Ukuta kuadhibu waendao haja ndogo ovyo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,870
34,357
151218163151_anti_pee_london_512x288_publicispixelpark.jpg
Baraza la Hackney limekuwa likitumia ?100,000 kila mwaka kusafisha kuta.

Aina mpya ya rangi ambayo imeundwa kwa mtindo maalum ili kurejesha mkojo kwa anayejaribu kuukojolea ukuta uliopakwa rangi hiyo, imeanza kujaribiwa na manispaa moja jijini London.

Rangi hiyo ya majimaji itakuwa ikipakwa katika maeneo maarufu kwa wanywaji pombe, katika tarafa za Shoreditch na Dalston, mashariki mwa London.

Manispaa ya Hackney, imesema imekuwa ikitumia ?100,000 kusafisha mkojo kutoka katika kuta za manispaa hiyo na pembezoni mwa barabara, mahala ambapo watu huenda haja ndogo ovyo.

Feryal Dermici, ambaye ni mbunge wa manispaa hiyo anasema: "ikiwa hatua ya kuwapiga faini haiwazuii kukojoa ovyo barabarani na pembezoni mwa njia, sasa hatari ya kumwagikiwa na mkojo wao wenyewe, litakuwa jambo la busara".

Sasa, adhabu ni kujenga kizuizi itakayopakwa rangi ambayo itawezesha mkojo kumrudia mkojoaji, ili anapomwagikiwa na mkojo wake mwenyewe, basi atapata adhabu inayomfaa.

Pia lengo jingine ni kuzuia mkojo kulowesha ukuta, kuondoa madoadoa ya uchafu na uvundo.

Haijafichuliwa hasa maeneo ambayo itapakwa rangi hiyo, ili wanaoenda haja wasijue na kukwepa maeneo hayo pekee.

Chanzo: BBC
 
1450834580902.jpg hii inafaa kuja hapa bongo na kwa kuanzia ifungwe mitaa ya Posta na kariakoo
 
Huyu anakojoa kasimama 90?, ntajaribu kusimama 45? afu nalimwaga
 
Back
Top Bottom