Ukombombozi wa wanywaji pombe umeribia.

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,285
9,922
KILA mwaka Serikali
imekuwa ikiongeza kodi
kwenye vinywaji, hususan
pombe ili kukidhi bajeti
ya mapato na matumizi
yake. Hali hiyo
husababisha bei ya
pombe kupanda karibu kila mwaka na
kuwaongezea mzigo wanywaji kwa kulazimika
kuzama zaidi kwenye mifuko yao ili kugharimia
kinywaji hicho.Kwa miaka yote hiyo wanywaji
wamekuwa wakilia kimoyomoyo bila ya kuwa na
mahali pa kupaza sauti zao, hali inayoifanya
Serikali ione kinywaji ni mahali kukimbilia
kupata fedha.
Kulingana na taarifa za viwanda vya bia, bei ya
kinywaji hicho huenda ikapanda kwa karibu
asilimia 25, kuanzia mwezi huu, jambo ambalo
limewafanya wanywaji kusema; “Hapana!
Haiwezekani.”
Kwa sababu hiyo, wanywaji tayari wameunda
jukwaa lao la kupaza sauti zao na tayari
wameweka mikakakati ya kudai haki
zao.Chombo hicho wamekipa jina “Chama cha
Wanywa Pombe kwa Staha Tanzania (TRBDA)”
na tayari kimesajiliwa na sasa kipo katika
harakati za mikakati ya kukabiliana na Serikali.
“Sisi tunachotaka ni bei ya bia kushuka au
kubakia palepale (Sh1,700). Hili ni suala nyeti
na hatari kuliko watu wanavyolifikiria sasa,”
anasema Rais wa TRBDA, Gasisi Mahuti.
Anaongeza; “Chama kimesajiliwa Mei 22
mwaka huu, hivyo tuna nguvu ya kisheria
kufanya kazi na kutetea maslahi ya wanachama
wetu.
“Tunaona kero kila mwaka, kila Bajeti ya Serikali
wanakuja na mikakati ya kuongeza kodi kwenye
pombe.”
Mahuti anasema kwa miaka mingi mzigo huo
wa ongezoko la bei ya bia ambayo ndiyo
inayotumiwa na watu wengi, imekuwa
ikiongezeka, lakini safari hii, hali ni mbaya
zaidi.
Mzigo huo kwa wanywaji anasema
umechangiwa na mambo mawili makubwa
ambayo ni kuongezeka kwa gharama za maisha
na kiwango kikubwa cha kodi kwa mwaka huu
wa fedha 2012/13 ulioanza leo.
“Hiyo bei itasababisha wanywaji wengi kuhama
kwenye kinywaji salama na kwenda kwenye
kinywaji hatarishi na haramu,” analalamika
Mahuti.
Anavitaja vinywaji hatarishi kuwa ni baadhi ya
pombe za kienyeji ambazo ni hatari kwa afya
kwa sababu nyingi zinaandaliwa kwenye
mazingira machafu na hakuna udhibiti. Pombe
haramu anaitaja kuwa ni gongo.
Madhara ya kupandishwa bei ya pombe,
anasema siyo hayo tu bali yapo ya kuathiri
uchumi na maenedeleo ya watu.
“Nenda baa utaona. Siku hizi wanywaji wengi
hawakai pamoja kila mmoja akiingia baa
anaagiza bia yake tofauti na hapo awali mtu
anazungusha ‘raundi’.
“Hili ni tatizo maana watu wengi sasa ‘hawa-
socialize’. Hawakai pamoja baa kubadilishana
mawazo, kupeana mbinu za maisha. Hii ni
hatari,” analalamika Mahuti.
Vita na Serikali
Mahuta anasema athari za kupanda kwa bei ya
bia ni nyingi na wanatarajia kuziwasilisha
serikalini kutaka zipunguzwe.
Kuhusu namna watakavyowasilisha taarifa hizo,
Mahuti anasema kwa kuanza watawasiliana na
ofisi ya Waziri wa Fedha na Uchumi na hata
likishindikana watabisha hodi ofisi ya Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda.
Pamoja na malalamiko hayo, anasema
wamekusudia kuishawishi Serikali kubuni
vyanzo vingine vya fedha ambavyo imekuwa
ikishindwa kuvitumia kutokana na uzembe wa
watendaji wake.
Baadhi ya sekta nchini zinapopeleka madai
yake serikalini hugoma ili kutoa shinikizo.
Kuhusu wana mpango wa kugoma endapo
serikali itakaidi kushusha kodi.
Kiiongozi huyo anakiri kuwa wanywaji wakigoma
Serikali inaweza ikatikisika kwa sababu
wanachangia pato kubwa serikalini.“Lakini sisi
hatutaki kufikia huko (kugoma) au kuandamana.
Sisi tunaenda kuzungumza tu hatuna haja ya
kufanya fujo.
“Sisi wanywa pombe kwa staha tunatazamia
busara zaidi zitatumika kuliko kulazimishana na
kusababisha madhara,” anasema.Nimemuuliza,
iwapo busara zitashindikana watachukua hatua
gani, anasema: “Kama nilivyokuambia awali
wanywa pombe walikuwa hawana jukwaa la
kusemea. Sasa wanalo.
“Tunaamini kwamba Serikali ilikuwa inaongeza
kodi kwa kutofahamu madhara yake ama kwa
kutokuwa na vyanzo vingine. Sisi tunaenda
kuwaambia madhara yake na tunaenda
kuwaeleza njia nyingine za mapato. Suala la
kugoma, kuandamana; halipo.”
Anasema kwa miaka mingi wanywaji ndio
wamekuwa wakichangia pato la Serikali na
kufanikisha utaji wa huduma mbalimbali kwa
jamii kama vile elimu, afya na maji.
Ingawa wanywaji wamekuwa wakichangia hayo
yote, anasema wao si wote wenye fedha sana
bali wengi wao ni watu wa kipato cha kawaida.
“Mtu haindi kunywa pombe kwa sababu ana
pesa nyingi. La, hasha! Ni sehemu tu ya
kubadilishana mawazo na kupata maarifa. Hii ni
njia ya kupashana habari,” anasema.
Majuku mengine TRBDA
Mahuti anasema jukumu la kuanzishwa kwa
TRBDA siyo tu kutetea maslahi ya wateja katika
suala la bei tu bali mikakati mingene ya kiafya,
kijamii na kielimu.
Anasema Septemba Mosi mwaka huu kwa mara
ya kwanza hapa nchini chama hicho
kitaadhimisha tamasha kubwa la maadhimisho
ya siku ya wanywa pombe duniani.
Anasema siku hiyo imekuwa ikisheherekewa
duniani, lakini hapa nchini imekuwa haijulikani
kwa sababu hakuna chombo cha uhamasishaji
wa maadhimsiho.
 
Duuuh, inaelekea habari uliiandaa vizuri ukiwa hujawa keroro, baada ya kupiga ulabu ukatafuta title na ku-post.
" ukombombozi" "wanyaji" "umeribia"
Pombe nouma!:crazy::crazy:
 
kutegemea kodi ya pombe! Nchi haiwezi kupiga hatua. Maana siyo mpango wa Mungu.achane kunywa pombe muone kama mtakufa.
 
Kesho baada ya kuamka naheng'ova kapige supu,
usizimue,
ukishakuwa sober,
njoo rekebisha title,
au omba mods wakurekebishie title fresh.
 
TRBDA'
nimependa.
kirefu chake nini vile?
hiki ndo chama.
 
&then kupeana mawazo bar! You must be kidding. Let us be a bit more serious. Iv wajapan au wachina mawazo ya maendeleo wanayapata bar
 
&kuungana itakuwa ngumu maana kwa wengine ndo zaman ikiitwa mtama kwa watoto! Si ndo imekuwa ya wachache?achana uchafu huo. Havakupeleka popote
 
Salushan ni homemade beer. Piga beer zako nyumbani tax free halafu unamalizia bar na hizo over taxed beer.
 
kweli mkuu suala la kugoma kunywa haliwezekani kwani wengine tusipostua kidogo tunahisi matumbo yanatetemeka... dawa ni kupanga siku ya maandamano tunaanzia pale sinza kijiweni mpaka magogoni tukiwa tushatupia kama 6 hivi kila kichwa halafu moja mononi tunaomba tukutane na mkuu wa kaya
 
siku hizi ni bia mbili tu mapeema nyumbani.CUT SPENDING!!! TRA itakula kwenu.
 
Salushan ni homemade beer. Piga beer zako nyumbani tax free halafu unamalizia bar na hizo over taxed beer.

kweli mkuu suala la kugoma kunywa haliwezekani kwani wengine tusipostua kidogo tunahisi matumbo yanatetemeka... dawa ni kupanga siku ya maandamano tunaanzia pale sinza kijiweni mpaka magogoni tukiwa tushatupia kama 6 hivi kila kichwa halafu moja mononi tunaomba tukutane na mkuu wa kaya

siku hizi ni bia mbili tu mapeema nyumbani.CUT SPENDING!!! TRA itakula kwenu.

wazo zuri

Acha kutuzingu wachina wanatuhusu nini? hapa tunazungumzia Tz.





Yeees Hommies, nawaona hapo na ninatoa big up kwa aliyekuja na wazo hilo maana tumeonewa kiasi cha kutosha,na pamoja na mchango wetu kwa Taifa bado tumepuuzwa kiasi cha kutosha kwa kuitwa walevi na wakati mwingine hata kunyanyaswa makazini kisa nini huwa muhudhuriaji mzuri pale chini ya muti,sasa tunasema basi na ikibidi hata kugoma tugome tu tuone wahudumu wote na wachoma kitimoto wataajiriwa na nani..
 
Naomba mwongozo wa kufungua ofisi ndogo ya chama huku niliko... Halafu mi nacheza game zote, taifa mpaka ndondo, ila kwa staha.
 
Back
Top Bottom