Uko wapi uhuru wa bunge la tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uko wapi uhuru wa bunge la tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by magiri, Apr 16, 2011.

 1. m

  magiri Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama ilivyo dhana ya utawala bora,bunge linapaswa kuwa chombo huru kwa maana ya kazi zake na hata kalenda ya mambo yake.kinachonishangaza bunge letu ni kama serikali tu. hivi kwa nini waziri mkuu anapotoa hotuba ya serikali kabla ya kuahirishwa bunge yeye ndiye anatangaza tarehe ya kikao kingine kinachokuja? hivi yeye ndo kiongozi wa bunge? ni ajabu maana spika huwa anakuja kutangaza baadae as a rubber stamp. kwani bunge ni excutive? maana waziri mkuu ni kiongozi wa serikali ktk bunge. hizo bado ni dalili kwamba bunge letu ni excutive dominated. lingine ni nafasi ya spika kutoa walao leadership katika mambo kadhaa. natambua bunge lina vyama na kiasi kuna competition. ninachoshindwa kujua ni pale spika anaposhindwa kuoffer leadership kwa masuala ambayo ukiyaona ni mambo tangible na very basic kwa maana ya kusaidia nchi na walau kuonyesha independence ya bunge. inawezekana kwa kanuni zao ni kweli maamuzi yanapitishwa kwa kuwahoji wabunge. lakini ni kweli kwamba spika hajui hata tofauti ya muhimili anaoongoza na muhimili wa serikali(excutive). katika muswada wa marekebisho ya sheria bungeni leo,mh.Tundu LIssu alitoa maoni yaliyokuwa yanataka wakuu wa mikoa wasiwe wajumbe kwenye bodi za ushauri za mahakama. hoja hapo ilikuwa ni kuweka separation of powers. ajabu spika ambaye muhimili wake ndo unatunga sheria na kwa maana ya kuonyesha superioty ya chombo chake na majibu rahisi kutoka kwa mwanasheria wa serikali(siyo mwanasheri wa bunge) akakubalia mswada kwa maana ya kipengele hicho kupita hata bila kutumia tu kinachoitwa natural wisdom mbali ya usomi wake na uzoefu lukuku tunaoamini anao. Au labda ni kwa sababu anatoka kwenye chama chenye serikali. na kama ni hivyo iko wapi independence na peculiarity ya bunge? je uko ndo kuongoza chombo huru kweli? au ni serikali all over? najua yeye anatoka chama tawala kuna wakati labda anataka kusaidia chama, lakini isiwe kwa mambo ambayo ni very basic katika kuweka misingi ya utawala bora na kuisaidia nchi. separation ni jambo ambalo kijana wa sekondari form two anajua iweje spika asijue? hebu aache ukeleketwa ambao tulio njetunaona kama unaiba hata hekima ya kawaida tu ya kufanya mambo. Bunge letu ni serikali au bunge kweli?
   
Loading...