Ukweli kuhusu ndege za Serikali



mmebanwa kila pahala wacheni wivu wa pwani
 

Duniani kote hata mashirika makubwa hawanunui Ndege kwa cash bali hukopa kwa kulipa kidogo kidogo, huo ununuzi wa cash kuna ufisadi ndani yake ndiyo maana wapinzani wanapiga kelele.
 
wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Sina jina la kukupa ila ndege hazikununuliwa kwa ajili ya kutoa huduma, zipo kibiashara zaidi ndiyo sababu hazikupelekwa Government Flight Agency ambako ni kwa huduma.
 
Watu hawapingi ufufuaji wa ATCL bali modus operandi. Yaani kwenye Ilani ya CCM na CDM wote walisema watafufua lakini siyo kwa namna anayofanya Meko. Yeye Meko anakaa na mpwa wake Dotto James Katibu Mkuu Hazina wanaamua kununua ndege na kulipa. Hawana business plan, hawana procurement plan wala hawatangazi zabuni.

Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2015 na Kanuni zake na Sheria ya Fedha zimevunjwa zote kwa 100% na CAG haruhusiwi kukagua shughuli za ATCL kwa vile zimehamushiwa kasma #20 ya Ikulu kutoka kasma ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Hapo kinachoendelea ni ufisadi na rushwa tu kwenye manunuzi. Tusubiri awamu ya 6, tutakuja kufufua uzi huu na sintoshangaa kumuona Dotto James akipelekwa Segerea.
 

Yaani Rais wa Nchi ndiyo ana Akili kuliko watanzania wote? au maamuzi yake hutoka mbinguni kwa mungu yeye ni malaika? Acha kusingizia mabeberu, Mbona mkienda kuomba omba misaada kwa wazungu mnawaita wafadhili lakini wakiyakosoa matumizi mabaya ya pesa zao hata za walipa kodi zenye 10% zenu mnakimbilia kuwaita mabeberu, acheni kuishi kwa Fikra za zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM pekee, usijona una Akili kuliko wengine Tambua kuwa Akili ni nywele na kila mmoja ana zake.
 
Kwenye suala wa ndege mimi namuunga mkono Magufuli. Ni kweli gharama zake ni kubwa na biashara ya ndege ni ngumu. Kitu kinachonifanya mimi nimuunge mkono ni kuwa hizi fedha kipindi cha awamu iliyopita zilitumika kwenye mambo ya kijinga kama safari za viongozi nchi za nje, kulipa wafanyakazi hewa, ufisadi kwenye idara mabali mbali za serikali, vikao vya gharama vya wafanyakazi wa serikali kwenye hotel kubwa nk. Sasa kama zilikuwa zinaishia mifukoni mwa watu si bora hata huyu aliyenunua ndege?
 
Kwenye suala hili Dotto anaingiaje?
Tujikite kwenye maada maana ndugu zangu nyingi mkitoa hoja na kujibiwa kwa hoja badala ya kuendelea na mjadala mna tabia ya ku-diverge issue yenyewe na hivyo kupoteza maana.
 

Segerea 2026 watakwenda wengi jela juu ya hizo Ndege tu kwani hata ukarabati wake umejaa ufisadi wa kutisha sana, mda utaongea waache wajimwambafy sasa huko mbeleni mwenye kinga ni mmoja pekee.
 

Mkuu kwenye vikao mbali mbali vya ccm ndivyo wanavyoaminishwa!
Na pengine kuna asilimia kadhaa za ukweli...
Ujue hizi ndege tangu zimenunuliwa zinazurura tu humu nchini!
Ila kwa jinsi nijuavyo hizo 30 bilions ni makusanyo ghafi wala si faida!
 
Kuna kitu watu hamjui ni kua magu anapiga cha juu kwenye madili karibia yote ya serikali siku hizi, ni ukweli mchungu ambao hamtaki kuusikia maana mnamuona ndugu yenu kama malaika kua hawezi fanya kitu kama hicho.

Hakukua na haja ya kununua ndege hizi kwa cash, tena kwa fujo ndege 11. Kafunga mashirika ya ndege mengine kama fastjet siku hizi kila mtu anapanda ATCL, ila cha kushangaza pamoja na yote hayo kuingiza 30Bil peke yake miaka yote hiyo inamaanisha hadi hiyo hela ije kurudi ni miaka zaidi ya 70. Hapo ni vizazi vingi vimepita.

Sasa tuacheni kugombana na kutukanana tujaribu kufikiria, kitu ambacho return yake ni 70 years (assuming tutaendelea hivi) hiyo hela si bora ingewekwa kwenye elimu na vitu vingine vya muhimu kama healthcare? Au kama tuna shida sana na ndege basi tungenunua angalau haat 5 mwisho, kuagiza ndege 11 kwa cash huku nchi yenyewe maskini na sehemu nyingine zote hazijadevelop ni kitu cha ajabu. Huo utalii mnaosema tunakuza tusijidanganye hata watanzania tu wataruka na Emirates, Qatar au mashirika mengine ambayo yana competitive prices, hakuna mtu atapanda ATCL bei za kijinga kwa sababu tu ya uzalendo, the market always win.

Ukweli hizo hela kwenye ndege zimetupwa tu, hizo ndege subiri ziange kupata matatizo tuinvest hela nyingine tena kuzifix. Wakati mashirika mengine duniani yanapunguza ndege sisi ndo tunaongeza tena kwa cash. Lol
 
Tofautisha manifest na manifesto. Anyways, mi sijasoma hizo nyaraka, lakini walisemaje kuhusu CAG na ukaguzi wa manunuzi ya ndege na uendeshaji wa shirika la ATCL?
 
Alijibiwa aisee
 
Watalii hawawezi wakaacha kupanda ndege za makampuni makubwa yenye muda mrefu kwenye biashara pamoja na usalama wa uhakika waje wapande ndege za Magufuli.
Hapa ndipo mnapodhihira kuwa wapinzani hamna akili sawa sawa... Mkuu umeshawahi kwenda AirPort ukaona lile Dreamliner linavyoshusha watu? Kwani lazima kila kitu mpinge?
 

Kikwete licha ya hayo mapungufu yake kila mwaka aliwaongezea nyongeza ya mishahara watumishi wa umma, na Deni la Taifa halikuwa kubwa kama sasa ambapo wanajinadi kudhibiti wizi safari za nje lakini Deni la Taifa limepaa kuwa maradufu huku watumishi wa umma wakibuni Mbinu za kisayansi kufanya ufisadi pasipo kugundulika kirahisi kwa haraka, Ndege wanunue kwa mikopo lakini vitu vinginevyo vya maendeleo vifanyike kwa kasi ikiwemo kujenga miundominu bora zaidi isiyo haribiwa na mvua kirahisi
 
Eti muda si mrefu mtatamani kuziuza na hakuna wa kuzinunua'
Huu ni uchawi sasa, wewe unasema hivyo kama nani na unajua nini kuhusu biashara ya ndege mzee!?
Ndio kwanza vitendea kaz vnaendelea kuletwa na kuboreshwa wewe tayari ushaanza kuleta nuksi. Kuna biashara gani ya haraka ivo
 
Hapa ndipo mnapodhihira kuwa wapinzani hamna akili sawa sawa... Mkuu umeshawahi kwenda AirPort ukaona lile Dreamliner linavyoshusha watu? Kwani lazima kila kitu mpinge?

Kukosoa ndiyo kazi ya upinzani huwezi kuwapangia vya kukosoa lazima wakosoe kuanzia dogo mpaka kubwa
 
Kwenye suala hili Dotto anaingiaje?
Tujikite kwenye maada maana ndugu zangu nyingi mkitoa hoja na kujibiwa kwa hoja badala ya kuendelea na mjadala mna tabia ya ku-diverge issue yenyewe na hivyo kupoteza maana.

Doto ni mmowapo wa waidhinishaji wa malipo ya cash , utakuja kujua huko mbele pindi CAG akituhusiwa kuingia humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…