Ukombozi wa mwanadamu atauleta yeye mwenyewe, wengine waweza kumsaidia kuufikia mapema

Landson Tz

Senior Member
May 8, 2011
196
250
Jamii yetu ya Tanzania imejazwa matumaini hewa yanayobuniwa na wanasiasa ili kuwaghilibu na kujinyakulia madaraka kwa gharama nafuu. Kuwafanya watanzania waweke matumaini ya uongo juu yao (wanasiasa) wanajiandalia dhambi mbaya sana kwa mwenyezi Mungu. Ila nataka watanzania wajue kuwa shida, unyonge, umaskini na matatizo mengine yaliyo juu yao hayataondolewa na mwingine yeyote awaye bali wao wenyewe.

Itakuwa ni bora kwa watawala kuwaeleza ukweli na kuwasaidia katika kutatua matatizo hayo na si kuwaaminisha kuwa wao ndio suluhisho la matatizo yao. Kusiwepo na mtu anayejipachika jina la mtetezi wa wanyonge kwa maneno ya mdomoni bali vitendo.

Pamoja na ahadi nzuri za kila uchaguzi mkuu kwa watanzia wote, bado watanzania walio wengi wameendelea kuogelea katika dimbwi la umaskini huku wachache wakineemeka.

Wadau mnakumbuka yule mwelekeza njia (Azimio la Arusha) aliye kuwa tumaini la wengi alivyo potezwa mwelekeo (Azimio la Zanzibar) na kuelekezwa kusikojulikana huku mwelekezaji mpya (ULIBELERALI MAMBO LEO) akijulikana kwa wachache ambao sasa ndio matajiri wakubwa ndani ya nchi iliyojaa maskini wa kutupwa. Maskini hawa ndio waliopotea njia wakidhani na kuaminishwa kuwa mwelekezaji hajapotea njia (Ujamaa na kujitegemea).

Atakuwa mpumbavua ambaye atadhani kuwa mapinduzi katika maisha ya ya mwanadamu huisha. Mapambano ya binadamu dhidi ya mazingira yanayomzunguka hudumu ila kwa sababu mbalimbali yanaweza kusimamishwa au kucheleweshwa. Ila ni hatari kujaribu kuyasimamisha.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Ni bora tukajitathmini upya kama taifa, ili dhana ya mapinduzi iendelee ndani ya mioyo ya watanzania wote hili atimaye tuweze kuendeleza mapambano dhidi ya maadui wetu (umaskini, maradhi na ujinga) hadi tutakapo tungaza ushindi kwa pamoja.

Nawasilisha

Hawa walipata kusema:

"Every man gotta right to decide his own destiny, And in this judgement there is no partiality.

So arm in arms, with arms, we'll fight this little struggle, 'Cause that's the only way we can overcome our little trouble" by Bob Marley

Emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds.

By Bob Marley

I am not a liberator. Liberators do not exist. The people liberate themselves.

Che Guevara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom