Ukonda ni uchafu?

Mwogahafi

Member
Jun 2, 2014
82
15
Hii tabia ya makonda wa daladala kuwa wachafu (wa mwili na nguo) ndio ishara mojawapo ya kumwonyesha mtu kwamba huyu ni konda? Maana imekuwa kero wengine wanatoa harufu mbaya na imekuwa kawaida kwa makonda wengi kutokuwa wasafi.

Swali, hii kazi ya ukondakta haihitaji usafi? Au ni sehemu ya masharti ya kazi yao?
Mchango wa mawazo mdau kupitia haya maswali
 
Ujue swala hili la makonda kuwa wachafu;ni serious issue.
Hapa inabidi uongozi wa manispaa ya jiji.Ikiwezekana wawafatilie watu hawa.
Manake Id ya Konda ni uchafu.
Kama walilazimishwa kuwa na Sare itashindikanaje kuwabana wawe wasafiiiiii?

Inatakiwa traffic point zote askari akisimamisha Daladala lolote kabla ya Kuulizia fire exitinguisher ipo wapi,anakaguliwa kwanza kama yupo nadhifu.
Nawashangaaga wanapo jiteteaga wapo kazini kama ww/sisi tulivyo kazn.
Kwangu mii huwa naona vichekesho kweli kweli,
mii nipo Supermarket,Sasa nikijitizama mimi na yy anaesema yhupo kazni kama mimi nnako elekea it is amazing.
Mbona makonda wanaoenda mikoani huwa wapo smart hata kama gari haina kiyoyozi.
Tatizo nini kwa hawa City bus,Mbona ma dobi wapo tele jijini.Jmani inakera sana makonda kuwa wachafu.
 
Kwani konda anatofauti gani na:
Mdada anaeenda kukojoa chooni hata maji ya kuosha utupu hana.
 
Hii tabia ya makonda wa daladala kuwa wachafu (wa mwili na nguo) ndio ishara mojawapo ya kumwonyesha mtu kwamba huyu ni konda? Maana imekuwa kero wengine wanatoa harufu mbaya na imekuwa kawaida kwa makonda wengi kutokuwa wasafi.

Swali, hii kazi ya ukondakta haihitaji usafi? Au ni sehemu ya masharti ya kazi yao?
Mchango wa mawazo mdau kupitia haya maswali

ngoja nikuambie kutokana na uzoefu wangu labda mm nahafanya kudogo hiyo nlikua nawasimamia makonda.utakuta unamkaa saa kumi na moja alfajiri konda ana nawa uso tu...na kusukutua mdomo huyo katoka kaenda mzigoni.kurudi saa sita na nusu kalala.kumi na moja ina msubiri....kwa hiyo makonda wanajinyima wenyewe time ya kujifanyia usafi
 
Wa uda tu ndio smart nafkiri swala la ajira liangaliwe upya.

Wasafi ila sijawaona na uniform, pia wanakuwa kama wana cha kubonyeza kengele, ila nashangaa wanagonga debe au mabati ya basi mpaka inakuwa kero, na pia UDA bado wanakero na SUMATRA kama sio serikali, hebu tusubiri...
 
ngoja nikuambie kutokana na uzoefu wangu labda mm nahafanya kudogo hiyo nlikua nawasimamia makonda.utakuta unamkaa saa kumi na moja alfajiri konda ana nawa uso tu...na kusukutua mdomo huyo katoka kaenda mzigoni.kurudi saa sita na nusu kalala.kumi na moja ina msubiri....kwa hiyo makonda wanajinyima wenyewe time ya kujifanyia usafi

Mjini madobi wa kazi gani
 
Ooyooo kwani yule jamaa yuko wapi yule alikuwa ni kiboko yao jina ni mwaibulla na kama yupo bado basi arudiwishiw tena
 
Wapo makonda smart ila wengi wamezidi uchafu. Sidhani kama wanakosa hela ya kununua ata pair za nguo za kazi na sabuni ya kufua. Ingekuwa vizuri sana kama makonda hasa wa Dar wangejirekebisha. Kuwa konda haimaanishi ni kazi ya hali ya chini, ni ofisi kama ofisi nyingine hivyo waiheshimu na sio kuchukulia ni simple na haiitaji kuwa msafi.
 
Kuwekwe sheria kwamba makonda wote wawe wasafi vinginevyo gari ya tajiri wao inapigwa faini kubwa na hata kuzuwiwa kufanya safari. Wengi ni wachafu kupindukia na ni kero kubwa kwa wasafiri walio wengi.
 
Sheria ya kwanza itakayofanya kazi ni ile itakayorasimisha kazi ya konda. Kuwe na muda maalum na shifti za kuingia kazini. Kijana konda asie na mke, mathalan anafanya kazi route ya mbagala posta ama vingunguti (namaanisha route inayomuondoa nyumbani saa tisa alfajiri na kumrudisha kulala saa saba usiku). Huyo anaoga saa ngapi, anafua nguo saa ngapi? Unakuta hana hata overtime ya kuweza kuweka mtu wa kumfanyia usafi pia. Unaweza kufikiria akitoka kaxini amechoka kiasi gani, pengine analala na viatu pia.
 
Nadhani ajira rasmi na masaa maalum ya kazi ndio yanatofautisha makonda wengine na hao wa UDA wanaodaiwa kuwa wasafi.
 
Wapo makonda smart ila wengi wamezidi uchafu. Sidhani kama wanakosa hela ya kununua ata pair za nguo za kazi na sabuni ya kufua. Ingekuwa vizuri sana kama makonda hasa wa Dar wangejirekebisha. Kuwa konda haimaanishi ni kazi ya hali ya chini, ni ofisi kama ofisi nyingine hivyo waiheshimu na sio kuchukulia ni simple na haiitaji kuwa msafi.

Ni kweli Appollo
 
Ooyooo kwani yule jamaa yuko wapi yule alikuwa ni kiboko yao jina ni mwaibulla na kama yupo bado basi arudiwishiw tena

dah jamaa sijui yuko wapi wamemfichiliaa mbali jamaa ndiyo alituwekea ruti hizi
 
Back
Top Bottom