Ukweli kuhusu ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
UKWELI KUHUSU UJENZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa yeye mwenyewe anaeleza, ananukuliwa kama ifuatavyo:

"Sikuwashinikiza nilitaka watumie busara zao tu. Ilikuwa hivi, wakati ule Rais alifanya uamuzi wa kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Alikuwa ametoka marekani yule tajiri mkubwa Bill Gates alikuwa amemuahidi angemjengea Centre of Excellence na Teknohama akamuahidi kwamba angejenga, lakini alipokwenda marekani kwenye ziara aliporudi hakupata matumaini makubwa kama ilivyokuwa pale mwanzo kwahiyo akanieleza tufanye jitihada ambazo tunaweza ili tujenge chuo kikuu kwasababu tumeshawaahidi wananchi, kwahiyo hatuna budi kujenga.

Kwahiyo siku moja nikawaita wakuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Niliwaita Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma, tukazungumza, tulizungumza vizuri, lakini hatimaye niliwaambia kwamba tumepewa kazi na serikali ya kujenga chuo kikuu cha Dodoma. Hatuna rasilimali wala fedha za kujengea, isipokuwa kuangalia hii mifuko ya jamii mnaweza kutusaidiaje? Kila mmoja akazungumza.

Wako waliokubali, wapo waliokataa. Wengi walikataa wakiniambia kwamba wamewekeza sana katika real estate (ujenzi wa nyumba) na pengine ni vizuri wakapunguza. Sikukubaliana na taarifa hizo kwasababu nilikuwa najua kuwa wanawekeza kwenye majumba ya watu binafsi na mashirika ya Umma. Hili kwangu mimi lilikuwa ni suala la kufa na kupona, ni uamuzi ya rais na tuna mahitaji ya wanafunzi kusoma.

Dunia yote watu wanaosoma wapo vyuo vikuu, sisi tuna population (Idadi ya watu) inayokua kiasi hicho, tusipoongeza vyuo vikuu itakuwa taabu sana, Kwa hiyo nikawasikiliza nikawaambia, nimewasikiliza lakini sikubaliani nanyi. Nikawaambia huyu hapa vice chancellor (makamu mkuu wa chuo).

Nikawaambia huyo ndio Vice Chancellor. Huyu bwana anajua eneo lote ambalo tunataka kujenga chuo kikuu nendeni naye, kila mmoja atamuonyesha mlima (eneo) wake. Angalia mlima wako, chagua mlima wako, fikiria, halafu tukutane kesho asubuhi.

Yule ambaye anataka kujenga tutaingia naye mkataba, yule ambaye hayupo tayari kujenga aje na barua yake ya kuacha kazi na kuchukua dhamana ya kukubali kujiuzulu kwake. Wote wakakubali na chuo kikajengwa.

Tumejenga kuliko uwezo na naambia sasa hivi kuna majengo yapo wazi. Tunajifunza nini, kwamba tuna uwezo wa kufanya vitu katika nchi yetu. Tukiamua kufanyia uamuzi, tunaweza kufanya makubwa zaidi."
 
Lowassa bana!hata mradi wa maji toka ziwa victoria alisema kajenga yeye mpaka Anthony Diallo akaja kumuumbua.
Lowassa angejielekeza katika kukiimarisha chama cha chadema chenye migogoro lukuki,badala ya kulilia ujiko
 
Tukubali alijenga yeye kwa kutumia hela za Mifuko ya hifadhi za jamii. Sasa chuo kinadaiwa na mifuko haina hela. Walichokifanya ni kutoa Fao la kujitoa ili waweze kumaliza wanachama!!!
 
Chuo hiki kilijengwa na Kikwete (apewe maua yake) na msukumo wa kukijenga uliwekwa na Lowassa baada ya kukutana na viongozi wa mifuko ya kijamii na kuwaeleza lengo la serikali japo hawakuwa na fedha. Mwanzoni Melinda and Gates foundation waliahidi kukijenga lakini baadae ni kama mambo hayakukaa sawa na hapo ndipo serikali iliamua kuingia mikataba na !ifukomya kijamii ili kukijenga chuo hiki. Kwa hili mwenyezi Mungu aendelee kumtunza mzee wetu Kikwete na swahiba wake mzee Lowassa.
 
Lowassa bana!hata mradi wa maji toka ziwa victoria alisema kajenga yeye mpaka Anthony Diallo akaja kumuumbua.
Lowassa angejielekeza katika kukiimarisha chama cha chadema chenye migogoro lukuki,badala ya kulilia ujiko
Kama kuna vitu huvijui si lazima kutoa comments, kati hili la UDOM ni lipi la uongo kuhusu Lowassa? Hata huo mradi wa maji ya ziwa Victoria kama usingekuwa msimamo wa Lowassa, Misri (Egypt) ilikuwa tayari imeshaupiga vita. Unatuletea habari za majungu na wivu wa Diallo, haya alikwambia kajenga yeye?
 
Back
Top Bottom