Ukweli kuhusu kukua kwa Deni la Taifa

yamindinda

JF-Expert Member
Jul 29, 2011
1,581
1,318
UCHAMBUZI WA HALI YA DENI LA TAIFA KIDUNIA
Anaandika Moses Machali!
Mbunge wa zamani Kasulu Mjini
Nimeona watu mbalimbali kama wakistuka baada ya kusikia kwamba deni ya Taifa limeongezeka kwa Asilimia 17 kutoka Dolla za Kimarekani Bilioni 22 za Juni 2016 hadi Dola Bilioni 26 Juni 2017. Watu wanaenda mbali na kusema kwamba serikali inatupoteza. Watu na hasa wanasiasa wenzangu wanatia hofu wananchi kwamba tutafika mahala pabaya na tusiweze kukopesheka, nk. Ukweli ni kwamba deni la taifa letu ukilinganisha na nchi nyingine bado linahimilika sana tu.
Ifuatayo ni orodha ya MADENI kwa nchi mbalimbali duniani kama wanavyoeleza CIA ktika WORLD FACT BOOK na IMF. Kwa nchi za AFRICA MASHARIKI ( EAC), hali ni kama ifuatavyo yaani kiwango cha asilimia ya deni taifa kwa kila nchi (COUNTRIES PUBLIC NET DEBT AS % OF GDP):
Tanzania 36.6%
Kenya 50.4 %
Uganda 35.4 %
Rwanda 36.6%
Burundi 43.4%
Hiyo ndiyo hali ya deni la taifa kwa nchi za AFRIKA YA MASHARIKI kwa mwaka 2016. Kenya na Burundi zinadaiwa zaidi ya Tanzania huku Rwanda ikilingana na Tanzania kiasilimia. Uganda ndiyo yenye tofauti ndogo sana ikilinganishwa na Tanzania ambapo Uganda ina deni la 35.4%.
HALI YA DENI LA TAIFA KATIKA NCHI NYINGINE DUNIANI
Uingereza 92.2%
USA Marekani 73.8%
United Arab Emirates 60.3%
Ureno 126.2%
Ugiriki 181.6%
Italia 132.5%
Eritrea 119.6%
Misri (Egypt) 92.6%
China 20.1%
Ubeligiji 106.7%
Autria 85.8%
Msumbiji 100.3%
Lebanon 132.5%
JAPAN 234.7%
Jamaica 130.1%
South Africa 43.3%
Nigeria 13.2%
Moroco 77.0%
Zambia 57.2%
Nk
HITIMISHO
Nchi kukopa siyo dhambi kama inavyoaminishwa na kupotoshwa na baadhi ya wanasiasa hapa kwetu ambao huwatia hofu wananchi kwamba nchi imeuzwa. Ukiangalia mifano ya viwango vya madeni ya nchi mbalimbali duniani hapo juu kiasilimia unaona kabisaa TANZANIA hatudaiwi asilimia kubwa sana unapolinganisha na nchi nyingine duniani ambazo zinadaiwa zaidi ya 100% hadi 234.7%. Sisi bado tuna 36.6% sawasawa na Rwanda hadi ilivyofika mwaka 2016. Tujiulize, maswali kadhaa: kama Marekani yenye Uchumi mkubwa wa zaidi ya DOLA TRILIONI 14 anakopa na kudaiwa deni la asilimia 73.8, je, sisi Tanzania ni nani hadi tuache kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu? Japan anadaiwa kwa asilimia 234.7, je, sisi watanzania ni akina nani? Nchi za Uingereza wanadaiwa kwa asilimia 92.2 ya pato lao la taifa. Sisi ni akina nani. Mtanzania mwenzangu shituka na jihadhari na upotoshwaji unaofanywa na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka kwa namna yoyote hata kwa kukupotosha ilimradi wakudanganye na kisha uwaunge mkono. Hata wao wakiingia madrakani lazima watakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini. Hakuna mtu au chama kinachoweza kuingia madrakani kisha kikaendesha nchi na serikali bila kukopa;haiwezekani. Jambo la msingi ni kwamba serikali inakopa kwa ajili ya nini? Hapa kwetu tunaona serikali inakopa kwa ajili ya kujenga Barabara, Reli, na Kwa ajili ya sekta za huduma kama afya, maji, Elimu, nk. Hakuna dhambi kukopa tusidanganayane.
09th November, 2017
 
tatizo sio kukopa,tatizo ni kwamba tulianza na tambo kuwa sisi ni wa kukopesha wengine na sio kukopa na kuombaomba
jingine ni kwamba hilo deni mnalifanyia nini,wenzetu wanakopa na hali za maisha kwa wananchi katika nchi zao zinaonekana kuwa nzuri

sisi tunakopa kununua wapinzani wetu wa kisiasa
tunakopa na kupeleka hela sehemu ambazo hazina manufaa kwa wananchi moja kwa moja(fly over dsm)!!!!!
 
Back
Top Bottom