Ukoloni mamboleo

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
597
1,000
Zimbabwe na Zanzibar kihistoria sote tumepata uhuru kutoka kwa wakoloni miaka tofauti,sisi tulipata mezani kwanza tarehe 10 december 1963,halafu tukatumia mapanga kufanya mapinduzi 1964 january 12,Zimbabwe walipata uhuru wao tarehe 18 april 1980,kwa maana hii sote inasemekana ni watu na mataifa huru hapa duniani kama yalivyo mataifa mengine yote yaliyojikomboa iwe kwa nguvu au hiari.

Matatizo ya Zimbabwe na Zanzibar yanafanana sana sote bado tunatawalana,tumepata uhuru kwa gharama kubwa sana na kumwaga damu nyingi, yenye hatia na isiyo na hatia,tulidhani kuwaondoa waliotutawala wakati huo ndio wakoloni, wanyonyaji,na tatizo letu pekee,laiti tungelijua kuwa tatizo jingine ni sisi wenyewe, basi wengi tusingekubali kupindua au kudai uhuru, ili tuje kutawalana kwa mitutu wenyewe kwa wenyewe,nani anadhani ukiuliwa na ndugu yako ni bora zaidi, kuliko kuuwawa na mtu asie kujua?

Nchi za kiafirika/kiafiriti mimi hupenda kulitumia hilo neno la pili,mara nyingi tumejenga utamaduni wa kuwatupia lawama wakoloni waliozitawala nchi zetu kwa karne nyingi zilizopita,kama kwamba ni sisi tu tuliofadhiliwa kwa karima hiyo,hakuna bara duniani ambalo halikukoloniwa na mbabe wa enzi hizo,Marekani alitawaliwa na Muingereza, na yeye ilimlazimu afanye mapinduzi,Mmarekani na yeye aliwapindua Wahindi wekundu, ambao ndio wenye asili na nchi hiyo,Mfaransa na yeye hakuwa nyuma pamoja na muhispania wote wamepigana kutafuta kukoni sehemu ya marekani na nchi nyingine, na wao wapate japo vipande ili wazikoloni,hii huitwa historia imeshapita wala haitorudi,pia haijayazuwia mataifa haya kuendelea kwa kuwa walitawala,kutawaliwa au kwa kuwa wana historia ya kutisha.

Sisi katika nchi zetu za kiafiriti,tumejikita sana katika kuwalaumu wakoloni mambo juzi,tumejitwika uhayawani na kuyafumbia macho matatizo ya “ukoloni mambo leo”ambayo lazima ni kiri kuwa, niliposomeshwa shuleni somo hili,nilikuwa naumwa kichwa siku zote, kwa kuwa sikuwa na uhakika, ufahamu/ nauelewa ukoloni mambo leo ni kitu gani?mwalimu wetu alijitahidi kutuelimisha, kuwa ukoloni mambo leo utatokana na wale wale wakoloni tuliowatimua,watarudi kwa milango ya nyuma na sababu tofauti, ili wazikoroge akili zetu na tuwakumbatie upya, hapo ndio tutakapodhulumiwa zaidi, tena safari hii kiuchumi zaidi hiyo ndio itakuwa bakora mpya.

Unapokuwa kijana kiumri bado mawazo huwa hayajapanuka vya kutosha,unaweza kupakia shehena yoyote ya mawazo safi na yenye maji taka katika kichwa chako kichanga,huu huwa ndio wakati muwafaka wa kuvijaza vichwa hivi visivyo na hatia,kasumba yoyote ya kisiasa na ikakaa au kudakwa kama sumaku,iwe Mapinduzi,Muungano au Ukoloni.

Zimbawe na Zanzibar hazitawaliwi tena na Muingereza wala Muarabu, hivi sasa zinatawaliwa na ‘MUAFIRITI/MUAFIRIKA’mwenyewe,wananchi wa nchi hizi mbili hawako huru hata dakika moja,japokuwa viongozi wao hulazimika kuwakumbusha siku zote, kuwa wao ni watu huru, na tarehe walizopata uhuru au kujikomboa wanazijua,inawawia vigumu wananchi sisi kuzikumbuka tarehe hizo, kwa sababu tarehe zilizo salia, yaani kila siku inayokwenda kwa Mola,sisi tumo katika ukoloni huu mpya wa mambo leo,tangu tupindue na kupewa uhuru bado hatujajitawala kwa ridhaa yetu,tunatawaliwa na wenzetu sasa kwa nini iwe salama,tukae kimya na kufurahia mauwaji ya wenyewe kwa wenyewe.

Tukithubutu kusema tunaambiwa sisi sio wazalendo, hatuna fadhila,au hatupendi muungano,pengine tutaambiwa hatuyaabudu mapinduzi au tunataka Waarabu warudi,kwani huyu muafiriti kachukua likizo lini hata muarabu apate nafasi ya kurudi?mimi naipenda Zimbabwe kama ninavyoipenda Zanzibar,na ni lazima nizionee uchungu nchi mbili hizi, kwa sababu sioni sababu hata moja ya watu tunaojitapa weusi,weusi wetu ndio tuutumie kuwaadhibu wengine, tunaitumia rangi hii maalum kuzibagua rangi nyingine, na hapo hapo tunawatawala raia wetu kwa kutumia weusi wetu, lakini bado tunawanyooshea vidole wakoloni weupe bila soni hata kama hawapo.

Siasa sio mchezo mchafu kama inavyoaminishwa hapa kwetu,inategemea na usafi au uchafu wa muhusika,Zanzibar walio wengi hawana sauti na wala hawatoipata ikiwa watalitegemea sanduku la kura kuwakomboa,lisilo budi ni lazima lifanywe ikiwa tumechoka na ukoloni wa mambo yoyote,zimetungwa sheria zinaitwa za uchochezi ili kuwa ziba midomo kina mzeekondo na wenziwe kina papax,sasa kama kweli sisi ni watu tuliojikomboa kwa kupindua na kumwaga damu ili iweje?hatukupindua ili tuje kuzuwiana kusema,uhuru wa kusema ni haki ya kila kiumbe alie huru,haki hii ni moja ya nguzo muhimu katika kulinda na kutetea haki za binaadamu,lakini Zimbawe na Zanzibar ni marufuku, na tunatakiwa tujihadhari na mawazo au tutakayosema, kwa sababu viongozi wa kiafiriti, muhimu wawaze, watawale na waseme wao tu.

Huu ndio ukoloni mambo leo,hakuna mwengine.

Nawatakia swaumu na mwezi mwema/njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom