Ukweli kuhusu limao na kupunguza "Cholesterol" (mafuta) mwilini

Ukweli kuhusu limao na kupunguza "Cholesterol" (mafuta) mwilini

MWANAKB

Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
51
Reaction score
18
Wakuu salaam,

Naomba kufahamu kitaalamu ni kweli limao lina uwezo wa kupunguza mafuta yanayoweza kupelekea unene usiotarajiwa mwilini!?

Naombeni kufahamu kama kweli limao lina uwezo wa kupunguza mafuta mwilini sababu nimekuwa nikiwaona watu wengi wakikamua juisi yake na kunywa huku wakiamini kwa kufanya hivyo kutawasaidia kupunguza mafuta yaliyozidi mwili na hii hufanywa na wale wenye miili na matumbo (kitambi) makubwa.

Naanza kunyemelewa na vinyama uzembe vya kitumbo ambavyo kwa kiasi kikubwa husababishwa na mafuta yaliyozidi mwili. Natumai kupata michango mizuri kwenu.

Karibuni,

Natanguliza shukrani zangu kwa maoni na uchambuzi wa kitaalamu.
 
Last edited by a moderator:
Yatakuletea acid nyingi mwilini, na kukunyonya damu ila hutapungua uzito.
 
Limau lina Tindikali
(Antioxidants na
Alkaline)
limao asubuhi hasa mda wa kuamka kwamba ni kirutubisho muhimu na husaidia kwa kiasi kikubwa kutoa sumu mwilini (detox) kwani limao lina kiwango kizuri cha Alkaline ambayo hupambana na sumu mbalimbali kwenye mwili hasa maeneo ya kwenye maini,figo,kibofu cha mkojo na mfumo wa damu na hata kuzuia kansa.

Sasa jambo ambalo ni muhimu kufahamu ni kuwa huruhusiwi kuweka sukari katika kinyaji chako kwani sukari ina trigger acidicity na hivokuwa kazi bure.
ad450f3eb1fc3cfda4027c36d41bd05e7004f7d1.jpeg


Wahenga wanasema nyota njema hung’ara asubuhi – mie kila asubuhi huwa ni muda muafaka wa kuanza siku yangu kwa kuzingatia afya. Kwa kawaida huwa napenda kuanza siku na chai au maji yaliyochanganywa na limao. Limao ni kitu kidogo sana lakini faida zake huwezi kuamini kama hujawahi kutumia. Leo hii naomba nikudokeze kidogo ili nawe upate kujua.

Kuna faida nyingi sana za kutumia limao, hasa wakati wa asubuhi wakati mwili umekaa bila kula usiku kucha. Kati ya nyingi, hizi hapa chache za kukufanya kufikiria kuanza kutumia limao kama utapenda.


Kusafisha mwili

Limao husaidia kusafisha uchafu usiohitajika mwilini kwa kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kulifanya ini kufanya kazi vizuri.

Kuweka harufu nzuri kinywani

Asidi iliyopo kwenye maji ya limao huua bakteria walioko mdomoni wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ni vizuri kama ukinywa limao baada ya kupiga mswaki ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kuleta nguvu mwilini

Limao baada ya kuingia kwenye mfumo wa chakula, huupa mwili nguvu. Hii husaidia kuondoa uchovu na msongo wa mawazo, sonono (depression), na wasiwasi.

Kupunguza uzito

Nyuzinyuzi za pectin (Pectin fiber) zilizomo kwenye limao husaidia kuzuia njaa na hivyo kutopata hamu ya kula mara kwa mara.

Kuongeza kinga ya mwili

Malimao yana acid, ni chanzo kizuri cha vitamin C, ambayo ni nzuri kuzuia baridi na homa. Malimao pia husaidia kuimarisha ubongo na mishipa ya fahamu kutokana na kuwa na madini ya Potassium. Vilevile Potassium husaidia kuzuia shinikizo la damu.

Kuzuia uvimbe

Cha kushangaza kabisa, ukiwa unakunywa maji ya limao mara kwa mara, unapunguza kiwango cha acid mwilini mwako. Hii ni kutokana na ukweli kuwa limao haitengenezi acid mwilini baada ya kumeng’enywa. Kutokana na hii, husaidia sana kupunguza asidi ya uric ambayo ni chanzo kikuu cha uvimbe mwilini.

Kuondoa mikunjo na makovu mwilini

Maji ya limao huweza kuondoka makovu na mikunjo kwenye ngozi. Huweza vilevile kupunguza makovu makubwa kama ukinyunyizia kila mara. Kutokana na uwezo wake wa kusafisha damu, maji ya limao huacha ngozi ikiwa inang’aa na yenye afya.

Husaidia kukufanya uache kunywa kahawa

Je wewe ni mlevi wa kahawa na unataka njia ya kuacha ? Basi kunywa kikombe cha maji ya moto chenye mchanganyiko wa limao. Hii ni dawa tosha. Huwezi kuamini hadi ujaribu, na ukishajaribu hutoweza kurudi tena kwenye kahawa.

Je unatakiwa kutumia limao kwa kiwango gani?

Kama una uzito mdogo, chini ya kilo 70, unaweza kula nusu limao, kama umezidi kilo 70 unatakiwa kula limao zima kwa siku. Ukifanya hivi kila siku utaanza kuona mabadiliko muda si mrefu.

Karibu kwenye ulimwengu wa afya. Jaribu kutumia limao na uone uzuri na faida zake kwenye mwili wako. Jua kuwa vitu vizuri mara zote huwa havina gharama, ni vilevile tunavyoviona kila siku, cha msingi ni jinsi ya kuvitumia. Ukifanya matumizi sahihi ya vitu, hakika utaona maisha yanavyokuwa mazuri.

Kwa Kupunguza Tumbo na Unene

changanya Limau moja na kjiko kimoja cha Asali safi ya nyuki na maji ya Uvuguvugu glasi 1 kila siku kwamuda wa miezi 6 utapunguwa uzito wako.
 
MWANAKB, Kunywa jusi ya limau na uchanganye an Asali kijiko ule kila siku asubuhi kabla ya kulaa kitu itakuondoshea mafuta mwilini yaliyozidi.
 
MziziMkavu,
Tayari umeisanijibu, nilitaka kuuliza kama ukichanganya na asli hayo maji kama kuna tatiz.
Ila lingine je, kwa mama Mja mzito limao lina tatizo akitumia? Tafadalli jibu Mzizimkavu
 
Tayari umeisanijibu, nilitaka kuuliza kama ukichanganya na asli hayo maji kama kuna tatiz.
Ila lingine je, kwa mama Mja mzito limao lina tatizo akitumia? Tafadalli jibu Mzizimkavu
Limau ukichanganya na Asali na Maji ya Uvugvugu ndio hapo umepatia inafaa zaidi kwa mtu mnene au mwenye kitambi litampunguzia kitamnbi chake. Kwa Mwanamke Mja Mzito au Mwanamke anaye nyonyesha Hafai kutumia limau mpaka Limau lipikwe kwenye chakula sio kunywa limau halijapikwa huenda mimba yake ikaharibika.

Special Precautions & Warnings:

Pregnancy and breast-feeding:
It is LIKELY UNSAFE to take lemongrass by mouth during pregnancy. Lemongrass seems to be able to start menstrual flow, so there is a concern that it might cause a miscarriage.

There is not enough reliable information about the safety of taking lemongrass if you are pregnant or breast-feeding. Stay on the safe side and avoid use.
 
Vipi kuhusu ndimu? vitu vilivyo ndani ya limao vina tofauti gani na ndimu??
 
Mdau yeyote anayeweza kunijulisha hospitali ya allerg kwa dar es salaam ninasumbuliwa na pua kuziba sana niliambiwa ni allerg sijajua ni hospitali gani inachombo cha kupima
 
Shukrani kwa wote mliotoa elimu yenu na mliochangia mada hii, naamini wengi wamenufaika na michango yenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom