Ukweli kuhusu maisha ya mbele ya binadamu

Suala la muda na hiyo miaka, mwanadamu ndiye aliyeigundua na kuanza kutumika na calendar zinatofautiana kulingana na utaratibu uliowekwa katika sehemu husika. Hivyo hoja ya maisha yetu kuandikwa tayari INAWEZA KUWA ni sawa ila usiweke hoja yako kwa kutumia MUDA ambacho ni kitu fikirishi, kiufupi muda haupo ni kitu tu tumejiwekea ila huwezi kuuona muda ila unaona mabadiliko fulani tu ambayo hayana uhusiano na suala la muda na MUDA ni DHANA TU iliyopo.

Mwanadamu ni nafsi inayoishi katika mwili, na suala na hatima ya kila mmoja kuwa tayari ipo hili suala linaweza kuwa kweli ukifikiria kiurahisi ila ukianza kulitazama kiundani utakuja kugundua kuwa kesho yako INATOKANA NA LEO YAKO. Yaani unachokifanya leo ndiyo kesho na keshokutwa kitaamua hatima ya maisha yako na hii ni kutokana na kile unachoamini na kukifanya.

Maisha ambayo unaishi leo WEWE mwenyewe ndiye uliyekuwa CHANZO cha wewe kuishi maisha hayo kutegemeana na MAAMUZI uliyochukua hapo nyuma.

Tuzungumzie ishu ya KARMA. Unachofanya leo kitakurudia, maamuzi unayoamua leo ndiyo hayo kesho matokeo yatakurudia, yaani maamuzi yako leo ndiyo maisha yako kesho bila kujali ukubwa au udogo wa maamuzi hayo, na matokeo hayo yanaweza kuja katika namna ambayo hukutegemea ila ndiyo hivyo ulishayafanyia maamuzi JANA.

Hili suala la kuamini kuwa maisha yako tayari yameshaandikwa BINAFSI NALIKATAA maana hicho kinachokutokea leo tayari ulishatengeneza mazingira Jana either kwa kujua au kutokujua.

Nani anayeandika maisha yako yote wewe utakuwa mwizi?? Mungu ndiye anyeandika?? Ni nani anayeandika maisha yako wewe utakufa masikini?? Ni Mungu ndiye anayekuandikia?? Nani anayeandika maisha yako yote utaishi kuwa mchawi?

Majibu ya NDIYO katika maswali hayo yataibua maswali mengine kuhusu huyo Mungu anayeandika hizo hatima.

Ulimwengu una principle zake na hili lazima litazamwe kiujumla kwa kuangalia namna tu maisha yanavyoenda na mabadiliko ya ghafla ambayo yanatokea kuanzia hali ya hewa na mengine pia. Sisi wanadamu tumekuwa WACHUNGUZI TU wa jinsi ambavyo ulimwengu ulivyo na siyo kwamba tunayo majibu ya uhakika ya jinsi ulimwengu ulivyo na jinsi unavyofanya kazi, tuna NADHARIA nyingi sana na kati ya hizo ni chache zenye kuweza kuonyesha ukweli wa kitu husika.

Ulimwengu tunaoishi unaendeswa kwa nishati (energy), yaani viumbe vyote na kila kitu kinafanya kazi kulingana na energy inayo exist katika viumbe au vitu hivyo.

Mabadiliko yote yanayotokea ni kwasababu ya mabadiliko ya nishati hizo (Nieleweke hapa).

Wewe maisha yako yapo hivyo kwasababu ya mabadiliko (adjustments) ya NISHATI yako. Nguvu inayoendesha maisha yako ndiyo yenye kuleta matokeo, kile unachogusa au kufanya, main source ya TENDO husika ambayo mwili unaufanya ni kutokana na mabadiliko ya nishati tawala katika maisha yako WEWE MWENYEWE.

Nishati hii huwa inakuwa affected na IMANI (Sizungumzii dini tu hapa) fulani katika maisha yako ambapo kupitia imani hiyo ndipo matokeo huonekana.

Hivyo kinachotokea katika maisha yetu na jinsi tunavyoishi ni namna tunavyotumia energy zetu, na kumbuka hizo energy zinafuata sheria fulani za ulimwengu ili ziweze kuleta matokeo sawasawa na ufanyaji kazi.

Wewe kama unaamini ulizaliwa kuwa mwizi, yaani kitendo cha kuamini na kuishi hayo maisha ndiyo mwanzo wa energy yako kubadilika na kuanza kufanya jinsi ambavyo wewe umeiamuru na itakuletea matokeo sawasawa na jinsi ambavyo sheria za ulimwengu unavyotawala na siyo jinsi ambavyo wewe unataka. Nikimaanisha wewe utaiba na kupata unachokitaka ila ulimwengu utafanya kazi ya kukupa matokeo ya tendo lako kwa kufuata sheria za ulimwengu sawasawa na matumizi ya energy yako hapa ndipo KARMA inapoingia.

Maisha yako unayoishi leo ndiyo yanaamua kesho yako, ila suala la MAISHA yako ni script iliyo tayari na IMEKAMILIKA kuanzia kuzaliwa hadi kufa siyo kweli bali ni DHANA YA KIMAZOEA inayoishi na yenye kuleta MANTIKI fulani kwa kuona kwa macho na fikra za kawaida but DEEPDOWN ulimwengu unaendeshwa kwa nishati na sheria zake ambazo ndiyo hufanya yote yanayoonekana na yasiyo onekana.

Hivyo ewe ndugu yangu ukiona leo maisha magumu na ulimwengu kama unakutenga siyo kwamba uliandikiwa maisha yako kuwa hivyo, unaweza tumia nafasi kama hizo ku-adjust energy yako kufanya vitu vitakavyobadili maisha yako kesho.


Tarehe moja mweza wa kwanza huwa naamini ni siku ya kawaida kabisa na ni sawa na tarehe 31 December. Hizi ni DHANA tu ila maisha yapo na yanaendelea (NON- STOP).

Udhaifu wetu mpaka sasa ni uwezo wa kujua chanzo cha nguvu zinazotawala ulimwengu zilitoka wapi?? Hapo science na dini HAZINA MAJIBU zaidi utaambiwa Mungu alikuwako, yupo na ataendelea kuwepo milele Amina (alitoka wapi?) , yeye anaishi nje ya MUDA.

Sayansi nao watakuja na masuala ya kuelezea vitu ambavyo tayari vipo na vilikuwepo bila kutuambia vilitoka wapi??.

Mada kama hizi zinaweza badili mtazamo wako na kujiona kana kwamba hali ya maisha yako ya sasa yalishaandikwa hivyo na kuamini kuwa ndivyo yatakavyokuwa milele mwisho wa siku kujikatia tamaa na kujiona wewe ni wa kundi fulani. Aisee siyo kweli, amua kufanya kitu leo na mabadiliko utayaona ila ukikaa na kuamini "MIMI NI YATIMA SINA BABA WALA MAMA NDIYO MAANA MAISHA YANGU MAGUMU NA NDUGU WANANITENGA" yaani kila kitu katika maisha yako kitakuwa kigumu, ndiyo maana huwa nashangaa sana mtu kutumia maneno kama hayo kwa lengo la kutetea hali ya maisha yake.

(Codes zingine hizo za kutoboa maisha).
 
Time travel ni ngumu kueleweka kwa sasa kutokana na mfano uliotoa.
Nimewaza hapa kama ikafika 2025 alafu ukapigwa risasi kweli, je huyo aliekupiga risasi ni nani? Ametokea wapi? Ukisema ni identical twins bado maswali yataibuka.
 
Na bado wanadai hata ukienda future ukaona mtu flani atakuua, na ukajianda kabisa ukijua siku flani atakuja jamaa atataka kuniua but hautaweza badili future yaan you will die tu
 
Hoja yako uliyomaliza nayo inajaribu kugusa kitu kinaitwa grandfather paradox
But me kwa akili yangu nahis ukirudi nyuma ufanye hayo mauaji hayatatokea kwa sabb nikitu ambacho kilishapita means kwa lugha rahis tunaweza kusema past us just read only and not read and write by killing them nothing you can change
 
Ila me nahisi muda hatujaweka sisi nahis muda umeanza pale Mungu alipoanza kuumba (kwa wanaoamin) maana bibilia inasema HAPO MWANZO MUNGU ALIUMBA MBINGU NA NCHI hivyo nahisi alipoanza kuumba tyu ndo kuhesabu kukaanza maana before there were nothing
 
Dah swali zuri sana
 
Kwa means ipi unaweza rudi nyuma ya muda au kwenda future
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…