Ukweli Kuhusu Kilichotokea Ndago Singida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli Kuhusu Kilichotokea Ndago Singida

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Imebidi, Jul 15, 2012.

 1. I

  Imebidi JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Kiomboi, Singida katika idara ya elimu. Nilishiriki katika mikutano miwili ya CHADEMA iliyofanyika Ndago na Kinampanda na nilishiriki kupokea msafara kuanzia Mbelekese. Ukweli ni kwamba utaratibu wa kuvuruga mikutano ya CHADEMA uliandaliwa mapema kwa kuwashirikisha OCD, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Iramba Magharibi, na jambo hili tuliwaeleza viongozi wa CHADEMA kabla hawajafika Ndago. Mpango uliokuwepo na utakaokuwepo katika mikutano ya leo ni kuwaandaa vijana wasio pungua 50 wakiwa wamelewa chakari. Wao kazi yao ni kuhakikisha kwamba viongozi wa CHADEMA hawahutubii mikutano na wakijifanya hawaelewi basi mawe yapopolewe. Jambo hili halijawafurahisha watumishi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanaopenda haki, na kuna malumbano makali yanaendelea chini kwa chini.

  Sasa jana, mara msafara ulipofika Ndago na kabla mkutano haujafunguliwa wale vijana walikuwa wamekaa pembe tatu tofauti nyuma ya Mnyika, mbele kabisa karibu na barabarani na kushoto wakiwa wamejichanganya na maaskari. Lengo ilikuwa ni kumlenga mawe Mnyika moja kwa moja ili ionekana kwamba hatakiwi kabisa Iramba. Bahati nzuri aliposimama Waitara akaanza na tahadhari kali sana kwamba tunafahamu mipango yote haramu na akawaambia maaskari wanawajibika kulinda mkutano kwa sababu mkutano ni halali na una baraka zote za Jeshi la Polisi. Moja ya wale vijana alimpigia simu Mwigulu kwamba mpango wao umeingia mkenge kwa sababu jamaa wa CHADEMA wanaujua mpango mzima. Mwigulu alimfokea yule kijana kwa ukali sana na akamwambia anataka kuona mawe yanapigwa ndani ya dakika tano vinginevyo ajiandae. Moja kwa moja yule kijana akawaambia wenzake kwa ishara na wakatoa mawe mfukoni wakaanza kurusha. Purukushani ziliendelea na vijana wa CHADEMA wakawa wanajihami na kuwalinda viongozi waliokuwepo kwa karibu kabisa.

  Vurugu ziliendelea kwa takribani kati ya dk 20-30, na wananchi wengi kusambaratika. Waitara na Mnyika walionekana wakiwasiliana kwa simu na kuwalaumu polisi waliokuwepo, ambao wao walikuwa wanachekacheka tu. Ndipo utulivu ukarejea na wananchi walirudi kwa kasi ya ajabu, na mkutano ukajaa tena na Mnyika akaendelea kuhutubia. Mnyika alipokuwa anamalizia hotuba yake, ndipo landrover ya FFU ikaingia ikiwa imesheheni maaskari. Mnyika akawaambia wananchi kwamba maaskari wameingia lakini baada ya fujo kutokea na wananchi wamejilinda wenyewe.

  Mkutano uliisha kwa amani, na kisha msafara ukaelekea Kinampanda palipokuwa na Mkutano mwingine. Tukiwa pale Kinampanda ndipo habari zikaanza kusambaa kwa kasi kwamba kuna kijana ameuawa. Mkutano wa Kinampanda uliisha salama na hapakuwa na kurushwa mawe. Wananchi walihudhuria kwa wingi ukizingatia pale ndipo palipo Chuo cha Ualimu cha Kinampanda.

  Taarifa nilizozipata baadaye ni kwamba yule kijana aliuawa ndani ya nyumba ya mtu kando kidogo na mkutano ulipokuwa unafanyika. Mtu huyo pia anatajwa kuwa kada wa CCM aliyekuwa anagombea ukatibu kata na ndiye aliyepewa fedha na Mwigulu kuratibu shughuli nzima ya fujo.

  Sina uhakika kama mikutano ya leo ya CHADEMA itafanyika kwa sababu vijana wameshaanza kukamatwa na kuna hatari polisi wakazuia mikutano ya leo.

  Pamoja na yote haya, Mwigulu watu wanamchukia sasa hivi kwa mambo ya kihuni anayoyafanya. Hatujuwahi kuwa na Mbunge wa namna hii katika Jimbo hili.

  Bahati mbaya ndiyo nimejiunga na hii JF rasmi leo na sina uhakika kama nitapata sehemu na mtandao niweze ku-post tena.
   
 2. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa taarifa mkuu!
   
 3. M

  Magesi JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chemba go 2 hell
   
 4. g

  gabatha Senior Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Asante kwa kutujuza mkuu, ugdalimu una mwisho
   
 5. i

  ibange JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwigula ni moja ya wabunge waliofilisika na hana akili kabisa. Hawa ndio wanaoletaga vita na mauaji
   
 6. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa taarifa
   
 7. T

  Tewe JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Jf=tpb popote we jianae kuleta updates na karibu sana
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Shukrani sana mzalendo umejitahidi vya kutosha .Ila haya ni mafuriko kuyazuia si kazi nyepesi only time will tell
   
 9. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,125
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa mkuu,karibu jf omu ov gret sinkaz.
   
 10. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,125
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  afu ww kwanini unaquote threads ndefu hvi?inakua haina ulazima,unachosha watu
   
 11. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,672
  Likes Received: 17,728
  Trophy Points: 280
  Nilijua lazima iwe Mwigulu............kawafungisha tela polisi na OCD,hivi Mwigulu ulishindwa nini kugombea kwako Tegeta mpaka unakuja kuchonganisha vijana huku kwetu..........wewe wanao kina Joshua umewaandalia maisha mazuri, tuache na sisi kina Mnyika, watuandalie/watupiganie maisha mazuri..............leka kua pa-luula.....
   
 12. t

  the horse JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwa mtu mwenye uwezo wa kutafakari na kufuatilia mambo kwa kushirirkisha ubongo atagundua kuwa ulichokiandika ni povu tupu...
   
 13. t

  the horse JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  na wewe bila aibu unajiita great thinker..????
   
 14. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama haya unayotueleza ni sahihi, basi TBC ni chombo change serikali kinachopandikiza chuki na kupaka matope upinzani. Hali hii inaweza kuchochea uvinjifu mkubwa wa amani na kuleta vita ya wenyewe kwa wenyewe Kama radio moja ilivyochochea vita huko Kenya. Matukio Kama haya yanatakiwa yawekewe kumbikumbu na vielelezo sahii ili yafikishwe kwenye mahakama ya kimataifa kuishtaki viongozi wa serikali na dola kutumika katika uvunjifu wa amani.
   
 15. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  huyo marehemu kauwawa ndani nyumbani kwa mtu!?
  Kuna pro-CCM mmoja humu ndani jana alianza kutabiri hayo, yeye akasema marehemu wawili.

  itV wakajifanya kuwa wamepata news wakati wanatangaza habari, na kuwashutumu CDM moja kwa moja.

  Ukiangalia utagundua haya yalikuwa yamepangwa. Udhalimu mwisho wake aibu
   
 16. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,672
  Likes Received: 17,728
  Trophy Points: 280
  Tumika tu kama kondom, ila moyo wako unajua A-Z, lete basi taarifa yako itu-convince, sio kukashifu watu iihali umeshindwa kukosoa kwa hoja.......mi naamini vijana wa Mwigulu kuna vitu vikubwa sana anawafanyia kiasi cha kumwabudu, sidhani kama ni pesa tu, kuna makubwa mno ambayo siku tukijua hatuta amini, mngekuwa mnatunga mimba ingesha dhihirika
   
 17. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  karibu sana ndg Imebidi umeanza vizuri

  huu ndiyo mwisho wa hawa jama kama wana akili nzuri wangeacha watu wapime wenyewe lipi jema na bovu kitendo wanacho kifanya cha kuanzisha vurugu kinawazika haraka sana

  jambo la msingi wajisahihishe ili kulinda heshima yao
   
 18. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  rpc singida katangaza kuwa chadema imetoa maneno mabaya kuhusu mbunge wao ndipo wananchi wwakachukia,tbc ndivyo walivyoripoti.
   
 19. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  shukran za zati mkuu nimekukubari ila hapa kuna magamba wanasumbu inabid uwavumilie cdm hawakatishw tamaa!!
   
 20. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  CHADEMA watalaumiwa sana hata TBC walionyesha hali ya kuwalaumu ninacho sema hizi lawama zitaondoka pale CHADEMA watakapo kuwa na chombo chao cha habari ambacho kitakuwa kikieleza ukweli halisi

  lakini pia kuna tatizo la wanahari wa CHADEMA maana hata ukifungua blog ya ya M4C huoni recent issue au ufafanuzi wa karibuni
   
Loading...