Ukweli kuhusu"kukaza kwa vyuma"

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
82,971
Reaction score
89,191
Salam wadau wa jf
Kauli ya vyuma vyuma vimekaza ilivuma sana siku za hivi karibuni ikichagizwa na kauli pacha ya pambana na hali yako lakini observation yangu imeprove tofauti kabisa
Mwanzoni mwa mwaka huu nilifanya safari ya kutoka Mpanda kwenda Morogoro kupitia Mbeya kwa shughuli binafsi,huku kwa mara ya mwisho nilisafiri 2016,nilichokishuhudia njiani ni kukua kwa miji kwa ongezeko la nyumba,maeneo ya biashara na ongezeko la mahari
Watu wamejenga na wanazidi kujenga nyumban na majengo ya biashara,nimeshuhudia magorofa mapya kila mji kuanzia Tunduma,Vwawa,Mbeya,Makambako,Mafinga,Iringa hadi morogoro,miji imekua kweli kweli.Idadi ya magari hasa malori yameongezeka zaidi tofauti na swali
Hitimisho langu,usiseme tuna hali mgumu,jisemee nafasi yako.Sina nia ya kukana hii kauli lakini uhalisia ni tofauti,kauli ya vyuma kukaza haiakisi uhalisia na ilitiwa chumvi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…