Ukuaji wa elimu chanzo cha uhamiaji mijini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukuaji wa elimu chanzo cha uhamiaji mijini...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MtazamoWangu, Jun 29, 2009.

 1. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimefurahishwa na jambo moja ambalo kidogo linaashiria mwelekeo mzuri katika elimu yetu hapa bongo, miaka mitano iliyopita nakumbuka pale kwenye kitongoji changu ungesikia watoto waliofaulu darasa la saba ni 5% tu ya waliomaliza shule ya msingi.
  Lakini mwaka jana nilipokuwa pale wakati wa matokeo, niliambiwa 85% ya watoto wamefaulu..bravo..thanks to shule za Lowasa...sasa kitongoji kina shule za sekondari 5 wakati kulikuwa hakuna hata moja...sitaki kuamini kwamba watoto wamefaulu ili kwenda kujaza zile shule kwakuwa zipo pale na sio kwa uwezo wao..na pia nataka niamini kwamba ukuaji wa shule uliendana na maandalizi ya walimu bora...sasa pale kijijini kwangu at least kila nyumba ina mtoto anayesoma sekondari...changamoto kubwa sana japo wengine wameshindwa kutokana na ada.
  Nasema ni jambo zuri sana tutapunguza kw kiasi kikubwa sana idadi ya watu wasiojua kusoma na kuongeza idadi ya waliona elimu ya sekondari...
  lakini najiuliza kitu kimoja...kuna mtoto ambaye hataki kufika mpaka chuo kikuu kweli??? tena ukizingatia na siku hizi vyuo ni vingi sana...wote wana nia hiyo hiyo na ndivyo tunavyotakiwa tuwashauri...
  suala lingine linalonitatiza sana, Je tumeandaa mazingira gani kwa hawa watoto wakimaliza elimu zao...wangapi wanaomaliza form 6 au chuo kikuu wanabaki vijijini mwao??? je yapo mazingira ya wao kutumia elimu yao kule wanakotoka??? maana serikali last week imetangaza watanzania wawe wabunifu wa kazi wasiwe wanategemea kazi za kuajiriwa kwa sasa...ndivyo alivyojibu makongoro last week bungeni...Je hiyo elimu wanayopata watoto wetu inajitoshereza mtu kujiajiri au mitaara ni ileile ya mwaka 47 lakni sera ni za 2009...mimi nina mifano mingi ya best student from University kushindwa kudeliver kazini mpaka wenyewe wakaacha kazi maana waliajiriwa kwa upendeleo wa matokeo yao ya flying colors..but they knew nothing on the ground...je hawa wa form 6???
  nikiangalia "maendeleo" ya elimu pale kitongojini kwangu sioni maandalizi yanayoendana kimaendeleo, hakuna hata shughuli moja ya uchumi ambayo inaweza kuja kuacomodate hawa wasomi...na ninachoona hapa ni kwamba tutakuwa tunasomesha watu ili wahamie mijini tu...viwanda mikoani vimekufa..serikali pamoja na kusema KILIMO KWANZA, haionyeshi vitendo kwenye hili.
  1. Je tunazani kama sera ya serikali ni ajira za kubuni, mitaara yetu inajitoshereza??
  2. Je hatuoni kama idadi ya watu/vijana kuhamia mijini itaongezeka kutokana na elimu wanayopata ili kuja kutafuta kazi?? na Je kazi hizo zipo??
  3. Je sasa si wakati serikali ikaaza kufundisha elimu ya ujasiliamali toka shule za sekondari??
  4. kukua kwa ongezeko la watu mijini kunaendana na resources zilizopo??

  Je Unajua population growth ya Dar..???

  MtazamoWangu tu...it is my constitutional right...
   
Loading...