Ukomo wa serikali ya tz kukopa ili isifilisike unakaribia mwisho.....imefahamika..

Watu waliopoenda kupiga kura mwaka jana walifikiria wanaenda kumkomoa nani au kuchagua nini?
Mzee mwanakijiji, hao wananchi waliotulositisha wapo vijijini, wao utakuta wanateseka na njaa tu na hawajui kama serikali inajukumu la kulipa mishahara, bali ukifika muda wao wa kofia ndiyo wanafahamu muda wao wa kuchuma na kuichagua CCM!
 
Kikwete chukua hatua hizi kunusuru taifa:-

1. Ondoa manaibu mawaziri wote, na manaibu makatibu wakuu wa wizara.

2. Punguza wizara zibaki wizara muhimu tu.

3. Futa mara moja kuanzishwa kwa mikoa mipya na wilaya mpya

4. Hakikisha magari yote ya serikali yanafanya kazi za serikali peke yake, familia za viongozi watumie magari yao ambayo wamepewa kipaumbele cha kununua kwa pungufu ya kodi.

5. Magari yote ya serikali yaengeshwe nje ya ofisi za serikali muda wa kazi unapoisha. Watumishi wote watumie magari yao binafsi kwenda na kurudi nyumbani.

6. Futa safari za nje, ikilazimu viongozi wasafiri kwa daraja la kawaida.

7. Punguza manunuzi ya silaha kwa jwtz.

8. Simamisha wabunge wa viti maalum.

9. Piga mnada wa magari ya kifahari yote yanayotumiwa na viongozi wa serikali, kwa kuanza na ofisi yako.

Waitu ebigambo byawe birungi muno!
 
rais ajaye Baada ya jk atapata shida
Atapata shida kubwa sana maana misingi yote ya uchumi imeshavunjwa. Atalazimika kutumia muda mwingi (kama atakuwa jasiri na mwenye akili) kujenga misingi ya uchumi, ajambo ambalo linachukua muda kidogo. Tunaweza tusimuone kama anafaa kwa sababu ya hilo
 
Kimetumika kiasi cha kuruka kusherehekea miaka 50 ya mfu na mafuriko ya siku 2 yametutoa kamasi. Nchi hii ni zaidi ya uijuavyo
 
Sasa na ule Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano 2010-2015, itakuwaje? Ulizinduliwa kwa mbwembwe kule St. Gasper Hotel Dodoma...au wameuahirisha? Na huu wa Mizengo Pinda wa Kilimo Kwanza nao je?
 
Bila kuangalia mambo mengine, BWM alimwachia dr JMK fuko/hazina iliyoshiba, kwa jeuri akateua timu ya kutisha ya mawaziri na kuteua majaji 20 kwa mpigo, haya yalikuwa ni matumizi ya kifujaji yanayofanywa na kiongozi asiyejua namna ya kutafuta na kutumia pesa. BWM alipunguza kukopa ndania na alilijitahidi kulipa wazabuni wa ndani pia.

3Dr JMK baada ya kufuja na kuubinafsisha urais (haamini kuwa urais ni taasisi-rejea hotuba yake ya kuwaapisha mawaziri awamu ya pili), ameanza kukopa ndani kama Mtz anayehiriki michezo ya upatu, wachumi wanajua madhara ya serikali kukopa benki za kibiashara zilizoko ndani ya nchi, tena anakopa si kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Kupunguza matumizi yake (kusafiri sana, baraza la mawaziri, linaweza kuwa ni suluhisho sahihi lakini kikubwa ni kujitambua kuwa yeye ni rais wa JMT na si rais wa mpenda sifa zisizo tija kwa umma
 
Watu waliopoenda kupiga kura mwaka jana walifikiria wanaenda kumkomoa nani au kuchagua nini?

% kubwa ya hao wapiga kura wajua nini maana ya anguko la kiuchumi? wape elimu ya kutosha kabla ya kuwaomba kura yako! na kama hilo haliwezekani basi ni heri wajionee hilo anguko ili wafunguke na kutorudia makosa.
 
Hakuna ubishi katika hili:-

Kwa staili hii ya utawala tulionao, ya kukopa fedha za matumizi ndani ya nchi.

Mwaka ujao 2012, ni lazima salamu ya Ulale mahali pema peponi, ianze kupokelewa na ofisi ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi.

Lawama zote ziende NEC kwa ku2tumbukiza kwenye janga la kitaifa.
Lawama pia zirudi kwa watanzania kwa kukubali upumbavu wa NEC. Kwani ilishindikana nini kubaini ukweli wa wizi wa NEC??Kumbukumbu si zipo!!kwanini hatuchukui hatua na tunaishia kuongeaongea tu???Mi nadhan hata sisi watanzania ni LEGELEGE PIA
 
% kubwa ya hao wapiga kura wajua nini maana ya anguko la kiuchumi? wape elimu ya kutosha kabla ya kuwaomba kura yako! na kama hilo haliwezekani basi ni heri wajionee hilo anguko ili wafunguke na kutorudia makosa.
Kiongozi sio kwamba wataumia wasiojua maana tu, haya matatizo kwa ujumla wake yanatucost watanzania wote tena hasa wale wanaojua maana na waliokataa kurudisha utawala wa kibabaishaji. Kwani katika mijadala ya JF unaona waliomchagua JK wanpata hata shida kufkiria na kuchangia mada kama hizi??Mimi nadhani kuna haja ya kufikiria zaidi ya hapa na kuangalia nini cha kufanya katika chaguzi zijazo ili utumbo huu na NEC kutuwekea mtu wao ukome, tukicheza sebene na mwanaNEC mmoja atakayetuingiza taabuni nadhan wataacha kutufanyia ushenzi.

Anyway! tupambane tume ya uchaguzi iwe huru 100%, Tuhakikishe elimu ya uraia inawafikia wananchi wa vijijini ambao CCM inajivunia kuwa ndiyo Ngome yao. Haya yafanywe kuanzia sasa na sisi vijana. Ili ukifika wakati wa uchaguzi, moto uanze kuibabua CCM kutokea vijijini kurudi mjini. Hima vijana isaidieni nchi, rudini vijijin mkashike majimbo na kata za udiwani huko. Hii ndo namna pekee ya kuimwaga serikali hii legelege, yaani haiingii akilini, kwa ulegelege huu serikali hii inashindaje???Hapa ni kwamba serikali imeshajua kuwa wananchi wake ni legelege zaidi.
 
Naiogopa nchi yangu TZ sasa,
Mkuu wa Nchi tafadhali punguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali yako,
Zuia utumiaji wa magari ya kifahari na ikwezekana piga mnada fasta,
Punguza kabisa baraza la mawaziri, na Ondoa manaibu mawaziri na manaibu makatibu wakuu
Mh. Dr. Jakaya Kikwete, nakuomba hata kwa hili wasikilize na fuata ushauri wa wanaJF, japo mara moja tu.
Ahsante
 
Kikwete chukua hatua hizi kunusuru taifa:-

1. Ondoa manaibu mawaziri wote, na manaibu makatibu wakuu wa wizara.

2. Punguza wizara zibaki wizara muhimu tu.

3. Futa mara moja kuanzishwa kwa mikoa mipya na wilaya mpya

4. Hakikisha magari yote ya serikali yanafanya kazi za serikali peke yake, familia za viongozi watumie magari yao ambayo wamepewa kipaumbele cha kununua kwa pungufu ya kodi.

5. Magari yote ya serikali yaengeshwe nje ya ofisi za serikali muda wa kazi unapoisha. Watumishi wote watumie magari yao binafsi kwenda na kurudi nyumbani.

6. Futa safari za nje, ikilazimu viongozi wasafiri kwa daraja la kawaida.

7. Punguza manunuzi ya silaha kwa jwtz.

8. Simamisha wabunge wa viti maalum.

9. Piga mnada wa magari ya kifahari yote yanayotumiwa na viongozi wa serikali, kwa kuanza na ofisi yako.

Mkuu hizi ni ndoto
Kwa serekali ya huyu jamaa hawezi kufanya na hana ubavu wa kufanya hata moja la hayo hapo juu
yahitaji mtu jasiri kuweza kuchukua maamuzi kama hayo na sio huyu jamaa yetu
 
CCM....(A.K.A)..... NA WATAWALA WAKE ............sawa na GENGE LA MBWEHA .........wanao chunga kondoo ........MBWEHA hawa wasikiapo njaa hawana huruma na KONDOO wanao wachunga 89% ya watanzania nimasikini!!...........Usually
when people are sad they don't do anything they just CRY over their
condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)

LOL

Mpeni nchi Lowassa mambo yatakua safi. Vumilieni kidogo jamani 2015 sio mbali.
 
Back
Top Bottom