Ukweli kuhusu nia ya Marekani Afghanistan.

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
17,036
22,714
Majeshi ya Marekani na NATO yalivamia Afghanistan zaidi ya miaka 16 iliyopita, October 2001.Baada ya vita majeshi hayo yaliikalia kijeshi Afghanistan.Sababu zilizototewa za vita hiyo na kukaliwa kijeshi kwa Afghanistan ni kwamba Afghanistan ni mfadhili wa ugaidi, ambao ulihusika na kushambuliwa kwa Marekani September 11,2001.

Vita ya Afghanistan inaendelea huku Marekani ikichukulia vita hii kama vita ya kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi ya September 11.Hata hivyo majeshi ya Marekani yapo Afghanistan mpaka leo.

Sababu ya msingi iliyotolewa na Marekani na NATO kuivamia Afghanistan na kuikalia chini ya "dhana ya usalama wa pamoja "ni kwamba mashambulizi ya September 11 yalikuwa ni mashambulizi ya kijeshi kutoka nje ya Marekani na taifa ambalo hata hivyo halikutajwa wazi wazi wakati huo, lakini ikiwa na maana ya Afghanistan. Jambo la kushangaza ni kwamba hapakuwa na ndege za Afghanistan kwenye anga la New York asubuhi ya September 11.

Makala hii inajaribu kueleza kwa nini hasa majeshi ya Marekani na NATO yalivamia Afghanistan baada ya kinachoitwa mashambulizi ya September 11.

Chini ya mkataba wa usalama kati ya Marekani na Afghanistan ulioundwa na Obama kwa kufuatia msingi wa mkataba wa usalama kati ya Marekani na Asia,Washington na marafiki zake wa NATO wametengeneza mfumo wa kudumu kijeshi Afghanistan, huku kukiwa na vituo vyenye vifaa vya kijeshi karibu kabisa na mpaka wa magharibi mwa China.

Mkataba huo ulikusudiwa kuiruhusu Marekani kuwa na vituo tisa vya kijeshi vilivyo karibu kabisa na mipaka ya China,Pakistan,Iran,Turkimenistan,Uzbekistan na Tajikistan.

Katika matukio ya hivi karibuni,Rais Donald Trump February 28,2017 alipokuwa akihutubia mkutano wa baraza la Congress, aliapa kuviteketeza vikundi vya kigaidi Syria,Iraq na Afghanistan akitumia mandate ya kugushi ya ugaidi.Kufuatana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani,wapo wanajeshi wa Marekani wengi zaidi Afghanistan kuliko sehemu nyingine yeyote yenye mapambano ya kivita. Wanajeshi hao wanaruhusiwa kushambulia vikundi vya Taliban,Al Qaeda na IS.Hata hivyo vikundi hivi vinasaidiwa kijeshi na Marekani!

Ipo agenda ya kisiasa ya kikanda na kiuchumi Afghanistan, ambayo inahitaji uwepo wa majeshi ya Marekani. Pamoja na uwepo wa hazina kubwa ya madini na gas Afghanistan,nchi hii pia inazalisha zaidi ya asili mia tisini (90%) duniani ya Opium ambayo inatumika kuzalisha heroin grade 4.Vituo vya majeshi Afghanistan pia vinatumika kulinda biashara ya madawa ya kulevya (Narcotics Trade), ambayo kwa sasa ndiyo inayochukuwa nafasi kubwa zaidi kwenye biashara ya nje ya Afghanistan.

Biashara ya heroin ambayo ilianza mwanzo wa vita ya Urusi na Afghanistan mwaka 1979,inalindwa na CIA, na inazalisha kwenye masoko ya nchi za magharibi kiasi cha dola za Marekani billioni 200 kwa mwaka.

"Idadi kubwa kabisa ya wanajeshi wa Marekani na NATO Afghanistan inakwenda sambamba na ulimwaji mkubwa kabisa wa Opium poppy. Hali hii inatia wasi wasi kuhusu nia halisi ya kupambana na ugaidi. "Anasema Victor Ivanov,Mkuu wa Kitengo cha Urusi cha kupambana na madawa ya kulevya.January,2010.
 
Wamerekani wanapovamia nchi Kwa ajili ya matakwa yao, hutafuta sababu kwanza, hupanga mbinu na wazawa ili iwe rahisi kufanikisha mpango wao, tena hakubali kutoka Kama alichotaka hakupata hata kama ataua raia wote ili mradi apate anachotaka wakati huohuo akitengeneza FAKE NEWS ulimwenguni kote aonekane Hana makosa na akubalike.
 
Disasters don't just happen, there is a series of critical events that triggers them to a certain situation
 
Back
Top Bottom