Ukweli haupingiki; Wazanzibar tunadhulumiwa na TANESCO kwa kuwekewa makato ya ziada kwenye umeme

we don't provide free lunch to anybody kila kitu mnalalamika
vunjeni muungano mtengeneze umeme wenu wa bure mjiunge na ile OIC yenu mnayopigiaga kelele. kodi zetu zinawalisha alafu kelele nyingi vunjeni muungano simple
Hakuna Mazanzibar hata mmoja anaeutaka muungano
 
Tuta lalamika mpaka mutakapo tuachia tupumuwe maana nyie ndio munao lazimisha haya kila tukijipapatuwa munatuletea majeshi
Kama musinge tufanyia vurugu kwenye uchaguzi basi wakati huu tungalikuwa tuna zungumza mengine maana ingalikuwa tusha wakimbia mbaali na munaanza tena kupanda maboti kuja kuchukuwa bizaa

InshaaAllah iko siku yatakuwa tuu mutayona tena mukiambiwa eti munatubeba sasa mimi nawauliza umeona wapi mtu ambae hachoki kumbeba huyo mtoto wako unamuweka chini
Hamna lolote nyinyi ndio tuna wabeba tena munataka tuwabebe kwa nguvu
Hebu angalini zenj kuna watu 2m lakini kuna kambi 10 za jeshi mbali za police sasa nambie dar ina watu wangapi na ina kambi ngapi za jesh?
 
Balozi seif ali iddi, wana usemi wao huku zenji ni balozi mkaazi kutoka tanganyika kwa lugha nyengine ni pandikizi la tanganyika katika SMZ
Hahahahaaaa sawa bwana sikujua hilo eti balozi mkaazi lol
 
HV kwa akili ya kawaida nijibiwe swali hili
"Wasioutaka muungani in wepi?
Wazanzibari au Watanganyika?

Ni yupi anaetumia nguvu zaidi kuhakikisha Muungano hauvunjiki?
 
Sasa tunachotaka sisi hiyo Package iondolewe maana ni un necessary costs, ni kawaida kwenye biashara munapoeka mikataba ukaona Costs ambazo si za ulazima ni kukaa kitako mkafanya negotiations mkaziondoa hizo cost. Asante kwa kunifunua macho kwa kunipa mfano wa dangote, hapo nimejifunza jinsi gani Tanganyika inavoikandamiza Zanzibar. Maana tukitaka tusitake hizi Package ulizosema hazina faida hata moja kwa Zanzibar.
Biashara ni mapatano ila kwenye utilities kama gesi, maji, umeme, petrol sio mapatano tena bali it is regulated.

Kwenye taasisi za muungano ziko taasisi ambazo ni za bara tuu lakini mandate yake inaextend hadi Zanzibar, Ewura ndio regulator wa utilities Tanzania kama ilivyo TCRA kwa mawasiliano na Sumatra kwa vyombo vya usafiri, TCAA kwa usafiri wa Anga, SSRA kwa mifuko ya hifadhi za jamii etc etc. Tanesco iko regulated na Ewura na REA ni sera ya nchi. Kinacholipishwa ni kinachozalishwa hivyo umeme wowote ambao Tanesco itazalisha na kuuza popote hizo charges za Ewura lazima zipo na aloyeziweka sio Tanesco ni Ewura. Hata tukkwauzia umeme Kenya zitakuwepo kwa sababu zinatoka pale umeme unapozalishwa.

Hata hivyo ZECO inaweza kujenga hoja kuwa kwa vile wao hawana REA, then ule mchango wa REA uondolewe. Ila pia ZECO wawe tayari kufidia kwenye usafirishaji.
P
 
Wabunge weng huku zanzibar wanakula tu pesa sio kwamba ugumu wa maisha unasababshwa na tanesco hapana...ila pia n vyema bei za tanesco zikawekwa sawa kwa zanzibar....

ila tunaomba mwenye data juu ya umeme wanaotumia kagera unaotoka uganda watuoneshe tunavowalipa uganda labda itasaidia
 
Hatimae Waziri wa nishati na Bunge limekubaliana na ukweli juu ya jinsi Wazanzibar tunavyodhulumiwa kuwekewa makato ya ziada kwenye Umeme.

Makato hayo Ni:
3% Umeme vijijini (REA)
2% Energy and Water Regulatory Authority. (EWURA)
Pia kuuziwa kwa bei ya retail price(rejareja) shirika la Zecco Kama anavyonunua Mtu binafsi.

Jana niliweka ujumbe hapa kuhusu hili jambo na jioni walikubaliana na hoja za wabunge wetu na hatimae wamekubali mpaka tarehe 25/6 hili Jambo litakuwa limepatiwa majibu.

Shukran za dhati kwa Spika Ndugai kulipa uzito Jambo hili na kukubali kwamba hii sasa linakuwa ni Jambo la Bunge zima na ukitaka serikali kulimaliza kwa muda uliowekwa.

Pia nimshukuru MH Najma Giga mbunge pekee kutoka CCM Zanzibar kuungana na wabunge wetu makini kutoka CUF kusimamia Hoja hii pamoja huku akiwaacha wabunge wengine wa ccm kama vile jambo hili haliwahusu.

Hakika utumwa wote ni mbaya lakini utumwa wa kutawaliwa kifkra ni mwisho wa uovu. Hata jambo hili wabunge wa Zanzibar walisubiri amri ya Balozi mkaazi?

Wabunge wetu pamoja na kutoitambua serikali iliopo Zanzibar lakini kwa kujali wananchi wanyonge wameamua bila kujali kuwa maslah yakipatikana Zanzibar yatapitia mikononi mwa haohao. Hapa lengo Ni unafuu kwa wananchi wetu.

Inaumiza sana tukiwa hapa bungeni unamsikia waziri wa madini wa Tanganyika akisisitiza wananchi wa Tanganyika waungiwe Umeme kwa sh 27,000/-tu. Wenzetu wana Dhahabu, gesi, almasi, na mali tele kwa tele lakini bado serikali yao inawapa unafuu huo huku kodi ya REA na EWURA wakibebeshwa wanyonge wa Zanzibar ambao vijiji vyao havijawahi kunufaika na msaada wa REA.

Tujiulize huko Zanzibar ni kiasi gani mnyonge wa Mungu inabidi apapatue kuunganishiwa Umeme? Nasikia kima cha chini Ni 18000/

Kweli tuna serikali inayowajali watu wake?
Kweli tuna wawakilishi wanaojali matatizo ya watu wetu?
Hakika inauma wachaguliwa na wananchi waliopo bungeni wanaposhindwa kutetea maslah ya Zanzibar
Wanasahau kwamba bila Zanzibar wasingeitwa waheshimiwa.

Naamini Mungu muweza anasikia kilio Na mateso ya wazanzibar Na yeye ndio tegemeo letu.
Mola wetu tuondolee udhalim huu-
Amein

Muwachunie hao TANESCO na mtumie vibatari tu au mishumaa.
 
Umeme mwautaka.. wekezeni kwenye mitambo ya kuzalisha umeme.. Wazanzibari hamshindwi
 
Nashauri viongozi wa Zanzibar wawekeze kwenye Wind Energy. Wamezungukwa na bahari pande zote hivyo wana fursa ya kuweka mioundombino ya Wind Farm baharini. Kuna masuala ya solar power pia. Kila jengo la serikali na binafsi linalojengwa lazima liwe na miundombinu ya solar. Hii itapunguza utegemezi kutoka Tanesco na madeni yao wataweza kuyamudu. Kisitokee kisingizio kwamba suala la nishati ni la muungano wakati wamepigana kuyaondoa mafuta ktk masuala ya muungano.
 
Tatizo kuna harufu ya ufisadi kwenye hili suala la tanesco kwa viongozi wa CCM
 
Back
Top Bottom