KikulachoChako tumuombe sana Mungu tusije fika huku vita ni mbaya na madhara yake ni makubwa mnoTanzania ndiko tunakoelekea huko japokuwa speed ndogo sana kuelekea huko lakini tutafika tu huko...
KikulachoChako tumuombe sana Mungu tusije fika huku vita ni mbaya na madhara yake ni makubwa mno
KikulachoChako tumuombe sana Mungu tusije fika huku vita ni mbaya na madhara yake ni makubwa mno
Haya mambo hayaepuikiki Katika nchi ambayo dhuruma kwa wenye haki imekuwa ni jambo la kawaida.......katika nchi ambayo wezi wa mali ya umma wanabembelezwa kurudisha walichoiba bila ya kuangalia madhara waliosababisha.......Katika nchi ambayo wanaodai haki zao wanakamatwa na kung"olewa kucha na meno kwa bisibisi....katika nchi ambayo watoto wa walalahoi hawajui kesho yao matukio kama hayo hayashangazi.......katika nchi ambayo watawala wanagawana keki ya taifa wao na familia zao huku watawaliwa wakiishi chini ya dola moja haikuhitaji kuwa mnajimu mkuu kutabili machafuko......Katika nchi ambayo mwekezaji mgeni anathaminiwa kuliko mwekezaji mzalendo machafuko hayaepukiki.......katika taifa ambalo kiongozi wake mkuu hajui kwanini wananchi wake wanakabiliwa na umasikini kama sio ufukara ni vigumu kudumu kwa amani........katika nchi ambayo hakuna huduma za afya za uhakika katika vituo vya afya huku wananchi wakiwashuhudia viongozi wao wakienda kucheki afya zao nje ya tena kwa msururu wa magari...machafuko hayaepukiki......................KikulachoChako tumuombe sana Mungu tusije fika huku vita ni mbaya na madhara yake ni makubwa mno