Ukweli kuhusu kona tulokutana na bwana mkubwa 2014

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Mimi ni kijana ambaye nilikuwa nafanya kazi benki kama afisa mauzo , mwaka 2013-2014 ,Kipindi hicho kulikuwa na ujenzi wa mradi fulani mkubwa tu kuna mkandarasi kutoka China jina nimeliifadhi,Huyo mkandarasi akawa anakuja pale benk kuweka hela.

Sasa tukawa marafiki wa kweli nikawa namtembelea kule avic city, ikatokea siku moja akaniambia ana Biashara anataka tufanye ni ya kuuza majenereta kadhaa ambayo yalikuwa tiyari jijin Dar, nikakubali akanambia utakula ten percent, nikafurahi maana kwa haraka haraka ilikuwa ningepata million 90,

Siku ilofuata akanipeleka majenereta yalipo nikayaona yalikuwa mengi sana na mpaka ninashangaa maana yalikuwa magenerator 420, ten kva na 5.35 KVA.

Akili ikaja niombe ruhusa kazini one week nitafte mteja.Nikaanza kumsaka mteja nikazurula Kariakoo wapi sikufanikiwa nikazurula weee sikufanikiwa , nilichofanya ikabidi nitumie wauzaji wa jumla wakanambia kuwa haya sasa hivi umeme uko stable sana hayauziki, Prof. Muhongo kawabania.

Nikasema ok , nilikuwa na shughuli ya kuwafungulisha akaunti vijana wa CCM Kawe Ukwamani kuna mwenyekiti wao anaitwa Laiban Kallaghe. Nikamaliza kazi ilonipeleka nikampa dili la majenereta, akasema ok hayo anaweza kuyanunua bwana mkubwa apeleke jimboni kwake, ila kumpata vigumu, either umtumie wapambe wake kama Sophia au katibu wake ndo utampata.

Nikakubali wakasema watanikutanusha naye Saphire hotel Kariakoo, nikaenda Jumatatu sikumuona, nikaenda Jnne nikakutana na mpambe wake bwana mkubwa huyo akasema tutayanunua ila bei yenu ya million 5 kwa kila moja punguzen tuyachukue yote kwa 600,000,000/= badala ya 900,000,000/= nikasema ngoja niwasiliane na boss Wangu, nikampigia yule mchina akasema ok sell.

Nikawa Mwenye furaha kuwa naenda kupata million 60 kama ten percent,
Kesho yake niko ofisini nikaona nafuatwa na messenger, akanambia unaitwa na meneger , kufika pale ofisini nikaona kuna mwanaume mmoja kavaa miwani mweusi Yuko na meneja

Swali alilouliza yule mwanaume ni " kijana Mwenyewe ndo huyu?" Manager akajibu ndiyo.

Akasema twende , nikawa na furaha sana nikajua bwana mkubwa kanunua naenda kupata changu hapa haraka haraka nikaanza mahesabu ya kiwanja Kigamboni , tukaingia kwenye gari yule jamaa hanisemeshi chochote , tukaelekea njia ya serander bridge , tulivyofika Palm beach akapigiwa simu akapokea akajibu NDIYO KIJANA NINAYE NIMEBAHATIKA KUMPATA,

Nikaanza kujiuliza tunaenda wapi,Nikatulia tulivyofika ubalozi wa Ufaransa tukapinda njia ya Oysterbay , tukaenda mpaka hotel moja maarufu uko jina nimelihifadhi.

Tulivyofika hotelini duh badala ya kukuta kitita nikakuta tuhuma,
Kuangalia naona polisi wako hapo nikamuona mzee wa mabarabara naye yupo meza kuu.

Nilikuwa nimeandaliwa ka daftari kuorodhesha maelezo yangu kupelekwa polisi, yule muheshimiwa alinihoji Mwenyewe ambaye alikuwa anasimamia mabarabara mwanzo mwisho , akaniuliza mambo mengi mengine nayaweka akiba , nikawaza kuwa kweli huyu atazuia dili lililoingiliwa na Laigwan?

Nikajipa moyo Laigwan MTU mkubwa sana ,Baada ya maelezo marefu kuhusu generators akaniachia na akanipa nauli elfu kumi akasema nenda ila bado nina kazi na wewe nikikujitaji onesha ushirikiano, polisi nao wakaondoka,,nikaogopa sana tena sana, nikaenda sikurudi hata ofisini, asubuhi meneja akanihoji nikamwambia.

Upande wa wanunuzi nikakutana nao wakasema huyo akishaingilia hapindishi hivyo haiwezekani tena , kichwani nikawaza aigwan ina maana tunakuogopa tu nje kumbe nawe kuna watu unawaogopa dah!!

Kila Jumatano nikawa napigiwa simu na Polisi naenda kutoa maelezo central kuhusu zile generator, cha kushangaza maswali ni yale yale kila siku generator zimeingiaje, vibali, kwanini nijihusishe, duh, nikaja kusikia yule mchina kashafukuzwa na generator kazitelekeza kumbe alizileta kwa mgongo wa serikali akataka auze kimya kimya.

Mi nikaendelea kuhojiwa kila na Jumatano, nakumbuka ilikuwa Jumatano moja mheshimiwa walikuwa na kikao Mliman City akaniita akasema nimejiridhisha hauna makosa makubwa ila kuwa makini na watu wanaotaka kuangamiza taifa.

Nikajua huyu ni MTU mwenye roho nzuri akanipa elfu zangu kadhaa za nauli nikaondoka sikujiamini

Tokea siku hiyo nikawa makini sana sana sana.

Baada ya mwaka mmoja nikasikia kachukua form duh mama yangu tunapona kweli Tanzania ya madili hii watu watapona lakini ikabidi nimuunge mkono na nikamtumia meseji kumtakia kila la heri na nilifarijika kuona ananijibu meseji wakati viongozi wengi huwa hawajibu, sasa watanzania wameanza kuzoea na nashukuru Mungu kupata kiongozi wa namna hii japo million 60 niliikosa dah.

Yaan huyu jamaa hapendi rushwa nime experience hicho kitu hapendi rushwa na ana nia ya dhati kwa taifa ili, tumuombee sana na akisema ana maanisha.
 
Hii ni story ya kutunga yenye lengo la kusafisha ufisadi wa Nyumba za Umma, Meli Chakavu, kuhamisha fedha za umma kienyeji enyeji, kukandamiza Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea, kufumbia macho Escrow, Lugumi, Richmond, Kiwira, Rada, Kagoda, Meremeta. Nk.

Mwambie ajipange tena. Sisi hatudanganyiki.
 
"Nitawashusha Wanaoishi kama Malaika waishi Kama Shetani" JPM.

Baada ya miezi kadhaa

"Wanaopinga jitihada zangu za kupambana na Ufisadi ni mawakala wa Shetani" JPM

Sasa kama watu umeshawashusha kwa Shetani, wataachaje kuwa Mawakala wa Shetani?

Ukizitafakari hizi kauli mbili unapata wasiwasi na mtoa tamko.
 
Umesema huwa anajibu sms zako basi mwambie vijana wanasubiri ajira alizowahaidi ili wafanye kazi, au mil. 50 alizohaidi kwa kila kijiji ili waanze ujasiriamali. Pia mwsmbie watu wanaomba asizuie mambo yanayoruhusiwa kwenye katiba au atangaze hali ya hatari tujue moja.
 
Huyu jamaa ameongea mengi sana, ila concept yake sijaielewa. Anaongelea issue ya generator? Tena za KV 5.5 ambazo zinauzwa laki 6, yaani ameshindwa kabisa kuwasilisha mada, nimeamini kweli wewe bank teller. Kajipange upya uje na post ya maana ndugu, zaidi tatajua ndio walewale wa bk7.
 
Hii ni story ya kutunga yenye lengo la kusafisha ufisadi wa Nyumba za Umma, Meli Chakavu, kuhamisha fedha za umma kienyeji enyeji, kukandamiza Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea, kufumbia macho Escrow, Lugumi, Richmond, Kiwira, Rada, Kagoda, Meremeta. Nk.

Mwambie ajipange tena. Sisi hatudanganyiki.
Sure siyo yankutunga rejea mwaka Jana niliwahi kuiandika kivingine kama unadhan nadanganya, ni pm nikupe vielelezo
 
Hiyo kazi huko Benk uliipata ki mjomba mjomba au!
Mbona hadithi yako inaelea tu angani?
Kaka kazi hiyo sikuipata kimjomba MJOMBA na maeneo hayo nimeshatoka niko kwingine juu zaidi ya hapo , na kama unahisi unanibeza ni pm tujuane kwa CV tuone nan mkali
 
Back
Top Bottom