Ukweli kuhusu siasa za zanzibar.

farsyyy

New Member
Jan 13, 2016
1
0
TUAMBIZANE UKWELI HATA KAMA UNAUMA

Unapoona watu wanaojiita vijana, tena eti wasomi tena eti waswalihina wenye mijisijida kama vifuu wanaelekeza na kusimamisha msingi wa siasa zao katika ubaguzi wa uPEMBA na uUNGUJA na uCCM na uCUF basi ujue sasa nchi inanukia hatari.

Wazanzibari tumegubikwa na chuki, choyo na unafiki wa kizanzibari. Lakini haya hatupendi kuyasema wala kuyasikia sababu ni RAHISI zaidi kuwalaumu ''vichogo" na "zimwi" liitwalo TANGANYIKA.

Sio ajabu kuwasikia baadhi ya Wazanzibari wanasema eti "Wallahi ningekuwa na uwezo ningeifukuza mipemba yote" akaa! au "Tukipata nchi yetu vichogo wote kwao" au "Mijitu ya Unguja yote mibunju, mijinga" akaa! Tunaitana majina mabaya mabaya kama magozi, mabunju, magozi, wakuja .. halafu eti tunaranda na mitasbihi mirefu kama minyororo eti tunastaghafiru.
Adui nambari wani wa Zanzibar ni Mzanzibari mwenyewe. Tusitafute mbali.

Baba yangu alinifunza hivi:
"Usikubali hata siku moja kudharauliwa au kudhalilishwa kwa rangi yako, kabila, umaskini au dini yako.Lakini kamwe na wewe usimbague mtu hata siku moja kwa misingi hio." Sasa tujalie ushauri wa baba siutaki na nikaamua kutukana na kubagua; nitabagua nani nitamuacha nani?
Babu yangu mzaa baba: Muarabu wa kabila la al Zakwani kutoka Oman.
Bibi yangu mzaa baba: Mpemba mwenye asili ya Kizaramo.
Mama yangu: Mkongo, wazee wake wakongo + chembe chembe za Rwanda.

Lugha zangu: Kiswahili, Kifaransa, Kiingereza na nyenginezo. NIMBAGUE NANI NIMUACHE NANI?

NAAMINI Zanzibar inaweza kutoka hapa kwani ubaguzi wetu sio wa kijadi per se bali wa kimfumo ambao umepandikizwa na watu flani kwa maslahi yao binafsi.Naendelea kuwa na 'DREAM' kwamba iko siku utawala wa sheria utatamalaki Zanzibar na kwamba wana wote wa MAMA Zanzibar watakuwa sawa mbele ya sheria bila kujali rangi zao, dini zao au maeneo wanakotoka.

Msingi wa 'DREAM' hii ni mapinduzi matukufu ya Zanzibar, kama alivyo 'ENVISION' mzee Karume.

KIZAZI KIPYA KINAPASWA KUPINGA UBAGUZI KWA NGUVU ZOTE.

NAPINGA UBAGUZI KWA NGUVU ZANGU NA AKILI ZANGU ZOTE.

EWE MWENYEZI MUNGU NISAIDIE.
 
Back
Top Bottom