Ukweli ambao wengi hatuutambui

Ukweli ambao wengi hatuutambui

SMART PASSENGER

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
1,274
Reaction score
1,933
Maisha yanatufundisha kwamba mara nyingi hatujui thamani ya kitu mpaka tunapokaribia kukipoteza.
Tunapokuwa nacho, tunakichukulia kawaida. Tunakitumia bila kufikiria kesho. Lakini pale kinapoanza kupungua, ghafla tunaanza kukiona cha muhimu sana.

Mfano mzuri ni simu ikiwa na 90% battery. Unaendelea kuitumia bila hata kujali kesho kama vile NI Mali ya serikali Lakini ikifika 1%, ghafla kila kitu kinabadilika. Unazima Bluetooth, data, location, brightness… hata vibration unaanza kuiona kama adui wa taifa. 😂

Unaanza kutafuta charger kwa haraka, unauliza kila mtu: “Una charger ya aina hii?” Na ukiona simu imebaki 1% lakini bado haijazima, unaanza kuiheshimu kama mgonjwa wa ICU. 😂
 
Back
Top Bottom