NIlipelekwa mpaka kwa mwenyekiti. Wakati tunaelekea huko kuna watu nilikuwa nawaona sura zao kama nazifahama, wengine ni viongozi wakubwa kabisa. Lakini ilinibidi nikae kimya maana sikui kitu gani kinafuata.
Mwenyekiti, akafungua kitabu cheusi kikubwa akaanza kuniuliza Jina, umri wangu na maswali kadha wa kadha yanayoniuhusu mimi. Kisha akasema kuna sifa tumezipata kupitia kwa Misoji ngoja tutakujaribu tuone kama kweli sifa hizo ni za kwako.
Baada ya hapo tukaambiwa mnaweza kuendelea sasa maana tumeshamuweka kwenye kumbukumbu zetu.
Ngoja nielezee maeneo tulio kuwa tunapita:-
Jamani maenoe tuliyokuwa tunapita yalikuwa yananukia vizuri sana, barabra zikuwa za lami safi na hakuna takataka hata moja. Magari yalikuwa yakipita kwa mpangilio. Mauwa mazuri yalikuwa ya mepandwa kwenye kingo na katikati ya barabara. Pembezoni mwa barabara kulikuwa na mambomba tofauti tofauti. Mambomba mengine yaikuwa yakitoa maziwa, na mambomba mengine yakitoa vinywaji vingine.
Nilishindwa kijuzuia ikabidi niulize, hayo mambomba kazi yake ni nini? Misoji akaniambia usiongope tutakueleza kila kitu. Hayo mambomba unayoyaona ni mamboya ya kuwahudumia wakazi wa huku. Unajua sisi tunaokaa juu ya ardhi kuna mambo mengi sana tunashindwa kufanya kutokana na kutaka sifa ambazo hazina hata manufaa. Vilevile ubinafsi umetujaa.
Lakin huku watu wanafanya vitu vyote kwaajili ya jamii. Mimi baada ya miaka 20 nitakuwa raia wa kudumu wa huku Gamboshi. Watu wa huku wanaishi umri wa miaka mingi sana. Unakuta kijana tu ana miaka mia mbili. Huku watu wanaoa na kuolewa. Lakini ili uwe raia wa huku kuna masharti mengi sana unatakiwa kuyafuata.
Kuna mambomba ya maji, mvinyo, maziwa na vinywaji vingine vingi tu vizuri. Ukikubaliwa kuwa mmoja wa raia wanaotazamiwa kuna mafundisho mengi utapitia. Sasa hivi mimi nina mika kumi nakuja huku. Watu wa huku wameniamini sana. Na nipo na marafiki zangu huku. Kuna wakati huwa tunaenda juu ya ardhi kwa pamoja. Huwa wanaiuliza namna mateso tunayoyapata kutokana na joto kali, baridi kari, magonjwa na watu kupigana na kumwaga damu.
Unajua sisi juu ya ardhi huwa tunashindania vitu vingi sana, siasa, pesa na mengine mengi kiasi kwamba tunauana, tunapigana na tunafanya mambo mengi sana ya ajabu.
Lakini huku watu wapo na upendo, walima mazao mazuri, wanafuga wanyama wa kila aina. Kuna mazao na wanyama wengine hawapatikani kabisa kule juu ya ardhi. Nipo na mabo mengi sana ya kukuambia kwa kuwa leo ni siku ya kwanza na umeingia huku utajifunza mengi. Na ukiwa mwepesi wa kuelewa utafanya mambo makubwa.
Watu wa huku wanapenda sana waongozwe na watu waliotoka juu ya ardhi.