Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,582
- 28,737
Wakuu
Miaka ya nyuma(si zamani sana) nchi ya Ujerumani ilikua imejengwa ukuta uliokuwa ukiigawa katika pande mbili yaani Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi, na mara baada ya kujenga ukuta huu zilikua ni nchi mbili tofauti kabisa kila moja ikiwa na mfumo wake wa utawala.
Miaka ya hivi karibuni ukuta huu ulibomolewa na kuifanya Ujerumani kurudi tena kuwa moja baada ya miaka mingi ya mgawanyiko wake.
Kuna mtu yeyote anaweza kufahamu undani wa kwa nini ukuta huu ulijengwa??
Mfumo wa utawala wa pande hizi mbili baada ya kujenga ukuta ulikuaje??
Nini kilipelekea ukuta huu kubomolewa na kuirudisha Ujerumani kuwa moja bila kuwepo mikwaruzano yoyote ya kiutawala na kimadaraka mpaka sasa??
Nani aliyekuwa nyuma ya pazia ya mgawanyiko huu wa Ujerumani.
Nawasilisha
cc The Emperor, Udadisi, TIGOPESA
Mshikaji Si Ugoogle Tu!
Ukutawa Berlin (Kijerumani Berliner Mauer) ulitenganisha sehemu mbiliza jiji la Berlin (Ujerumani) kuanzia 13 Agosti1961 hadi 9 Novemba1989.
Mashariki ya Berlin ilikuwasehemu ya nchi ya kikomunisti Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani na magharibi ya jiji ilikuwa chini yamamlaka ya Marekani, Uingereza na Ufaransa. Ukuta huu ulikuwa na urefu wa kilomita45.3 ukiwa sehemu ya mpaka kati ya madola mawili ya Ujerumani yaliyokuwepo kuanzia1949 hadi 1990. Ukuta wa Berlin ulikuwa mfanouliojulikana zaidi wa "pazia la chuma" katika Ulaya lililotenganisha nchi zakikomunisti za Ulaya mashariki na nchi za Ulaya magharibi. Takriban watu 200waliuawa walipojaribu kuvuka ukuta kutoka mashariki kwenda magharibi.
kuhusunani alibomoa ukuta.
1.Ukoministi ulipoanza kuporomoka UlayaMashariki, ukuta huo ulibomolewa na watu wa mji wa Berlin, mwaka wa 1989.
kuhusu nani aliyekuwa nyuma ya pazia yamgawanyiko huu wa Wajerumani.
2.Chanzo cha ukuta ulikuwa ugawaji wa jiji la Berlin baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia tangu 1945. Nchi washindi ziliamuakugawa Ujerumani yote wakaanzisha kanda nne zilizotawaliwa na Umoja wa Kisovyeti, Marekani, Uingereza na Ufaransa. Berlinilikuwa ndani ya kanda ya kisoyeti lakini ikiwa mji mkuu wa Ujerumaniilitangazwa kuwa mkoa wa pekee ikagawiwa pia katika kanda nne za washindi.Tangu 1946 washindi walianza kutoelewana na kipindi cha vita baridi kilianza ambako nchi za magharibi (Marekani,Uingereza, Ufaransa) zilisimama dhidi nchi za mashariki zilizoongozwa na Umojawa Kisovyeti.
Sina uhakika kama mleta mada alitaka kujua kama baada ya nchi hizi mbili kuachana na uhasama wao na kuungana kwa sasa zinatumia mfumo gani wa muungano!
Naomba kama kuna mwenye uelewa wa hili atujuze pia ili tujue kama ni serikali mbili au nako kuna 'mvaa koti'.
Asante mkuu kwa kuliona hil
cc: TIGOPESA, asigwa