Ukomo wa Rais na Mawaziri kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Tanzania

Mar 2, 2012
57
17
Pamekuwa na minong'ono na maneno toka kila kona kwanini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete havunji baraza la Mawaziri huku wengi wa Mawaziri hao wakiwa busy kutafuta nafasi za uwakilishi za kurudi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kampeni zinazoendelea.

Tupite pamoja

Katiba ya Tanzania - Ibara ya 57.

Ibara ndogo ya (1),

Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo".

Fasiri yake "Mara baada ya Rais kuchaguliwa na yeye kumteua Waziri Mkuu na kisha kushirikiana na Waziri Mkuu kuunda Baraza la Mawaziri na manaibu wao".


Ibara ndogo ya (2),

Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:

(a). Endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki dunia;

(b) ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;

(c). Ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini mwenye madaraka hayo;

(d) iwapo atachaguliwa kuwa Spika;

(e). Iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;

(f). Ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo;

(g). Iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ibara ndogo ya pili (2) kipengele (b) kinaweza kisieleweke kwa haraka lakini natumai kimejitosheleza.

Kama kuna sehemu hapajaeleweka,naomba uulize na patatolewa maelezo tafadhali.

SERIKALI YAFAFANUA UKOMO WA MADARAKA YA RAIS NA MAWAZIRI.

Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu ukomo wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na mwisho wa uhai wa Baraza la Mawaziri kwa kadri Tanzania inavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu unaofanyika jumapili,oktoba 25,mwaka huu, 2015.

Taarifa imetolewa jioni ya leo jumatano oktoba 21,2015,ikulu,Dar es salaam na ofisi ya katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Yohana Sifue imesema kuwa serikali imetoa ufafanuzi huo kuwasaidia wananchi kuelewa maelekezo na matakwa ya katiba na sheria kuhusu ukomo wa madaraka wa Rais na mwisho wa Baraza la Mawaziri kufuatila mijadala ya Karibu katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Taarifa hiyo imekariri ibara ya 42(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inasema kwamba ukiacha sababu nyingine,mtu anaye chaguliwa kuwa Rais atashika madaraka ya kiti cha Urais hadi Rais mteule atakapoapishwa.

Ibara hiyo ya 42(3) inasema:"Mtu anayechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-(a) siku ambako mtu anayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo"

Taarifa hiyo inasema :Hivyo kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,Rais ataendelea kuwa Rais,akiwa na madaraka na mamlaka yote na kamili yanayo ambatana na nafasi hiyo,hadi Rais mteule atakapo kula kiapo cha Urais.Hivyo ni vyema wananchi waelewe kuwa haitatokea wakati wowote ambapo hakuna Rais na Amiri Jeahi Mkuu mwenye Mamlaka kamili na aliyetaari kutekeleza mamlaka hayo.Lengo ni kuhakikisha kuwa haitokei wakati wowote nchi yetu ikakosa Rais na Amiri jeshi Mkuu"

Imesisitiza taarifa hiyo: "Madaraka na mamlaka ya Rais yapi na hayapungui kwa namna yoyote ile, hata baada ya uchaguzi mkuu,mpaka Rais mpya atakapo apishwa".

Kuhusu ukomo wa Baraza la mawaziri taarifa imefafanua kuwa kwa mujibu wa ibara ya 57(2) ya katiba,Waziri na Naibu Waziri ataendelea kushikilia mamlaka ya nafasi yake hadi,ukiacha sababu nyingine Rais mteule atakapoapishwa.

Ibara hiyo ya 57(2) inatamka: "Kiti cha Waziri au Naibu waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais,basi mara tu kabla ya rais mteule hajashika madaraka hayo."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wanaendelea kushikilia nafadi zao,wakiwa na madaraka na mamlaka yanayo ambatana na Nyadhifa zao hadi mara tu kabla ya Rais Mteule hajashika madaraka.

Imemalizia taarifa hiyo: "Naomba vyombo vya habari,vyenye majukumu ya kuelimisha jamii,kuwaelewesha kuhusu utaratibu huu wa kubadilishana madaraka kati ya awamu moja ya uongozi wa nchi na nyingine. MMadaraka na mamlaka ya Rais yapo na hayapungui kwa namna yoyote ile,hata baada ya uchaguzi mkuu mpaka Rais mteule atakapo apishwa. "

 
Na hao wanaogombea je..? Hawakutakiwa kuwa wameachia uwaziri na ubunge na vyeo vyote kwenye utumishi wa uma?
 
B) na F) vinajicontradict kipindi hiki cha uchaguzi. Bunge si lilishavunjwa?

"(b). Ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge" fasiri yake ni kwamba kama kutakuwa na jambo lingine lolote litakalopelekea Waziri kukosa sifa ya kuwa katika uwakilishi kama vile kusimamishwa na kuvuliwa uanachama ambao moja kwa moja humpelekea kupoteza sifa ya kuwa Mbunge,nafasi yake ya uwaziri itakoma kuanzia hapo au ikitokea kifo. Bunge likivunjwa kwa fasiri hiyo,Waziri bado ataendelea kukaimu madaraka yake.

"(f). Ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo" fasiri yake ni kwamba mara baada ya Rais mpya kuchaguliwa na muda kabla ya kuanza kuwa na mandatory kama Rais wa Nchi.
 
Hujaeleweka. Hivyo Baraza la Mawaziri halijavunjwa su limevunjwa? Na Bunge limevunjwa au halijavunjwa? Hivyo wabunge mawaziri wako kwenye campaign huku wanapokea mishahara ya Ubunge na uwaziri!? Tutolee kifungu cha sheria utufafanulie haya na pia campaign zimetangazwa kuanza na wabunge na mawaziri bado wako ktk nyadhifa zao sheria inasemaje!?
 
Siasa za Ukawa za hovyo sana kuwahi kutokea ..mara Mwamunyange mara sijui mawaziri, yaani Fujo tu

Halafu eti mtu anakuja na thread eti anaipa serikali siku 7 iwe imempa majibu juu ya alipo Mkuu wa majeshi. Yaani wanategemea mkuu wa majeshi avunje ratiba zake za msingi ajibu thread za majukwaani?
 
Hii sheria kuna kitu inakilinda na au haijitoshelezi na ina mapungufu mengi. Sikumbuki vizuri kifungu cha katiba lakini kipo na kinaelekeza kuwa waziri kabla ya uteuzi wake ni lazima awe mbunge. Rais alishavunja bunge toka Augost, sasa mawaziri waliopo wanatokana na bunge lipi? Na mawaziri kugombea au kutetea nafasi zao bila kujiuzulu kwanza nafasi za awali sheria haijakiukwa? Anaweza kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka?
 
Nyie watu baraza la mawaziri litavunjwa muda ambao Jk atakuwa anataka kuelekea Uwanja wa taifa kukabidhi madaraka,

Hayo ndio majumuisho ya tafsiri ya vifungu vya katiba kwa mazingira ya sasa
 
Asante kwa kutuletea hivi vifungu vya katiba,
Hapo kifungu kilichowazi ni kifungu no 2 kipengele (f) ndicho haswaa kinachomlinda mh JK,JK hatolivunja bunge lakini bunge litavunjika automatic mara tu magufuli atakapotangazwa mshindi na katiba itakua baijavunjwa.
 
Siasa za Ukawa za hovyo sana kuwahi kutokea ..mara Mwamunyange mara sijui mawaziri, yaani Fujo tu

Yaani siasa za UKAWA ni full vurumai. Bora liende na hasa huyu mkuu wao mr.master mind anacheza na akili za watz wote hata wale waliomzidi elimu
 
Back
Top Bottom