki kuyasema wala hatoyasema maisha.
  Angalia ufedhuli wa watu hawa, jana wanasoma risala mbele ya Seif Ali Iddi na kusema kuwa kama serikali haitochukua hatua, wao watachukua hatua mikononi mwao. Huyu eti ni VP 2 wa nchi, na watu wanamwambia watavunja sheria, yeye na timu yake, wanacheka. Watu wanafikiria kulipiza kisasi, au kuuwa, au kufanya hujma, yeye mwenzetu anaona rahaaa, na anacheka kwa kuraha. Keli tumepata vingozi au tumepatikana.
  Lakini yote hayo ya nini? Hayo ni mambo yamepanga na system. Inawezekana waliochoma moto ni serikali au hata hoteliers, au hata wengine xxxx! ili kukamilisha agenda yao. Mnaijua?
  Jawabu: katiba mpya. Kwa vile mmeikataa, sasa wanabuni tension, ili kukamilisha agenda hiyo.
  Bottomline: lazima katiba mpa iwe by 2014, kama alivyosema au anavyotaka JK.
  Sasa Zanzibar kuanzia siku mliyoikataa mswada wa katiba mpya, mpaka 2014 – mtaona mambo mengi ya ajabu ajabu – popobawa atarudi, wale ramba ramba watarudi, vitisho, na visa, na mikasa mingi tu mtaiona. Ushindi lazima, na lazima katiba mpya ipite, na lazima Zanzibar tuifute katika ramani ya dunia…kwa utaalamu na kisayansi.
  Tusisahau kuwa katika kuchomwa moto vibanda hivi upo mkono wa kanisa.
  Unajua huko nyuma sana, nilisema kwa sauti kubwa kuwa Seif NO.1 na NO.2 hawatufai, na ni lame duck – niliambiwa sijui niko CUF, wengine wakasema mimi CCM. Ahhhh…jamani: mimi atayesema ni CUF – basi mimi ni CUF aliyekata kamba zizini; na atayesema mimi CCM; basi mimi ni CCM mfu – sina mbele, sina nyuma. GNU, narudia tena haitufai; inazidi kutuletea matatizo.
  - Na Maalim seif mwenyewe (menyewe….baba dogo veve, amekiri juzi jamat khan) kuwa hawawezi kutatua matatizo ya wananchi, na ametoa visingizio miteni kidogo. Mwisho hana la kusema anasingizia eti pirates wa Somalia, ndio wamesababisha kupanda kwa bei ya vyakula. Balahau bora sasa ukae na uandike vitabu vya comedy. Maalim Seif bora aungane na akina Chimbeni Kheri au Mr.Bean, watupatie tales za vichekesho.
  Mwisho,nimesitikitika zaidi kuona waandishi kama Salma Said, naye amejaa tele katika hamasa na kuandika lugha mbovu kabisa, iweje yeye aandike neno ‘vibanda vya wabara’. si aseme tu, vibanda vya wafanya biashara……yaani wazanzibari wote tumetekwa akili zetu na watu hawa.
  Inasikitisha sana.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,445
  Likes Received: 22,362
  Trophy Points: 280
  Malaria Sugu sijui ni lini itakuisha. Najua unasapoti huo utumbo kwa kuwa jamaa walijenga KANISA.
  Sina jina la kukuita.
   
 3. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,394
  Likes Received: 8,528
  Trophy Points: 280
  nyie waunguja kweli kweli. ha ha ha[​IMG][​IMG][​IMG]
   
 4. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Tunao wapemba huku bara wana biashara zao na wapo maofisini, nyie anzeni sisi tutamaliza, maana aliye kwenye nyumba ya vioo kaanza tupa mawe
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Haya tumekusikia...sijui ali saleh vile
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  naona kuwa wewe pia ni moja wa waliochoma kwani msimamo wako ni kulaumu ujenzi wa kanisa , kulaani uuzaji wa vinyago, kudai hati miliki ya ardhi, lakini pia unajua kwamba kuchukua sheria mkononi ni kosa na unasema ni vibanda vya wafanyabiashara siyo wabara wewe unasema hawana hata saa 1 ya kushi zanzbzr, mbona hamjavichoma pale mjini wanapofukuzwa wafanyabiashara na serikali? Nao si wafanya biashara?
   
 7. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Unaonyesha dhahiri kwamba una choyo fulani hivi na Wapemba. Jitahidi tu Mungu yupo atakuona na utafanikiwa siyo usubiri mali ya Wapemba ukawafanyie ujambazi.

  Vibanda vimechomwa Unguja wewe umeng'ang'ania na Wapemba tu kwenye maelezo yako. Angalia kijana usipate pressure ukafa mapema.
   
 8. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  2 way side, inawezekana ni kweli unayodai, na vyombo vya habari vimelikuza, na pia SMS inaagenda yake, labda great thinkers inabidi waelewe hii hali, kama ilikuwa (mfano) inasababisha usumbufu kwa watalii, then govt ipo kimya, na ustawi wa jamii maeneo hayo unashuka kwa kuuziwa madawa ya kulevya na uharifu, hawakuwa na budi kuionesha gvt kikomo cha uvumilivu.
   
 9. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein serikali yake inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo kero mbali mbali za wananchi ambazo zinaonekana kukosekana kuchukulikiwa hatua zinachochea cheche za uvunjifu wa amani nchini

  Sita mahakamani kwa kuharibu mali
  JUMLA ya watu sita jana wamepandishwa katika mahkama ya mkoa Vuga Mjini Zanzibar wakikabiliwa na tuhuma za kuchoma moto mabanda ya wafanyabiashara katika kijiji cha Pwani Mchangani wilaya ya Kaskazini Unguja.
  Walioshitakiwa ni ni pamoja na Mohammed Masoud Afadhali (21), Mwinyi Abdallah Msanif (22) na Hassan Makame Chande (21) wengine ni Haji Ame Idd (45), Talib Faki Ame (60) na Mohammed Haji Sheha (21).
  Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Mohammed Khamis Hamad Mwanasheria wa serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), aliieleza mahakama hiyo kwamba mnamo tarehe 5 Mei watuhumiwa hao wote kwa pamoja walichoma moto mabanda ya biashara na kusababisha hasara kubwa.
  Alisema watuhumiwa hao wanakabiliwa na kosa ya kuharibu mali kinyume na kifungu cha 324 (a) cha sheria namba 6 sheria mwaka 1984 katika sheria za Zanzibar.
  Washitakiwa hao walielezwa mahakamani hapo kwamba kwa pamoja walichoma moto mabanda ya wafanyabiashara ya wajasiriamali na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha za wafanyabiashara hao katika maeneo yao ya biashara mashitaka ambayo kwa pamoja walikana kufanya kosa hilo .
  Mwanasheria huyo alisema watuhumiwa hao wamesababisha hasara kubwa kutokana na uamuzi wao wa kuchoma moto maeneo ya bishara ambapo jumla ya shilingi milioni 80,470,000 pamoja na paundi 70 za Uingereza na dola 60 za Marekani zimeteketea katika tukio hilo la uchomaji moto mabanda hayo .
  Washitakiwa hao walipotakiwa kujibu shitaka hilo walikana, ambapo upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wake bado unaendelea.
  Baada ya hoja hizo za upande wa mashitaka, upande wa utetezi unaosimamiwa na Wakili wa Kujitegemea Abdallah Juma uliwaombea wateja wake wapatiwe dhamana kwa vile ni haki yao kikatiba kupewa dhamana .
  Alisema kuwa, kwa kuzingatia kifungu cha 150 (1) cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar , shitaka linalowakabili ni miongoni mwa mashitaka yenye dhamana hivyo wanapaswa kupewa dhamana .
  Aidha wakili Juma alidai kuwa, kifungu hicho kimeainisha mashitaka yasiyokuwa na dhamana ambayo ni uhaini, mauaji, wizi wa kutumia silaha pamoja na kusafirisha dawa za kulevya, na kubainisha kuwa shitaka linalowakabili wateja wake ni shitaka lenye dhamana.
  Wakili huyo alisema kwamba wateja wake wana wadhamini madhubuti na wapo tayari kutekeleza masharti yote ya dhamana watakayopewa, sambamba na kuhakikisha wanawafikisha mahakamani kila watakapohitajiwa wakati kesi yao ikiendelea.
  Upande wa mashitaka ukiongozwa na Mohammed Khamis ulipinga hoja hizo za upande wa utetezi na kuiomba mahakama hiyo isiwapatie dhamana washitakiwa hao, kwa madai kwamba hatua hiyo ya dhamana inaweza kuingilia kati upelelezi ambao bado haujakamilika.
  Mwendesha mashitaka huyo alidai kwamba, hivi sasa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea, na kuna washitakiwa wengine bado wanatafutwa ili waweze kuunganishwa katika kesi hiyo pamoja na wenzao.
  Licha ya pingamizi hizo, Mwendesha Mashitaka huyo alikubaliana na upande wa utetezi kuwa dhamana dhidi ya washitakiwa hao ni haki yao ya msingi nay a kikatiba lakini aliiomba mahakama hiyo iwapo itaamua kuwapatia dhamana izingatie ukubwa wa kosa hilo lililotendeka.
  Hakimu wa Mahkama ya Mkoa Vuga George Joseph Kazi aliwaamuru washitakiwa hao kwenda rumande hadi Mei 23 mwaka huu, ambapo ombi lao la dhamana litakapozingatiwa siku hiyo na kesi hiyo kuakhirishwa.
  Wakati kesi watuhumiwa wakifikishw amahakamani hapo mamia ya wananchi kutoka sehemu mbali mbali hasa kutoka vijijini walionekana kufika katika mahakama hiyo ya Vuga kuja kusikiliza kesi hiyo inavyoendeshwa huku baadhi ya wananchi hao wakiwa wamekaa nje ya mahakama kutokana na kuwa sehemu ya mahakama hiyo ni ndogo kulingana na wingi wa wananchi waliofika.
   
 10. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,172
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Hapa napata jibu moja tu, NI UBAGUZI (WATANGANYIKA NA WAZANZIBAR; WAKRISTO NA WAISLAM).

  My take Watanganyika na wakristo hawatakiwi Zanzibar.

  Pendekezo:

  Tuuvunje muungano kila mmoja kivyake, na tunapofikia hatua hiyo Wazanzibari wote mlioko huku Tanganyika mjiandae kung'oa majumba yenu mpeleke kwenu.
   
 11. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Athari za usultani, mmezoea ubaguzi. Leo mnawabagua waafrika wenzenu wabara huku mkitumia visingizio rahisi kama kanisa, kelele kwa wazungu, vibali feki, historia uchwara. Zamu yenu ikifika mliivyo laini laini sijui itakuwaje!
   
 12. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo kny ubaguzi umemaliza mazee,hii mijamaa sijui vipi!
   
 13. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  narudia tena...watu wengi wana-comment ishu za muungano kinadharia...mimi nimekuwepo kule...hawa jamaa wana chuki iliyopitiliza dhidi ya wabara na wakristo!! hivi hakuna mtu/watu wanaoweza kutoa demonstration kwa wazenji huku bara?? japo mara 1 tu kuwastua!!???
   
 14. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ni kweli mkuu ni ubaguzi maana Wazanzibari wako katika nchi kadhaa duniani wala hawakuungana na nchi hizo.

  Walihama kwao kwa fitna zenu na kama nyinyi mna uchoyo tu mali zao mnazitaka, watarudi.

  Na baada ya miaka kumi, mtawaomba msaada hao hao kwa kuendekeza ufisadi.

  Nchi yenu tajiri, wananchi wake maskini.
   
 15. M

  Maga JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Muungano huu mbona unatuumiza sisi wa bara tu? Kuna dalili zote kuwa wazanzibar hawatutaki sisi, si bora tuuvunje tu
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  abdulahsaf, umejichanganya sana kwa maelezo yako yasiyoeleweka, lakini kusudio lenu kubwa lilikuwa ni kuchoma moto KANISA na siyo mabanda ya wafanyabiashara.
   
 17. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama tukianza kutimuana eti kwa sababu hawa Wamejenga Kanisa, na huku sisi Wabara tukianza kuwatimua hawa Wachuuzi wa Kipemba pamoja na Majini yao, je mna mahali pa kuwaweka huko!

  Angalieni uvumilivu huu usije ukaisha na huku Bara, sijui Mtawapeleka wapi Majini yoote ya Wapemba watakayofukuzwa nayo toka huku Bara!
   
 18. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Laini nyinyi mliopata nchi kwa karatasi, sisi tumeipata kwa kupigana Mkuu.
   
 19. K

  Kabathe Member

  #19
  May 13, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja ameegemea upande mmoja, upande wa kulaumu na inaonekana ni mbaguzi. Hatakama hawakua na vibali, aihalalishi kuvunja sheria. Hatua ya mwisho ya kudai haki ni kwa MAANDAMANO na si kufanya vurugu na kuwa rudisha wenzanko ktk umasikini. Na kama ni swala la vibali na biashara zingine ambazo si alali mbona tunasikia vibanda vya wazenji zilibaki. Serikali iwachukilie hatua hao wazunja sheria.:mod:
   
 20. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... unfortunately, dhana ya ubaguzi itawatafuna tu. ukaburu wao utawarudi wenyewe. it is a historical phenomenon.
   
Loading...