Ukweli kuhusu mhimili wa dunia

pauli jm

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
391
278
Wakuu mko poa?

Ninaombeni kujuzwa kuhusu 'Mhimili wa dunia', unapatikana wapi katika dunia yaani bara lipi, nchi ipi na sehemu gani? Maana kama kweli upo kama tunavyousoma ni lazima ungeonekana katika hali ya kawaida.

Maana tunauona katika michoro ya ramani ya dunia ukiwa katikati ya umbo la tufe, yaani katikati ya dunia ukiwa umepitiliza pande mbili juu na chini.

Katika mazingira kama haya ni lazima ungeonekana kwa vyovyote vile walau vichwa viwili vya huo mhimili kama unaonekana uko wapi katika hii dunia nikautembeleee??

Nyongeza, mfano wa picha ya mhimili wa dunia, unaonekana kikiwa ni kitu kilicho katikati ya dunia. Na ndicho huwezesha dunia kuzunguka. Swali langu nikwamba huu mhimili kama kweli upo na kama ni kweli dunia ni mviringo, na zaidi tunaweza kutembea popote juu ya dunia, ni kwanini tusiuone huo mhimili???

Na kama unaonekana, upo wapi katika mataifa ya dunia?
 
Attachments

  • 220px-Earth's_Axis_(small)-1.gif
    220px-Earth's_Axis_(small)-1.gif
    227.4 KB · Views: 114
Hata sielewi hili swali lako sijui unamaanisha north pole na south pole labda ufafanue kidogo. Kwani mkuu ulishawahi kuiona mistari ya latitude na longitude au X,Y,Z naomba ufafanuzi wako ili nipate kukujibu.
 
achana na hiyo misitari ya kubuni.

anataka kufahamu earth axis ipo ktk nchi gani au wapi

yani ukifika sehemu hiyo na kupalanyaga utoke unasema nimekanyaga kwenye mhimili wa dunia kama sijamielewa vibaya
 
Hakuna hiyo midude ilokaa kama mnara katika dunia ambayo wewe umeipa jina la muhimili muhimili wa dunia kwa kiingereza Axis ni sawa na kusema kuiitoboa dunia kuanzia north pole mpaka south pole yaani juu na Chini huku north Pole na south pole kama utaingalia ramani ya dunia kipitia tufe zipo chini na juu.

Sasa dunia kupitia principle ambazo zimewekwa hujizungusha katika axis yake (muhimili) na dunia hujizungusha kutoka magharibi kuelekea mashariki na hii kusababisha jua kuchomoza mashariki kuzama magharibi

NB: Muhimili ni kipenyo kutoka north pole kueleke south pole na sio kitu kingine.
 
Jibu ni hakuna mhimili unaoonekana kwa macho. Muhimili wa dunia ni wa kufikirika.

Ila imekuwa assumed kuwa dunia inajizungusha katika muhimili wake. Na kumaliza huo mzunguko wake kwa masaa 24 kitu ambacho kinapelekuwa kupatikana usiku na mchana.
 
Hakuna hiyo midude ilokaa kama mnara katika dunia ambayo wewe umeipa jina la muhimili muhimili wa dunia kwa kiingereza axis ni sawa na kusema kuiitoboa dunia kuanzia north pole mpajka south pole yaani juu na Chini huku north Pole na south pole kama utaingalia ramani ya dunia kipitia tufe zipo chini na juu
Sasa dunia kupitia prinsple ambazo zimewekwa hujizungusha katika axis yake (muhimili) na dunia hujizungu kutoka magharibi kuelekea mashariki na hii kusababisha jua kuchomoza mashariki kuzama magharibi
Nb muhimili ni kipenyo kutoka north pole kueleke south pole
Na sio kitu kingine
Asante nime kuelewa.
 
Hata sielewi hili swali lako sijui unamaanisha north pole na south pole labda ufafanue kidogo. Kwani mkuu ulishawahi kuiona mistari ya latitude na longitude au X,Y,Z naomba ufafanuzi wako ili nipate kukujibu.
Soma post ya Mr Q, ame nielewa.
 
Jibu ni hakuna mhimili unaoonekana kwa macho. Muhimili wa dunia ni wa kufikirika. Ila imekuwa assumed kuwa dunia inajizungusha katika muhimili wake. Na kumaliza huo mzunguko wake kwa masaa 24 kitu ambacho kinapelekuwa kupatikana usiku na mchana.
Upo sahihi kabisa, muhimili ni IMAGINARY, siyo kitu hai ni cha kubuni. Nadhani mtoa mada kwa swali lako hilo kama muhimili ungekuwa unaonekana kwa macho, ungeleta pia maswali haya:
~Umetengenezwa kwa material gani? chuma, plastic, au mbao?
~Je, kama ni mhimiili wa chuma, vipi miaka yote hii usipatwe kutu na kuvunjika, hatimaye dunia ikaanguka?
Maswali hayo na mengine mengi yangepata majibu kama tu, mhimili ungekuwa unaonekana.
 
Sahihi kabisa mkuu ndicho kitu nilicho kuwa nikijiuliza paka muda mwingine nilikuwa nikiona tuna danganya tu nawala hakuna hivi vitu ila wewe ume nifumbua macho nime pata mwanzo ngoja nika some saidi nita rejea.
 
Masomo ya jiografia na sayansi kwani siku hizi hayafundishwi shule za Msingi kuanzia darasa la tatu mpaka la saba?

Kama yanafundishwa basi kuna shida sehemu Wallahi!!!!
 
Masomo ya jiografia na sayansi kwani siku hizi hayafundishwi shule za Msingi kuanzia darasa la tatu mpaka la saba?

Kama yanafundishwa basi kuna shida sehemu Wallahi!!!!

Waalimu walikaririshwa ili wafaulu mtihani na hao pia wanawakaririsha wanafunzi wao ili wafaulu mitihani tu na mabadiliko ya elimu bora yanayopongezwa ni quantity na si quality hivyo, tuna safari ndefu

Mhimili wa dunia ni mstari wa kufikirika kama ilivyo equator, longitudes na latitudes..hii yote hugawanywa kutokana na kazi zake kwa wanajiografia.

Mhimili huchukuliwa katika kueleza mfumo mzima wa masaa 24 tuutumiao kama muda ambao dunia hutumia kukamilisha mzunguko mmoja.... Mzunguko huu ndio uleta vipindi vya siku kama asubuhi, mchana na usiku ( kwa kuwa dunia hujizungusha kutoka usawa wa jua ndio maana mawio na machweo ya nchi nyingi duniani huwa tofauti )

Nadhani nimetoa msaada japo kwa uchache ila ukitaka kujua zaidi..zama vitabuni
 
Soma Yeremia 31:37 ndio utajua kua hakuna mwanadamu anayeweza kujua misingi ya dunia au hata hiyo mihimili
 
Soma Yeremia 31:37 ndio utajua kua hakuna mwanadamu anayeweza kujua misingi ya dunia au hata hiyo mihimili

YETEMIA 31:37" Inasema hivi;

Bwana asema hivi, kama mbingu zikiweza kupimwa na misingi ya dunia kugunduliwa , huko chini ndipo wazao, wa Israeli pia nitawatupia mbali, kwaajili ya hayo yote waliyo yatenda asema bwana.##

Kwahiyo wewe una amini misingi ya dunia haiwezi kugunduliwa kabisa ???.
 
msaada plz..

jumla ya namba mbil znazofatana ni 23,na tofaut kat ya namba kubwa na ndgo ni 1..tafuta namba ndgo

soln iwe waz
 
YETEMIA 31:37" Inasema hivi;

Bwana asema hivi, kama mbingu zikiweza kupimwa na misingi ya dunia kugunduliwa , huko chini ndipo wazao, wa Israeli pia nitawatupia mbali, kwaajili ya hayo yote waliyo yatenda asema bwana.##

Kwahiyo wewe una amini misingi ya dunia haiwezi kugunduliwa kabisa ???.
NDIO MKUU, HAKUNA AWEZAYE NA NI KAMA VILE HAIWEZEKANI KUZIPIMA MBINGU
 
Back
Top Bottom