Unaongelea jambo usilolijua, na wengi wanafanya kosa hili. Haiwezekani kabisa kutengenisha dini, Mungu, Shetani na mwanadamu.Dini ni njia ya kukupeleka kwa MUNGU Ila sio lazima uwe na dini ndo uwe Karibu na MUNGU.
Umejuaje mtoto akizaliwa anakuwa na imani? Any way tuachane na hayo najua hauna jibu tuendelee kujifarijii ziku zetu ziishe kwa amani tuwe udongo , kwisha[emoji114]Imani unazaliwa nayo ila dini unaikuta duniani ukimzaa mtoto anakuwa na Imani na mungu ila Hana dini hivo dini zote tunazikuta tu duniani ila Imani tunazaliwa nazo Nirahisi Mimi kuamini nitapata au kufanikiwa jambo fulan hata kama Sina dini
Hizi dini za kigeni uislam na ukristo na zingine zilizotoka ughaibuni, ni utumwa na utapeli mtupu. Zote zina agenda mbaya iliyojificha.Swali la MSINGI;
IN THE FIRST PLACE, KWANINI UNAAMINI KATIKA DINI UNAYOIAMINI?
Kabla hujaendelea kusoma be honest with yourself na ujijibu🙏
Ok tuendelee.
Kila mtu kwa mujibu wa imani yake amekua akijenga HOJA NZITO kueleza “UKWELI” na u HALALI wa Mungu wake huku akinukuu maandiko ya dini yake kwa ufundi mkubwa sana na kukosoa imani zingine.
UKWELI ni kwamba SIO KWELI kwamba dini unayo iamini ULIICHAGUA kwa hiyari yako baada ya kujiridhisha ni SAHIHI na ya KWELI
UKWELI ni kwamba 95% ya watu wote Duniani wanaamini dini wanazo ziamini ikiwa ni MATOKEO ya MALEZI/MAKUZI, GEOGRAPHY/HISTORY, nasio machaguo yao
MALEZI YA MZAZI.
Wazazi wanachangia pakubwa sana kupitia ile TRUST dhidi ya watoto...... kuna trust kubwa sana ya mtoto kwa mzazi. Mtoto toka mchanga anamuamini mzazi 100% na anaanza kuaminishwa na kujengewa hofu kuhusu Mungu husika hadi anapokua kijana.
Teenagers are suspicious, lakini hadi kufikia hapo inakua too late, brainwashed damage ya mzazi inakua beyond repair
MAKUZI YA JAMII
Namna jamii inavyoishi kwa kumkuza Mungu
Mitaani watu wataapa kwa jina la Mungu, kila kitu kikitokea watu watesema namshukuru Mungu au namuachia Mungu, jamii inatoa nafasi kubwa kwa viongozi wa dini kama kwenye misiba harusi nk
Majanga makubwa yakitokea viongozi wataingoza maombi ya kitaifa nk nk
Mtaani huko ukisema hadharani hakuna Mungu kila mtu atakuona unalaana au umechanganyikiwa, nchi nyingine una uwawa kabisa
GEOGRAPHY/HISTORY
Je wewe mkristo wa Iringa au muislam wa Tanga vipi kama ungezaliwa na wazazi wa kihindu India kwenye viunga vya Punjab ambapo 99% ni Budha?
Vipi ungezaliwa kule milimani China ambapo 100% ya wakaazi ni Budha?
Kwa mfano Tz watu zaidi ya 80% wanajua dini mbili tu ukristo na usilam, hawana kabisa access ya kujua dini zingine, hii ipo kwa nchi nyingi sana duniani kote. Nchi kama North korea hali ndio mbaya kabisa.
Huko China kuna majimbo ukiwauliza kuhusu Yesu au Mudi hawajui kabisa kama vile wewe ukiulizwa kuhusu dini kuu ya wachina na Mungu wao hujui chochote labda u google😂
JE, WEWE UPO KWENYE IMANI YAKO KWA SABABU GANI?
Kisha tafakari dhana nzima ya uwepo wa Mungu mmoja kama inawezekana kwa kuzingatia malezi makuzi jiografia na historia 🙏
Hapo uliposema Mudi umeyakanyaga kijana.Huko China kuna majimbo ukiwauliza kuhusu Yesu au Mudi hawajui kabisa
Mungu hayupo.Chakushangza kila mmoja anaamini dini yake ni ya kweli.
Waislam wanasema Allah anajibu maombi yao lkn nao wakristo wanasema Yesu anajibu maombi yao. Mungu wa kweli wapo wangapi?
Na kama ni mmoja, mbona watu wanaabudu Miungu tofauti lakini wanapata matokeo sawa? Anayeabudu Mungu wa uongo anapata matokeo sawa na anayeabudu Mungu wa kweli,hii imekaaje?
Au maombi ni dhana tu lkn hakuna kitu kama hicho?
Ukitaka kujua hilo mchukue mtoto huyo huyo aliyezaliwa Tanzania aende aishi china atakuwa na iman ya kichina Buddha ,akienda roma atakuwa na iman ya Kiroma hivo hivo akienda uarabun atakuwa na iman ya kiarabu hata mababu zetu hawakuzaliwa na dini ila walizaliwa na Imani ndio maana waliomba miti,misitu, mawe,vinyago na walifanikiwa Kwa kuwa wana imani hata hao wanao amini shetani wanaimani ndio maana wanafanikiwa na wanaomini mungu nao wanafanikiwa hivo amini tuna zaliwa na Imani ndio dini zetuUmejuaje mtoto akizaliwa anakuwa na imani? Any way tuachane na hayo najua hauna jibu tuendelee kujifarijii ziku zetu ziishe kwa amani tuwe udongo , kwisha[emoji114]
Upo sahihi kabisa mkuuUkweli nikwamba dini au imani ya dini fulani imekua kama milki ya familia na jamii husika.
Leo mtu akitaka kubadili dini anawaza familia itamchukuliaje. Bora kuacha mke kuliko kubadili dini. Maswali nimengi mnooooo.
Hapa ukitaka kufunga ndoa( kwa walio wengi) na mtu swali lakwanza ni dini kisha mengine yatafuata
Habari za dini ni nzito kidogo sio rahisi kama tunavyozijadili hapa
Utoto huo Mimi siwez jadili huo utotoMungu yupi?
Krishna?
Zeus?
Allah?
Thor?
Jehova?
The list is endless
Let’s assume Mungu wa kweli ZeusKuna asimilia fulani ya imani ya kweli katika kila dini -- hata zile ambazo zinaeneza uongo wa wazi.
Ukweli unaweza kuchanganywa na uongo ilimradi tu uvutie akilini mwa watu wanaopenda kudanganyika na kudanganywa.
Aidha, ukweli halisi wa Mungu haujifichi na wala hauna sababu ya kujificha.
Kanuni ya ukweli ni kudhihirika kama nuru ya adhuhuri, isiyohitaji wala umahiri kuing'amua.
Kanuni ya uongo ni kujificha kama giza la usiku wa manane, linalohitaji kutia maanani ili kupata utambuzi wa ziada ili kubaini kinachoendelea duniani.
Tatizo la wengi sana si kwamba hawaujui ukweli.
Shida ipo kwenye maslahi binafsi wanayohofu yatavurugika iwapo wakiufuata ukweli.
Maslahi (mali, kipato, fedha, familia, marafiki, mazingira, mfumo, mipango fulani fulani, nk)
Shida ipo kwenye utaratibu mpya wa maisha watakaolazimika kuufuata iwapo wakiukubali ukweli huo.
Shida ipo kwenye raha na starehe potofu watakazolazimika kuzivua kwa vile zinakinza ukweli mpya ambao hawana budi kuupokea.
Shida ipo akilini mwao kwamba jamii iliyowazoea wakiwa hivi itawaonaje ghafla tu wakiwa vile.
Shida ipo kwenye utashi wao ambao haujafanya maamuzi ya kina, wakidhani kwamba wana muda wa ziada kesho, ambayo kimsingi haitafika kamwe.