kitongakipikiqum
Member
- Apr 19, 2015
- 38
- 9
Tatizo hapa ni kutafuta sifa ambazo ustaili na ujazitole jasho, ni sawa na kuokota embe dodo chini ya mwarobaini alafu kwa papara anashindwa kula ndiyo mzee sitta.:juggle:
Mheshimiwa Mwakiembe,
Je kile kiwanja ulichonunua kule Bahari beach kwa bilioni moja kupitia Yono Auction Mart, hizo pesa umezitoa wapi kama sio dili kama hii ya kuleta mabehewa mabovu?
Uliunda hii kamati ya kuchunguza mabehewa na ukapewa ripoti yake. Wewe ukaifungia makabatini mpaka mzee Sitta amekuja na kuifanyia kazi. Kuunda hii tume ulilazimishwa na malalamiko mengi yaliyokuwepo hasa kutoka kwa chama cha wafanyakazi wa reli. Lakini ulikuwa unaujua ukweli wote na ndio maana uliifungia ripoti.
Unamlaumu mzee Sitta kwa kuchukua hatua, lakini unajua ukweli kwamba hata kuondolewa kwako wizara ya ujenzi ilikuwa kwasababu hizi hizi za mabehewa mabovu na dili za bandarini. Ikulu ilichunguza na kujua ukweli na ndio wakakuondoa na kumwagiza mzee Sitta achukue hatua. Ulitaka mzee Sitta aendelee kukulinda mpaka lini?
Bilioni 230 zimepotea wewe unasema sheria inakukataza kuingilia manunuzi. Ilikuwaje ukakubali pesa zote zilipwe asilimia 100 kitu ambacho ni kinyume cha sheria? Ilikuwaje hukusimamisha malipo kipindi hicho wakati kila siku wafanyakazi walikuwa wanakuambia hayo mabehewa ni mabovu?
Mwakiembe, tunajua umebanwa vibaya sana kule jimboni Kiela na uliamua kusaka pesa nyingi ili utoe rushwa kwa wapiga kura wako. Wapiga kura hawakutaki kwasababu umeshindwa kutimiza ahadi zako. Sasa unataka kuwahonga kwa kupiga dili kutumia cheo chako. Nenda Kiela kawaombe msamaha wapiga kura wako maana sasa hata umechafuka zaidi.
Pole sana Mwakiembe, vile visa ulivyomfanyia mzee Lowassa kwa kushirikiana na huyo rafiki yako Sitta, sasa vinakuandama. Pasco atasema karma imeanza kufanya kazi yake vizuri. Tulia sindano ikuingie vizuri.
Bilashaka tunadili na watu wasiojuwa kusoma kama huyo anaejita jenifa, anaonekana ni walewale wa mgao milioni 152 kwa siku ambao mh mwaki alikata mirija yake, na ndiyo maana anaandika vitu asivyo vielewa. Mzee sitta kati maelezo yake yote alisema kutokana na majibu ya ripoti aliyounda mtangulizi wangu yani mh mwakyembe inimekuja na majibu haya. Vilele kumbuka mkutano wake wa kwanza TRL waandishi wa habari walimuuliza mh sitta vipi kuhusu tume iliyo undwa na mh mwakyembe je utaivunja kabla ijamaliza kazi yake?????, sitta akasema hapana hata mimi naiunga mkona na majibu yake nitayafanyia kazi sito mwogopa mtu. Sasa ni majibu gani ambayo mh mwakyembe aliyafungia kabatini na kama siyo unafiki na uzandiki wa kuandia vitu uvyo vijua.
Jenifa umepotea ghafla. Tunasubiri ulete uongo mwingine.