Ni kweli kwanza inabidi ujue watts ngapi unahitaji. Rahisi kukadiria hizi kwa sababu vifaa vyote vya umeme huandikwa watts zake (au Amps na Volts - Ohm's law itakupatia Watts)
Nyumba ndogo inahitaji kama 3KWatt (nakisia hapa inategeme vifaa). Kwa kweli ni gharama kubwa kujitegemea kiumeme. Bila ya grid (Tanesco ) inabidi uwe na mchanganyiko wa solar, windmill na stand-by generator ili likikosekana jua au upepo utategemea generator.
Tatizo kubwa la umeme wa solar (au wind) ni jinsi ya kuuhifadhi umeme wakati unatengenezwa ili siku za mawingu au usiku uchote umeme kutoka kwenye hifadhi yako. Njia rahisi inayotumika kuhifadhi umeme ni kutumia deep-cycle batteries . Kawaida hizo huwa na uwezo wa 12V. Unatakiwa kutengeneza Battery Bank kwa kuzipangilia battery kama 4 mpaka 8 in parallel or series kutokana na mahitaji ya vifaa vyako.
Kwa ufupi vitu unavyohitaji:
1. Solar Panels (ziko aina nyingi hizi - Tahadhari na wabongo wasikuuzie vioo vya kichina)
2. Charge controller (kwa sababu ya kurekebisha umeme unaotoka kwenye panel usizidi na kuharibu battery)
3. Invertor - Kubadilisha umeme wa jua DC kwenda kwenye umeme wa nyumbani AC. Hizi ziko ambazo unaweka ukutani kwenye plug na ina-supply kwenye circuit yako ya nyumbani.
4. Deep cycle batteries ( hizi ziko kama battery za magari )
Ushauri wangu binafsi ni upate kama solar panels 3 au 4 za 250Watts/each na circuit yako iwe inakunywa umeme kwa matumizi ya taa, fans na vifaa vidogo vidogo. Achana na vifaa vikubwa kama vile Oven.
Kwa kweli ukishapata vifaa hivyo (ukimpta mdau akakutolea China bei poa) kufunga ni rahisi sana unahitaji elimu ya darasa la saba tu. Uchawi wa umeme wa jua ukishavifunga vifaa vyote basi unacheka tu kwasababu hamna bili tena na hivi
vitu hudumu kama miaka 30 hivi. Angalia mchoro hapo chini.
¬K
[1] Mchoro unaonyesha bulbu inachukua umeme moja kwa moja kutoka kwenye charge controller bila kupitia kwenye Invertor.Kwa hiyo bulbu zitakuwa zinatumia umeme wa DC ?.
Umeme unaotoka kwenye inverter ndio unaelekea kwenye circuit ya nyumba na una-power vifaa nyote vya nyumbani.[2] Mchoro unaonyesha pia vifaa kama computor vitakuwa vinapata umeme uliobadilishwa kwa maana ya kupitia kwenye Inverter kutoka umeme wa DC kwenda umeme wa AC ?.Naomba kujuzwa kama niko sahihi au kuna mahali nimechemka ?.
Nisaidie ili kama siyo nione uwezekano wa kuitumia kwa pasi pia.
Naomba utupatie specs ya hiyo installation yako. Natanguliza shukrani.Binafsi natumia solar power kwa miaka miwili sasa na tanesco hata sitaki kuwasikia hata kidogo na nimeshauri marafiki zangu nao wamefunga solar
Solar power inategemea na load utakayo funga
nakushauri ukisie mahitaji yako halafu upost na mie niakupa data zote na contacts numbers za wapi unawaza pata at whole sale prices
Mimi naombeni data wapi nitapata mitambo ya 'wind energy' hapa kwangu kuna upepo mwingi tu 24x7!
Binafsi natumia solar power kwa miaka miwili sasa na tanesco hata sitaki kuwasikia hata kidogo na nimeshauri marafiki zangu nao wamefunga solar
Solar power inategemea na load utakayo funga
nakushauri ukisie mahitaji yako halafu upost na mie niakupa data zote na contacts numbers za wapi unawaza pata at whole sale prices