FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
1. Ondoa manaibu mawaziri wote, na manaibu makatibu wakuu wa wizara.
2. Punguza wizara zibaki wizara muhimu tu.
3. Futa mara moja kuanzishwa kwa mikoa mipya na wilaya mpya
4. Hakikisha magari yote ya serikali yanafanya kazi za serikali peke yake, familia za viongozi watumie magari yao ambayo wamepewa kipaumbele cha kununua kwa pungufu ya kodi.
5. Magari yote ya serikali yaengeshwe nje ya ofisi za serikali muda wa kazi unapoisha. Watumishi wote watumie magari yao binafsi kwenda na kurudi nyumbani.
6. Futa safari za nje, ikilazimu viongozi wasafiri kwa daraja la kawaida.
7. Punguza manunuzi ya silaha kwa jwtz.
8. Simamisha wabunge wa viti maalum.
9. Piga mnada wa magari ya kifahari yote yanayotumiwa na viongozi wa serikali, kwa kuanza na ofisi yako.
MAAMUZI MAGUMU KAMA HAYA ANAYAWEZA EDDO LOWASSA PEKEE NDANI YA CCM.