Ukweli kuhusu MAZIMWI

Ukweli kuhusu MAZIMWI

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,775
Reaction score
9,202
Mheshimiwa mmoja baada ya kupata cheo si
akapewa nyumba mitaa ya watu wenye pesa,
akahamia huko akiwa na mke na mwanae. Siku
moja mwanae aliyekuwa kazoea maisha ya
Uswazi akawa anawinda ndege na manati
kwenye uwanja wa jumba lao, bahati mbaya
jiwe likapitiliza na kwenda kuvunja kioo cha
nyumba ya jirani. Mheshimiwa na mkewe
wakaamua kumfuata mwenye nyumba
wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango
akafukua mbaba mmoja akawakaribisha kwa
heshima, wakaingia na kuanza kujieleza.
‘Samahani sie tumehamia karibuni hapo
nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako
kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha
na kuona kama tunaweza kutengeneza'.
Mwenyeji wao akawaomba wakae kisha
akawaambia, ‘Naomba niwahadithie kitu.

Kwanza mimi nawashukuru nyinyi na mtoto
wenu. Mwenye nyumba hii ni mchawi mkubwa
sana, mimi ni ZIMWI alikuwa amenifungiwa kwa
zaidi ya miaka 200 kwenye kichupa ambacho
kilikuwa kwenye dirisha lililovunjwa na chupa
nayo ikavunjika nami nimekuwa huru, kwa hiyo
kwa shukurani ombeni chochote mtakacho
nitawapa, nina uwezo huo' Hapo hapo
muheshimiwa akauliza tena,'Yaani kitu
chochote?' Akajibiwa ‘Ndio'. Basi pale pale
akasema, ' Mimi naomba niwe bilionea mpaka
nife' Akajibiwa ,' Hilo jambo dogo sana kwangu,
umepata na kesho utaamka tajiri' Mama nae
akaomba vyake, ‘Mi nataka niwe na nyumba
kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na
China na HongKong' Akajibiwa, ‘Umepata
mama, kuanzia kesho hayo ni yako. Mimi
nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina
kaombi kadogo'.
Mheshimiwa haraka akajibu,
'Sema tu wewe ni kama ndugu yetu sasa' Basi
ZIMWI likasema, ‘Naomba mkeo abaki hapa
kama masaa mawili tu, unajua kifungo
nilichofungwa kilinizuia kila kitu, hata mke
sijapata kipindi chote hicho. Nikimaliza tu hilo
ntaondoka kurudi kwetu Uzimwini hamtaniona
tena, itakuwa siri yetu'. Mme na mke
wakajadiliana wakaona utajiri waliopata ni
mkubwa sana, na hilo jambo ni dogo sana la
mara moja tu tena kwa siri, wakakubali sharti.
Mke akabaki pale kwa masaa kadhaa. Shughuli
ilipokwisha, mama wa watu akiwa
anajitayarisha kurudi kwa mumewe kichwani
akiwaza utajiri, ZIMWI likakohoa kidogo na
kumuuliza yule mama, ‘Samahani una miaka
mingapi na mumeo ana miaka mingapi?" Mama
wa watu akajibu, ‘Mie nina miaka 40 mume
wangu ana miaka 46' Yule Mbaba akacheka
sanaa, ‘Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka
leo mnaamini stori za MAZIMWI?
 
Tamaa ya Mali huondoa maarifa
MCHUNGAJI alikuwa anaombea waumini
akauliza; "Wangapi wanataka kuokoka inueni
mikono niwaombee." hakuna aliyeinua mkono.
Tajiri mmoja akapita mbele na kutangaza..
"Jamani mchungaji anasema wanaotaka
kuokoka wanyanyue mikono juu. " Mtoto mmoja
akanyanyua mkono, tajiri akatoa laki tatu
akampa yule mtoto. Tajiri: "Haya jamani
ninaomba nirudie tena niwaombe wanaotaka
kuokoka wanyooshe mikono juu ili Mchungaji
atuombee." watu wote wakanyanyua mikono
juu, tajiri akamgeukia Mchungaji ili awaombee
akakuta na mchungaji nae kanyosha mkono juu.
Pesa Pesa Pesa........hata Yuda zilimkengeusha
akamnadi Jesus!!Ijumaa Njema wapendwa
 
Madame B njoo huku kuna mitaji ya bure kwa wanaoataka biashara kubwakubwa
 
Last edited by a moderator:
Hii Leo nimeona kwa Kitime ..Nimecheka sana 😀 ..Asee pesa ni kitu ingine 😉
 
Back
Top Bottom