Mkwaruzo
JF-Expert Member
- Feb 21, 2011
- 563
- 98
Assalam 'Alaykum. Leo napenda na mimi nizungumzie machache kuhusu ukweli juu ya SENSA iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kama wasemavyo wengine (hata humu pia wamo).
Mambo mengi ambayo yanayofanyika nchini mwetu au hata katika nchi nyengine Afrika huwa yanapatiwa misaada (yanafadhiliwa) ili yaweze kufanyika na kufanikiwa kwake bila ya kuwepo kikwazo cha pesa. Na baada ya misaada hiyo kupatikana na kupangwa bajeti ya kitu husika kinachotakiwa kufanyika, pesa inayobaki, huingia katika makucha ya viongozi wetu waliyo na tamaa na uchu wa pesa na kugawana. Na ni kama hivyo ndivyo ilivyotokea katika sensa.
Viongozi wa kiislam waliiambia serikali kuhusu kuwekwa kipengele cha dini katika dodoso za sensa tokea mapema (tokea machapisho ya madodoso ya sensa hayajachapishwa). Lakini walipuuzwa na kudharauliwa. Serikali ikakataa kuweka kipengele hicho na kutoa sababu zisizo za msingi, kwani walishindwa kukubali kwani kufanya hivyo ni kuenda kinyume na amri ya kanisa. (Laiti wangeliambiwa baada ya machapisho hayo, wangelipata sababu kibao za kusema "ooh! mmechelewa kutuambia" oooh, hatuna pesa" yani blaa blaa zingelikuwa nyingi).
Serikali kwa kuhakikisha lengo lake linafanikiwa bila kipengele cha dini kuwepo, iliwabidi watowe madodoso mapya ya vitambulisho vya Mtanzania ili kuweza kuuliza hadi idadi ya watoto uliyo nao, kitu ambacho hakikikuwepo katika bajeti. Vitambulisho hivyo kwa kiasi fulani pia viligomewa baada ya waislamu kujua mchezo wa serikali juu ya hilo.
Mwanzoni taasisi za kiislam zilionesha msimamo wa ajabu katika kuigomea sensa kwani hata BAKWATA nao walikuwemo katika hilo. Lakini walikuja kubadili msimamo baada ya kununuliwa (kupewa pesa) na serikali na kutakiwa wawe wahamasishaji waislamu kuikubali sensa. Pia serikali ililipia katika vyombo vya habari ili kuhamasisha watu zaidi kitu amacho kimepelekea hata makarani wa sensa kutolipwa pesa zao za awamu ya pili.
Kamata kamata za hapa na pale zilijitokeza na zinaendelea hadi sasa, ila taratibu zinafanyika na wanaokamatwa huachiwa. Yote hiyo ni tisha tisha. Baadhi ya vituo vya polisi wamewekwa makarani ili ukitaka uachiwe huru sharti ukubali kuandikwa kwanza.
Mnamo siku ya kwanza tu, walisifia uendaji wa sensa na kupotosha ukweli wa mambo ili kutuvunja moyo tuliyoweka msimamo wa kuigomea sensa.
Hiyo ndiyo sensa iliyofanikiwa inavyokwenda maana ukianzia mkuu wa nchi hadi wenyekiti wa serikali za mitaa (masheha kwa Zanzibar) na mabalozi wa nyumba kumi wanahamasisha watu na kueneza propaganda zao ikiwa ni pamoja na kutayarisha sms.
Juzi Jumatano ya tarehe 29/08 ilikusudiwa kufanywa maandamao ya kupinga sensa ila yalihairishwa kutokana na kuwa walihofia serikali kuja kupata sababu ya kusema 'maandamano ndiyo yaliyoivuruga sensa' kitu ambacho siyo kweli. Lakini maandamano yatafanyika.