Ukweli: Kama Lowassa angekuwa rais, MCC wasingeweka pembeni faili la Tanzania

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Tutashabikia weee, tutajifanya wajuaji weee, tutatoa mapovu weee, tutajufariji weee, tutatofautiana weee, lakini ifike mahala nyeusi tuiite nyeusi na nyeupe tuiite nyeipe.

Ukweli kabisa Tanzania tunahitaji kujitegemea nak tunahitaji kabisa kuwa among the doner countries lakini bado tuna safari ndefu, bado inayohitaji hekima, mikakati na elimu ya kutosha ya uchumi wa kujitegemea.

Kuota ndoto usiku na kukurupuka asubuhi kusema we are going to be the doner country itatusaidia tu kujaza kurasa humu za kusifiana na kujazana vichwa, lakini itabaki nadharia bila kuwa kabisa na clear vision na objectives hatutaamka tu asubuhi tukajikuta tunajitegemea.

Hebu jiulize Machine mbili tu za MRI na CT scan zimeihenyesha serikali imeshindwa kulipa billion saba zinazodaiwa tatizo likafumbuliwa au kununua nyingine mpya kila siku ni kurepea repea viraka alafu unataka ufukuze watendaji!

Turudi kwenye mada sasa! Kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa ni kweli kwamba swala la zanzbar limechelewa sana na inahitajika mtu ambaye kweli amejaa hekima na busara kuweza kulimaliza mi simuoni mwingine kwa sasa zaidi ya Mh Lowasa... Na hapa tutamkumbuka sana pamoja na ushabiki wetu. Hivi niwaulize swali?

Juzi si tulimuona Mwigulu kule morogoro na vyombo vya habari kwenye mgogogoro wa wakulima na wafugaji? Alipoondoka tu kesho yake watu ishirini na mbili walifyekwa mapanga na mikuki je alirudi tena? Na je tatizo limeisha?

Hii nchi bado haiwezi kujitegemea kwa sasa iko kwenye kujenga misingi ya kujitegemea misaada ikikatwa moja kwa moja hakuna rangi mtaacha kuona.. "Maisha ni hatua huwezi kusimama kabla huja kaa" kufanya mambo kibabe tukidhani tayari tunaweza, itawaumiza hasa wale ambao mvua isiponyesha serikali inatakiwa iwe na chakula cha kutosha kwenye ghala Cha kuwasaidia sio kuwapa kopo tano unaita media tumetoa misaada ya njaa.

Mtu ambaye mshahara wake ni zaidi ya million 36 na anazipewa baada ya miaka mitano ya kazi hata akiharibu hatoathirika sana.

Tanzania ni yetu sote twende mbele turudi nyuma, wa CCM kaolewa na wa UKAWA, wa bara kaolewa na wa visiwani lolote likitokea wote ni wahanga.

Sijui kwanini nawaza sana juu ya hatma ya Tanzania..kila ukidhani mnapiga hatua kumbe indirect mnarudi nyingine kumi lakini mtanzania aliyeitwa kichwa cha mwendawazimu hataki kushirikisha ubongo amebaki kucheka tu na kushabikia kila kitu.
 
Tanzania yangu democrasia bado safari ndefu sana.
 
Magufuli kaachiwa zigo la Zanzibar ambalo kwake ni kumwonea. Msoga ndiye alipswa kulishughulikia.

kWELI KABISA. ila jambo jema ni kwamba tunkoelekea na kasi hii, hata hizo pesa za MCC hatutakuwa na haja nazo. Tumuunge mkono rais ili hawa Wazungu washike adabu. Wanatushia NYAU ili iweje.
 
kWELI KABISA. ila jambo jema ni kwamba tunkoelekea na kasi hii, hata hizo pesa za MCC hatutakuwa na haja nazo. Tumuunge mkono rais ili hawa Wazungu washike adabu. Wanatushia NYAU ili iweje.

Kweli tunamuunga mkono hata sasa ila hiyo ishu ya pesa kwa sasa hatuwezi kataa kuihitaji na tuliihitaji hadi hapo tuliposhtuka tumenyimwa nd0 tukaanzisha visababu flaniflani hivi vya mkosaji. Ukweli utatuweka huru daima. Msaada bado tunahitaji sana tu hadi mambo yetu yatakapotengemaa.
 
ukishanyimwa unasonga mbele siyo mambo ya angekuwa fulani, ujinga huo. unajikombakomba nini?
 
kwa SABABU Marekani wangejua iko siku zitawarudia kwa mlango wa Nyuma? Sasa wataisoma namba. Msukuma siyo mjinga kama akina LOWASSA.

Hivi we unaishi sayari gani...huku msikia Magufuli wakati ule alivyoongea kwa mbwembwe na furaha aliposikia marekani kupitia MCC inampango wa kuipa Tanzania msaada wa mradi wa umeme vijijini... Ukiwa huna taarifa ya jambo jifunze kutokukurupuka utasitiri jambo fulani
 
kWELI KABISA. ila jambo jema ni kwamba tunkoelekea na kasi hii, hata hizo pesa za MCC hatutakuwa na haja nazo. Tumuunge mkono rais ili hawa Wazungu washike adabu. Wanatushia NYAU ili iweje.
Dawa za UKIMWI, DAWA ZA TB, DAWA ZA MALARIA, CHANJO ZOTE tunawategemea wazungu hivi wakisitisha hii misaada na wewe utapona?
 
Back
Top Bottom