Habari wakuu,
Ikiwa zimebaki siku 15 tu kuanza kwa ile oparesheni yetu maarufu ya UKUTA, mambo si shwari hapa Ufipa.
Mpaka sasa duru zinaonyesha hii kitu itashindwa vibaya hasa baada ya makamanda wenye ndoa kuingia mitini katika kuisupport operation hii. Zile juhudi za JOYCE KIRIA kuhamasisha wake na familia za makamanda kuwazuia kushiriki zimezua taharuki kubwa kwani zinaonekana kufanikiwa kwa kasi huku zikiungwa mkono pia kwa kasi kubwa na wake wa viongozi, ambao ni members wa BAWACHA.
Wake hao wamembana kooni mwenyekiti wao na kumzuia kutoa tamko lolote kuhusu UKUTA, ndo maana mpaka sasa BAWACHA wako kimyaa kama maji.
Kumekuwa na vikao vya dharura vya kutosha, vikilenga kuhakikisha CC inatafuta suluhisho au mwanya wa majadiriano na Mh Rais ili kuepusha "kikombe hiki" ambacho wamekitangaza lakini zimegonga mwamba hasa baada ya upande wa rumumba kukataa katakata.
Kwa kweli UKUTA mpaka sasa mustakabari wake haueleweki, kwani ilipangwa mwezi mzima wa nane utumike kuhamasisha kupitia MITANDAO YA KIJAMII, hatahivyo hili pia halijafanikiwa kwani JOYCE Kiria na team yake wameliwekea upinzani wa kutosha.
Ikumbukwe hata Mgeni wetu maarufu Ndugu EL hauingi mkono mkakati huu wa mwenyekiti,kwani amewahi kutangaza hadharani kuwa siasa za kiharakati na maandamano si STYLE yake. Kutokuungwa mkono na EL pia kunaacha pengo kubwa kwani timu ya vijana iliyo nyuma yake nayo imeamua kukaa kimya.
UKUTA unaelekea kuanguka kabla hata haujasimama, Ufipa hata vikao havikaliki huku. Ingawa mambo ni magumu ila tumeapa HATUNYWI SUMU WALA KUJINYONGA