Smart mwananchi
Senior Member
- Jul 17, 2014
- 102
- 50
Hivi karibuni kumeibuka kikundi cha watu wachache wanaotumia mitandao na baadhi ya vyombo vya habari kupotosha ukweli kuhusu mabehewa ya TRL kwasababu zao binafsi zikiwemo za utafutaji madaraka.
Tatizo kubwa la baadhi wa hawa watu wana uelewa duni juu ya sheria ya manunuzi. Sheria hii hairuhusu waziri kuingilia mchakato wa manunuzi wa taasisi zilizo chini yake ili kujenga dhana ya uwajibikaji. Ikitokea taasisi zimeharibu wizara iweze kuchukua maamuzi bila kigugumizi.
Tujikumbushe kuwa mhe. Lowassa alipoteza wadhifa wake kwa kuingilia mchakato wa manunuzi wa TANESCO. Mwakyembe hajafanya kitu kama hicho TRL, ndio maana tetesi zilipoanza ni Mwakyembe aliyechukua maamuzi ya kuunda tume kufanya uchunguzi na kuagiza hatua zichukuliwe za kuivunja bodi ya zabuni ya TRL na kuwasimamisha kazi wafanyakazi sita waliohusika moja kwa moja kwenda nchini India kuchunguza ubora wa hayo mabehewa na kuundika ripoti iliyopasisha ubora wa hayo mabehewa na hivyo kupelekea kuruhusu mchakato wa malipo ufanywe na hazina na mabehewa yaanze kuja nchini.
Ni Mwakyembe aliyeombaTAKUKURU wachunguze huu mchakato na kuomba uchunguzi zaidi kutoka kwa wahandisi wa nje.Ametumia mifumo ya rasmi ya kiserikali kuchukua hatua stahili kwenye jambo hili.
Hata leo hii hatua alizochukua waziri Sitta ni kutokana na tume aliyounda Mwakyembe.Je, Mwakyembe engehusika asingeunda tume wala kuwasimamisha baadhi ya wahusika na wala asingewapeleka TAKUKURU kwa uchunguzi.
Tatizo lingine ni imani ya mhe. Sitta kuwa atafanikiwa kupata Urais kwa kurudia rudia maamuzi aliyofanya Mwakyembe na kuwasikiliza watu waliyoondolewa kwenye nafasi kwa ku underperform au ubadhirifu.
Leo hii anategemea wamweleze mwema ya Mwakyembe! Ni sawa na kusubiria boti ya kwenda Zanzibar kituo cha mabasi Ubungo.
Wizara ya uchukuzi ina taasisi nyingi sana ambazo zina changamoto nyingi pia ni wakati wa mhe. Sitta kuonesha ubunifu wake badala ya kurudiarudia kila alichofanya Mwakyembe ambaye alijenga matumaini na matokeo chanya kwenye baadhi ya taasisi hizo.
Nitumie nafasi hii kumpa pole Waziri wa Uchukuzi na mgombea urais kwa ajali za kila siku zilizouwa Watanzania 890 kwa miezi mitatu tu, hii ina maana kuwa ikiendelea hivi kwa miezi kumi tutapoteza nguvu kazi na wapiga kura wake 8900!
Mungu aepushe mbali na ampe moyo wa huruma na kumbukumbu mhe. Sitta kuwa hili nalo ni jukumu lake.