aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 792
- 1,144
Hatimae Waziri wa nishati na Bunge limekubaliana na ukweli juu ya jinsi Wazanzibar tunavyodhulumiwa kuwekewa makato ya ziada kwenye Umeme.
Makato hayo Ni:
3% Umeme vijijini (REA)
2% Energy and Water Regulatory Authority. (EWURA)
Pia kuuziwa kwa bei ya retail price(rejareja) shirika la Zecco Kama anavyonunua Mtu binafsi.
Jana niliweka ujumbe hapa kuhusu hili jambo na jioni walikubaliana na hoja za wabunge wetu na hatimae wamekubali mpaka tarehe 25/6 hili Jambo litakuwa limepatiwa majibu.
Shukran za dhati kwa Spika Ndugai kulipa uzito Jambo hili na kukubali kwamba hii sasa linakuwa ni Jambo la Bunge zima na ukitaka serikali kulimaliza kwa muda uliowekwa.
Pia nimshukuru MH Najma Giga mbunge pekee kutoka CCM Zanzibar kuungana na wabunge wetu makini kutoka CUF kusimamia Hoja hii pamoja huku akiwaacha wabunge wengine wa ccm kama vile jambo hili haliwahusu.
Hakika utumwa wote ni mbaya lakini utumwa wa kutawaliwa kifkra ni mwisho wa uovu. Hata jambo hili wabunge wa Zanzibar walisubiri amri ya Balozi mkaazi?
Wabunge wetu pamoja na kutoitambua serikali iliopo Zanzibar lakini kwa kujali wananchi wanyonge wameamua bila kujali kuwa maslah yakipatikana Zanzibar yatapitia mikononi mwa haohao. Hapa lengo Ni unafuu kwa wananchi wetu.
Inaumiza sana tukiwa hapa bungeni unamsikia waziri wa madini wa Tanganyika akisisitiza wananchi wa Tanganyika waungiwe Umeme kwa sh 27,000/-tu. Wenzetu wana Dhahabu, gesi, almasi, na mali tele kwa tele lakini bado serikali yao inawapa unafuu huo huku kodi ya REA na EWURA wakibebeshwa wanyonge wa Zanzibar ambao vijiji vyao havijawahi kunufaika na msaada wa REA.
Tujiulize huko Zanzibar ni kiasi gani mnyonge wa Mungu inabidi apapatue kuunganishiwa Umeme? Nasikia kima cha chini Ni 18000/
Kweli tuna serikali inayowajali watu wake?
Kweli tuna wawakilishi wanaojali matatizo ya watu wetu?
Hakika inauma wachaguliwa na wananchi waliopo bungeni wanaposhindwa kutetea maslah ya Zanzibar
Wanasahau kwamba bila Zanzibar wasingeitwa waheshimiwa.
Naamini Mungu muweza anasikia kilio Na mateso ya wazanzibar Na yeye ndio tegemeo letu.
Mola wetu tuondolee udhalim huu-
Amein