mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Ukoloni mamboleo (neo-colonialism) ni nini?
Ukoloni mamboleo unaeleweka kwa mapana kama mwendelezo wa siasa ya kibepari ambayo inaziwezesha mamlaka za kibepari (baadhi ya mataifa yaliyoendelea na mashirika yake) kutawala mataifa maskini kupitia shughuli za kibepari km kuwekeza mitaji kwenye maeneo watakayofaidika badala ya njia ya utawala wa moja kwa moja.
Je, Tanzania bado iko kwenye ukoloni mamboleo na kama ipo ni jinsi gani taifa linaweza kujikomboa? Je, vyama vya siasa vina sera gani kuikomboa nchi kwenye ukoloni mamboleo?
Lissu, mgombea Urais wa tikiti ya CHADEMA, ameulizwa hilo swali, akipewa ridhaa ya kuongoza nchi hii, atachukua hatua gani kuikomboa kwenye ukoloni mamboleo? Akijibu swali hilo amesikika akisema, nanukuu: ni maneno ya wanaofuata mfumo wa kijamaa akina Nyerere na Nkurumah. ... katika uchumi wa dunia ya leo ambao ni interconnected (kufungamana) ni upuuzi, ujinga na upumbavu kuzungumzia ukoloni mamboleo. ... yaani kuwekeza mitaji yao kwenye uchumi wetu, ndio ukoloni maendeleo? ... Je, nchi yetu inaweza kuendelea kiuchumi bila uwekezaji huo?
Majibu ya swali hilo yako kwenye YouTube hii hapa. Ni majibbu yanayofikirisha kama Lissu, mgombea Urais, anajua siasa za kiuchumi au hajui kuwa hajui?
Je, anajua kuwa ukoloni mamboleo ni nchi kutawaliwa kiuchumi na mataifa ya nje? Je, anajua kuwa matokeo ya ukoloni mamboleo ni pale mitaji ya kigeni kutumika kwa ajili ya unyonyaji badala ya maendeleo ya nchi maskini duniani? Je, anatambua kuwa uwekezaji, chini ya ukoloni mamboleo huongeza, badala ya kupunguza, pengo kati ya nchi tajiri na maskini duniani?
Yawezekana ni tafsiri ya Sera ya Uchumi iliyoainishwa kwenye Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu, 2020. Kwamba Chadema kimejipanga kuutafsiri ukuaji wa uchumi kwa vitendo ili kuwepo kwa mabadiliko chanya katika maisha ya kila Mtanzania. Hili litawezekana kwa kufumua mfumo wa sasa wa uchumi wa kijamaa ambao umeshindwa kuboresha hali ya maisha ya Watanzania, na kuanzisha mfumo wa soko jamii ambao unalenga kufungua fursa kwa kila mtu kutumia vipaji vyake katika kuzalisha na kumiliki mali. Mfumo huu mpya wa uchumi wa soko utaambatana na kujenga, kuimarisha na kusimamia uchumi wa kitanzania kwa kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na hisa na wawekezaji wenye mitaji mikubwa.
Kwa upande wake, katika Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu 2020, CCM inatambua umuhimu wa kujenga uchumi wa kitaifa ili kuhakikisha kwamba Watanzania ndio wanufaika wakuu wa uchumi na maliasili za nchi na ndiyo wenye kauli juu ya namna uchumi unavyoendeshwa. Kwa muktadha huo CCM itaelekeza Serikali kuendelea na juhudi za kuifanya Tanzania kuwa nchi inayojitegemea kiuchumi pamoja na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na nchi nyingine. Juhudi maalum zitaelekezwa kuhakikisha rasilimali za asili za nchi hii, hasa ardhi, madini, gesi asilia, mafuta, maji na misitu zinanufaisha wananchi na Taifa kikamilifu.
Tukikubaliana na dhana ya ukoloni mamboleo, kwa msingi kwamba nchi maskini bado hazijajikomboa kiuchumi, ni dhahiri kuwa Sera ya kuanza na maendeleo ya vitu kutachochea kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na taifa. Km kuwepo kwa miundombinu imara ya usafirishaji kutamwezesha mzalishaji mali (mwenye kiwanda, mkulima, mvuvi, mchimbaji madini, nk) kuuza bidhaa zake nje ya eneo lake kwani ukubwa wa soko unaongezeka.