Nyanidume
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 2,411
- 1,153
Kwema wadau?. Nimepita maeneo fulani ambapo kuna kijiwe cha pikipiki, nimeukuta ubishani mkubwa wa madereva wa pikipiki. Ubishani huo unamhusu mnyama Tembo, kuna wanaosema Tembo mkubwa akisimama, binadamu anaweza pita uvunguni mwake nae akiwa wima. Kuna wengine wanasema hapana, kwamba Tembo hana ukubwa huo wa kutosh binadamu kupita. Ubishi mwingine unahusu urefu mnyama Twiga, wanasema eti akisimama uvungu wake inaweza pita gari aina ya Landcruiser?, naomba majibu sahihi wadau.