Ukweli kuhusu Abdalah Ngajurange

Ukweli kuhusu Abdalah Ngajurange

Adolph

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2010
Posts
895
Reaction score
346
Ndugu zangu ningependa niwape Taarifa sahihi kuhusu bwana Abdallah Ngajurage aliyejitangaza kwamba alikua ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kibaha Vijijini na ameamua kurudi CCM kutokana na kuchoshwa na UKABILA na UDINI ndani ya Chadema

Kwanza kabisa kabla ya yote ningependa mumjue huyu Abdallah Ngajurage ni nani. Abdallah Ngajurage kweli ni mkazi wa Kibaha vijijini Kijiji cha Mpiji . Alikua ni mjumbe wa serikali ya kijiji kupitia chama cha mapinduzi hadi mwaka jana mwezi wa nne Katika mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika kijijini kwake Mpiji ambapo alijiunga rasmi na chadema na alitamka hadharani kwamba amechoshwa na ubadhirifu, unyonyaji na ahadi hewa za chama cha mapinduzi

Mwezi mmoja baadae yaani Tarehe 10/05/2012 CHADEMA Jimbo la Kibaha vijijini kulikua na uchaguzi wa Viongozi wa jimbo. Bwana Abdallah Ngajurage akaamua kujitosa kugombea nafasi ya mwenyekiti wa jimbo. Chadema jimbo la kibaha bila kuangalia DINI yake ( Uislam) wala bila kuangalia KABILA lake ( Mzaramo) na bila kuangalia chama alichotoka (Chama cha Mafisadi) wakakubali agombee nafasi ya Mwenyekiti. Katika uchaguzi huo alishinda na Thobias Charles ambapo alimshinda Thobias kwa kura moja hivyo kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Kibaha Vijijini

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kibaha vijijini alihimiza wanachama wa Chadema wachange pesa ili kulipia pango la ofisi. Cha ajabu baada ya michango kukamilika alikabidhiwa pesa yote iliyopatikana 120,000/= na akalipia pango 60,000/= nyingine akatokomea nazo na hakuonekana hata kwenye vikao vya chama. Ikawa kila siku ni visingizio kwamba yupo busy na shughuli zake.

Ilipofika mwezi wa saba mwaka jana kulikua na kikao cha dharura kumjadili mwenyekiti Abdallah Ngajurage. Bwana Abdalah Ngajurage aliitwa ili ahojiwe kuhusu utendaji kazi wake mbovu, tuhumu za wizi na kutoonekana ofisini tangu achaguliwe. Hakutokea kwenye kikao na wanachama wakaamua kwa kauli moja Fatuma abdalah kukaimu nafasi ya uenyekiti.

hakuwai kusikika tena wala kuonekana tena hadi hapo juzi alipojitangaza kwamba amehamia ccm akiwa kama mwenyekiti wa Chadema KIbaha vijijini..nashindwa kuelewa alikua mwenyekiti wa nani toka mwezi wa saba hajui hata ofisi yake ilipo leo anajitangaza kwa mbwembwe kama mwenyekiti wa chadema kibaha vijijini..

Madai ya Abdallah Ngajurage kwamba Chadema chadema kimetawaliwa na UDINI na Ukabila hayana hata chembe ya ukweli. Labda tuanze kumuuliza yeye alichaguliwa kwa dini au ukabila? Ngoja niwapatie mchangajiko wa viongozi ndani ya chadema kibaha vijijini 1. mwenyekiti Fatuma abdalah(mpemba)
2. Katibu ndugu John Luturagara(muha)
3. Katibu Mwenezi ndugu Saddala Iddi Chacha(mkuria)
4. Mwenyekiti wa baraza la wazee ndugu Ally Shomvi(mzaramo)
5. Katibu baraza la wazee Mtegeku(mhaya)
6. katibu bawacha Zawadi Salimu(mdigo)
7. Mwenyekiti wa bavicha Agrey Dudu(msambaa)

8. katibu wa bavicha ndugu Edson(------)
9. Mtunza hazina ndugu Zawadi Abdalah(------)

Huo ndo uongozi mzima wa jimbo la kibaha vijijin. Swala udini na ukabila liko wapi? Amefanya nini kwa chadema ili kuzuia huo udini na ukabila anaousema? Mbona hajaonekana kwenye chama toka akimbie na tsh 60,000/= ?

TUMECHOKA NA PROPAGANDA UCHWARA ZA CCM

NAWASILISHA!!

mkuu adolf magamba wanahaha sana. everywhere ni propaganda dhidi ya cdm. yaani wanatupa promo kwa kisigino.
 
hongera sana mkuu Adolf,kweli ww ni mzalendo halisi,udini,ukabila na ukanda avina nafasi ktk utendaji wako
 
Mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe!!CDM wawe macho,mamluki wako wengi kuliko anavyooneka Shibuda na Masalia!!!Dawa nikutoa dozi mpaka nahao mamluki waone bora wahamie kiukweli nasikukaa kimamluki kusubiri 2015 ooh ninarudi nyumbani......watanzania tuangalia nakufuatilia 2015 wengi tutawajeruhi kwenye sanduku la kura we waache!
 
ccm wanaishi kwa propaganda za ajabu sana....
 
Hata mm kinakirefu nikiwaita na kuwaambia n katibu wa chama chadema wilaya na nataka kujitoa nihamie magamba chama, watashangiria sana, magamba hayana akili yanajua tu kusema ccm oyeeeeeee, hakuna zaidi yanachojua haya ma mtu
 
Mbona kuna mtu alikuja na maelezo kuwa huyu hakuwahi kuwa mwenyekiti bali kaimu mwenyekiti sasa tumuamini wewe au yeye
 
Hatari kubwa CCM kutumia pesa za walipa kodi kupambana na Chadema .Kila kukicha ni Chadema sasa imekuwa ni sera sa oxygen maana nila hivyo wanakufa
 
Mkuu, mimi siku zote nasema CCM hakuna kiongozi ambae maono yake yanakwenda zaidi ya futi mbili mbele! Wao kwa sasa nguvu, mali na uwezo vyote wamevielekeza kuingamiza Chadema. Hawana upeo wa kuona vitu kama haya madai ya gesi Mtwara ni outcome ya wananchi kuchanganyikiwa na maisha magumu. Nakuhakikishia hizi fujo na migongano inayoendelea; mara huyu ndio anatakiwa kuchinja, mara gesi haitoki nk.... vyote ni matokeo ya uongozi ulioshindwa. Kikwete hana kipaji cha uongozi. Lakini hataki kukubali
 
Magamba wana akili za maiti damas alijifanya katibu mwenezi cdm kata ya saranga kavuta hela yake anatusumbua bar hapa stop ova
 
daaah,
dullah anazingua sana,sasa hiyo laki na 20 itamfikisha wapi??
 
Ndugu zangu ningependa niwape Taarifa sahihi kuhusu bwana Abdallah Ngajurage aliyejitangaza kwamba alikua ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kibaha Vijijini na ameamua kurudi CCM kutokana na kuchoshwa na UKABILA na UDINI ndani ya Chadema

Kwanza kabisa kabla ya yote ningependa mumjue huyu Abdallah Ngajurage ni nani. Abdallah Ngajurage kweli ni mkazi wa Kibaha vijijini Kijiji cha Mpiji . Alikua ni mjumbe wa serikali ya kijiji kupitia chama cha mapinduzi hadi mwaka jana mwezi wa nne Katika mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika kijijini kwake Mpiji ambapo alijiunga rasmi na chadema na alitamka hadharani kwamba amechoshwa na ubadhirifu, unyonyaji na ahadi hewa za chama cha mapinduzi

Mwezi mmoja baadae yaani Tarehe 10/05/2012 CHADEMA Jimbo la Kibaha vijijini kulikua na uchaguzi wa Viongozi wa jimbo. Bwana Abdallah Ngajurage akaamua kujitosa kugombea nafasi ya mwenyekiti wa jimbo. Chadema jimbo la kibaha bila kuangalia DINI yake ( Uislam) wala bila kuangalia KABILA lake ( Mzaramo) na bila kuangalia chama alichotoka (Chama cha Mafisadi) wakakubali agombee nafasi ya Mwenyekiti. Katika uchaguzi huo alishinda na Thobias Charles ambapo alimshinda Thobias kwa kura moja hivyo kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Kibaha Vijijini

Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kibaha vijijini alihimiza wanachama wa Chadema wachange pesa ili kulipia pango la ofisi. Cha ajabu baada ya michango kukamilika alikabidhiwa pesa yote iliyopatikana 120,000/= na akalipia pango 60,000/= nyingine akatokomea nazo na hakuonekana hata kwenye vikao vya chama. Ikawa kila siku ni visingizio kwamba yupo busy na shughuli zake.

Ilipofika mwezi wa saba mwaka jana kulikua na kikao cha dharura kumjadili mwenyekiti Abdallah Ngajurage. Bwana Abdalah Ngajurage aliitwa ili ahojiwe kuhusu utendaji kazi wake mbovu, tuhumu za wizi na kutoonekana ofisini tangu achaguliwe. Hakutokea kwenye kikao na wanachama wakaamua kwa kauli moja Fatuma abdalah kukaimu nafasi ya uenyekiti.

hakuwai kusikika tena wala kuonekana tena hadi hapo juzi alipojitangaza kwamba amehamia ccm akiwa kama mwenyekiti wa Chadema KIbaha vijijini..nashindwa kuelewa alikua mwenyekiti wa nani toka mwezi wa saba hajui hata ofisi yake ilipo leo anajitangaza kwa mbwembwe kama mwenyekiti wa chadema kibaha vijijini..

Madai ya Abdallah Ngajurage kwamba Chadema chadema kimetawaliwa na UDINI na Ukabila hayana hata chembe ya ukweli. Labda tuanze kumuuliza yeye alichaguliwa kwa dini au ukabila? Ngoja niwapatie mchangajiko wa viongozi ndani ya chadema kibaha vijijini 1. mwenyekiti Fatuma abdalah(mpemba)
2. Katibu ndugu John Luturagara(muha)
3. Katibu Mwenezi ndugu Saddala Iddi Chacha(mkuria)
4. Mwenyekiti wa baraza la wazee ndugu Ally Shomvi(mzaramo)
5. Katibu baraza la wazee Mtegeku(mhaya)
6. katibu bawacha Zawadi Salimu(mdigo)
7. Mwenyekiti wa bavicha Agrey Dudu(msambaa)

8. katibu wa bavicha ndugu Edson(------)
9. Mtunza hazina ndugu Zawadi Abdalah(------)

Huo ndo uongozi mzima wa jimbo la kibaha vijijin. Swala udini na ukabila liko wapi? Amefanya nini kwa chadema ili kuzuia huo udini na ukabila anaousema? Mbona hajaonekana kwenye chama toka akimbie na tsh 60,000/= ?

TUMECHOKA NA PROPAGANDA UCHWARA ZA CCM

NAWASILISHA!!

MTU KAMA HUYU KWA KIINGEREZA AMAITWA " A POLITICAL PROSTITUTE " kumpoteza sio hasara
 
Ukweli ni Kwamba propaganda za CCM kuwagawa wananchi kwa ukabila udini ukanda zinawarudi wenyewe na wakiendelea melody hiyo itawafanya waondoke nalo hata kabla ya mwaka 2015 hivi wanaona nchi ilivyotete huu si wakati wa kuongea vitu vya kijinga kama hivyo
 
Back
Top Bottom